Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,250
- 44,579
Na. M. M. Mwanakijiji
Kuchagua ni kuamua; kutokuchagua nako ni kuamua. Kuamua kuchagua au kuamua kutokuchagua yote ni kuamua kuchagua au kutokuchagua. Hivyo, uamuzi ni uchaguzi, na uchaguzi ni uamuzi. Kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba 29, 2025 Watanzania wanaitwa kufanya uamuzi na uchaguzi; au wachague kufanya uamuzi.
Sasa hivi inaonekana pendekezo lililo mbele yao ni kuamua kumchagua Rais Samia Suluhu Hassan aendelee kuongoza nchi yeye na chama chake cha Mapinduzi. Mpinzani wake mkuu ambaye angeweza kuleta upinzani wa kweli yupo "anaozea jela" kwa mashtaka ya uhaini. Mashtaka haya kama nilivyowahi kusema huko nyuma ni miongoni mwa mashtaka ya kijinga zaidi kuletwa na watu wanaoitwa "wasomi". Lengo la mashtaka haya na kuendelea kumshikilia Tundu Lissu jela ni kuwanyima nafasi Watanzania ya kufanya uamuzi na uchaguzi. Ni kuwa watakapoenda kupiga kura Watanzania hawataona jina la Tundu Lissu wala CHADEMA ambacho ni chama kikuu cha upinzani nchini.
Na hata kwa chama cha ACT Wazalendo ambacho nacho kilijitutumua kupata mgombea wa Urais mwenye jina linalojulikana Bw. Luhaga Mpina na wao wamejikuta kule kule. Jitihada zimefanyika na zinaendelea kufanyika kuhakikisha kuwa jina la Mpina halionekani kwenye kura za Urais. Watanzania pia wanakataliwa kufanya uamuzi na uchaguzi juu ya Mpina.
Ukiangalia kampeni nzito inayofanywa na mgombea wa CCM inabidi ujiulize swali moja tu; mahali ambapo CCM haina tishio lolote la Urais ni kwanini wanafanya kana kwamba mgombea wao ana mpinzani wa kumtisha? Yaani, inawezekana kweli kampeni hizi zote motomoto zinafanywa kushindana na Bi. Mwajuma wa UDM? Hivi, ni kweli kabisa wanataka kupata kura nyingi kwa mgombea wao wa Urais ili wajivune kuwa wameushinda upinzani wa Tanzania?
Kama nilivyosema kwenye makala yangu moja iliyopita siyo kwamba ingekuwa bora zaidi kwa Rais Samia kushinda dhidi ya Lissu "fair and square" kuliko kuonekana ameshinda dhidi ya Mwajuma "fair and square"? Katika hili inabidi twende mbali na kujiuliza - itakuwaje kama Watanzania wasiopenda yote yaliyotokea na wanataka sauti zao zisikike wakiamua wampigie kura za kususa Bi. Mwajuma wa UDM? Kama siyo Mwalimu wa CHAUMA na kwamba hakuna CHADEMA siyo kura zile za kususia uchaguzi ziende kwa Mwajuma?
Kuliko kuamua kutopiga kura na kususia uchaguzi; itakuwaje kama wananchi wakaamua kwenda kupiga kura za "maruhani" za kumchagua Mwajuma. Kama Mwajuma ameachwa kugombea Urais na hakuna mtu aliyeweka pingamizi lolote dhidi yake inamaana Bi. Mwajuma amekidhi matakwa yote na anaweza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kuna ubaya gani basi watu wakaamua kwenda kampeni za Bi. Mwajuma na kuwahamaisha wote wampigie kura za Urais?
Nauliza kama watu hawajapewa CHADEMA wala ACT-Wazalendo, Na kama hakuna matumaini ya kuichagua CHAUMA kwanini basi watu wasimue kupiga kura za kususa kwa Bi. Mwajuma wa UDM? Hivi itakuwaje matokeo ya uchaguzi yakaanza kuonesha Bi. Mwajuma akipata kura nyingi kuliko ilivyotarajiwa na hivyo kupunguza kura za Rais Samia na hivyo angalau inaonekane kuwa Rais Samia hakushinda kiulaini tu.
Kwanini wanaopinga uchafuzi uliofanyika kwenye uchaguzi huu hadi hivi sasa wasiamue na wenyewe kuongeza uchafuzi kwenye uchaguzi uliochafuka? Kwanini watu wasiende na Mwajuma?
Si kuchagua ni kuamua na kuamua ni kuchagua? Ila Bi. Mwajuma jamani.. si macho yake yanahamasisha kupiga kura?