Kama Star TV wamefunguliwa, tegemea maajabu ACACIA

Kama Star TV wamefunguliwa, tegemea maajabu ACACIA

Mkuu nimeona hapo mwishoni maswali yako kadhaa yenye kuhitaji majibu yaliyotukuka. Hivyo basi ili kupata majibu sahihi ya maswali yako ningekuomba kama ungeyafanya kwanza utafiti ili ujue hizo hela zimelipwa au bado na zimelipwa kwa account gani na benki gani.

Kuuliza maswali hapa sijui kama utapata ulichokitarajia Mkuu.
 
We mshana jr kama ulimuona Kayombo wa TRA anakutangazia wameifunga Star tv kwa kuwadai kodi, basi subiria huyo huyo atakuja kukupa maelezo kwa nini wameifungua au waulize TRA kwa nini wamefungua?
 
Sijivunii kuzaliwa Tanzania maana viongozi wote wanatetea matumbo ya wachache wenye nazo wakiacha wengi wakiumia na machungu ya umasikini. Huruma hakuna
 
Kwa hiyo unalinganisha hivyo vi-bilioni 4 vya TV na Trilioni 425 za ACACIA!!!????

mbona hujiulizi kuwa IPP media anadaiwa Bilioni 16 na TRA na AZAM anadaiwa Bilioni 40?
cha ajabu wanapo wadai hao wote wanatupa taarifa kuwa huyo tunamdai billion wengine trillion lakini hawatwambia wamezlipa? yaani umma aumbiwi washalipa . naunakuta shughuli zao zinafunguliwa na kuendelea hiki ndo kinacho ulizwa na umma na kama habar zilikuwa za kick pia mngetuarifu...
 
Ni mbinu fulani ya kimafia kuwapata unaowataka huku ukiupambaza umma kwa kuanzisha kampeni fulani, ambayo huanza kwa mbwembwe nyingi na mwishoni wakishapatikana watarajiwa mambo huisha kimyakimya.

Tumeyaona haya kwenye vita ya madawa ya kulevya(madaraka ya kulevya) nchi ikazizima ikawa ni kampeni ya safisha nchi/dar, wakakamatwa wa kukamatwa, tukaletewa na wahanga (watoto wadogo) wakatoa ushahidi kisha mambo yakaisha kimyakimya.

Limekuja hili la kodi, ambalo ni faraja ya wengi, tumechoka kuwa ombaomba wakati tuna kila kitu na wachache wanafaidi kwa kutolipa kodi, tunahitaji kodi ili kupeleka maendeleo ya nchi mbele, hospital ziwe na madawa na vifaa tiba, shuleni kukamilike, miundombinu iwe bora nk... Tunahitaji pesa.

Kufungiwa kwa Star TV ni kielelezo tosha kwamba hii vita haina macho ya makengeza. Walikuwa wanadaiwa BILLION NNE na ushee, kisha wakaja mabepari wa madini wakapigiwa mahesabu yaliyozua mijadala dunia nzima.

TRILLION 425 hivi, Hawa ni wezi bila kujali wana bei gani kibindoni! Walipe walichotuibia ili iwe fundisho kwa wengine.

Masikitiko yangu!
Je kodi iliyokwepwa kuiba ina mazungumzo? Kwamba kama ukikubali kosa basi upunguziwe ama usamehewe? Je star TV wamelipa ama wamepunguziwa au wamesamehewa? Kama wamelipa wamelipa bei gani? Kupitia akaunti gani? Kama kwa Star TV imekuwa hivi kwa ACACIA haiwezi kutokea? [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji144]

KILINGE leo kikavu hakuna wateja hakuna kabisa nakuja mjini kubangaiza chenchi za kodi

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwani siku TRA wanawafungia Star TV walikutangazia?? Kama unataka kujua anadaiwa kiasi gani na wamekubaliana nini si uende TRA ukapate maelezo kamili kuliko kuja kulalamika hapa JF. Pia fuatilia ITV, Azam, Channel 10, Clouds n.k wanadaiwa kiasi gani halafu utuletee hapa mkuu!!
 
Hii kitu inanipa mashaka inaeza kuwa mchezo wa kucheza na akili za watanzania, ili serikali ionekane inafanya kaz mwsho wa siku watu wanamalzana kimyakimya ,iwe kwa kupunguziwa deni au kusamehewa,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni mbinu fulani ya kimafia kuwapata unaowataka huku ukiupambaza umma kwa kuanzisha kampeni fulani, ambayo huanza kwa mbwembwe nyingi na mwishoni wakishapatikana watarajiwa mambo huisha kimyakimya.

Tumeyaona haya kwenye vita ya madawa ya kulevya(madaraka ya kulevya) nchi ikazizima ikawa ni kampeni ya safisha nchi/dar, wakakamatwa wa kukamatwa, tukaletewa na wahanga (watoto wadogo) wakatoa ushahidi kisha mambo yakaisha kimyakimya.

Limekuja hili la kodi, ambalo ni faraja ya wengi, tumechoka kuwa ombaomba wakati tuna kila kitu na wachache wanafaidi kwa kutolipa kodi, tunahitaji kodi ili kupeleka maendeleo ya nchi mbele, hospital ziwe na madawa na vifaa tiba, shuleni kukamilike, miundombinu iwe bora nk... Tunahitaji pesa.

Kufungiwa kwa Star TV ni kielelezo tosha kwamba hii vita haina macho ya makengeza. Walikuwa wanadaiwa BILLION NNE na ushee, kisha wakaja mabepari wa madini wakapigiwa mahesabu yaliyozua mijadala dunia nzima.

TRILLION 425 hivi, Hawa ni wezi bila kujali wana bei gani kibindoni! Walipe walichotuibia ili iwe fundisho kwa wengine.

Masikitiko yangu!
Je kodi iliyokwepwa kuiba ina mazungumzo? Kwamba kama ukikubali kosa basi upunguziwe ama usamehewe? Je star TV wamelipa ama wamepunguziwa au wamesamehewa? Kama wamelipa wamelipa bei gani? Kupitia akaunti gani? Kama kwa Star TV imekuwa hivi kwa ACACIA haiwezi kutokea? [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji144]

KILINGE leo kikavu hakuna wateja hakuna kabisa nakuja mjini kubangaiza chenchi za kodi

Sent using Jamii Forums mobile app
mshana jr kuwa kweli mkuu, vita vya madawa ya kulevya tulivi-dismantle wenyewe kwa ushabiki wa kijinga kabisa. Hatuna haja ya kulaumu wala kulalamika.
 
I doubt kama Star TV wamelipa..

Kwa jinsi sakata lao lilivyozungumzwa muda mrefu, kama wangekuwa wamelipa ingejulikana hapa..

" Mh Dialo sitakuangusha.. " JPM kwenye kampeni 2015.
Kilichofanyika ni kutafuta KIKI ili ionekane kwamba Serikali Inamaanisha kwenye kusaka KODI lkn zile ni SARAKASI za Kawaida tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom