Rufiji dam
JF-Expert Member
- Feb 20, 2020
- 3,804
- 8,798
CCM imekuwa na tabia ya kuleta maneno na kauli za ajabu sana. Nyerere alikuwa na vimisemo ambavyo vimekuwa vinadumaza sana akili zetu hasa neno kuwa Wananchi ni Wanyonge. Sijui alikuwa anasema Wajinga kwa kauli ya kificho. Zikaja kauli tofauti mpaka kuja kuitwa Malofa. Sasa hivi kumekuwepo na kauli ya Rais katoa pesa za miradi ya Maendeleo. Hii kauli imekuwa inatamkwa sana na Mawaziri wa hii Serikali na SSH nae anafurahia mpaka juzi kati hapa alisema kuna hela sijui kazipata wapi anaongezea kwenye ujenzi wa madarasa. Unajiuliza Rais anatamka hadharani kuna pesa kapata sehemu halafu anaileta nchini!? Bila hata kuhojiwa. Narudia tena tupinge hizi kauli za Rais kutoa pesa yeye hana pesa. Pesa ni za serikali na yeye ni mwajiriwa wetu awe wazi kusema pesa anatoa wapi kama ni zake.