Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria, ongoza kwa 'presidential decrees'!

Mr pasco. hii nchi haiwezi kwenda bila dictator hata kidogo. wacha afanye aonavyo yeye yafaa ila wananchi tunufaike. unadhani sisi wananchi wa kawaida inatusaidia nn hiyo democrasia kama haijibu matwakwa yetu. go go go MR PRESIDENT.
 
Wanabodi,
Tanzania ni nchi inayofuata utawala wa sheria, hivyo itaongozwa kwa mujibu wa sheria taratibu na kanuni!, no one is above the law!. Katika kufuata sheria hizo, taratibu na kanuni, pia kuna mamlaka ambayo katiba imempa rais wetu wa JMT kuyatekeleza at his pleasure, yaani vile rais atakavyoona inafaa, ikiwemo presidential appointments powers, and the power to hire and fire civil and public servants!.

Hata kama Dr. Magufuli ni rais wetu, haina maana ana inherent powers kuamua chochote na watendaji walio chini yake kazi yao ni kusema tuu 'YES!", "ndiyo mzee!". Ila kwa hali ninayoina sasa, jee kuna ubaya tukimshauri rais wetu, kamu huu Sio Udikiteta?!, then ni bora sana, Mhe. Rais aka "Futilia Mbali Utawala wa Sheria kwa muda, akaiweka pembeni katiba, kwa kuamua kutangaza hali ya hatari, na badala yake akuamua kuongoza kwa kutumia Presidential Decrees!, yaani kina anachokotaka rais na kukisema kinaandikwa na kinakuwa sheria!, kiukweli atafanikiwa sana kuinyoosha nchi hii ambayo imepinda sana!.

Mnaonaje mkiungana na mimi, tumshauri rais wetu ili kuyanyoosha mambo yake vizuri, awe na mamlaka ya kufanya kila anachotaka, mnaonaje kama tutamshauri asitishe utawala wa sheria kwa muda, badala yake aongoze kwa kutumia presidential decrees pekee?!.

Mungu Ibariki Tanzania,
Mungu Mbariki Rais Wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli.

Paskali
Nabandiko hili, inawezekana huku kuzuia
1. Bunge Live
2. Naibu Spika wa kupachika mwenye udikiteta uliopindukia!.
3. Nyamazisha wabunge vocal au"viherehere" kwa kuwatimua bajeti ipite kwa ulaini!.
4. Zuia mikutano na harakati za kisiasa!.
5. Ingilia freedom of expression kwa kuwashitaki watu hovyo ili kuwaogofya!.
6. Timua waziri mmoja kwa kumsingizia ulevi, wakati hakuna kipimo chochote kilichofanyika kulithibitisha hilo!.
7. Muendelezo wa tumbua tumbua usiofuata sheria, taratibu na kanuni!.
8. Tujiandae kuminywa kwa freedom of the press
9. Tujiandae kwa kufungwa kwa jf
10. Dalili ya mvua ni mawingu!, jee inawezekana hizi ni hatua za awali za kufuatwa kwa ushauri wa bandiko hili?

Pasco
Anko Magu alikuelewa sana na anafanyia kazi ushauri wako mzuri.

"Bosi mtata amekuja" - Sizonje
 
Wahenga walisema isipokufa haizai; huenda pia ni kweli Tanzania ya kale isipokufa mpya haiwezi kuzaliwa. Tukubali kuinywa sumu ilimradi inahuisha; anachofanya Magufuli ni sumu kwa wengi, maisha yatatetereka, mazowea yatakoma hata yale tunayoyapenda sana. Bunge litaonekana kama sio lenyewe linaburuzwa, demokrasia itaonekana inahujumiwa, nk. hilo ndilo tanuru la moto; natung'ate meno tupite humo kwa uchungu kwa manufaa ya kesho. Mradi wote tunakubali tumepata jembe, basi tuweke tumaini letu sote hapo. Wote tumuunge mkono, tukae nyuma yake, tuone anatufikisha wapi; hili lisijalishe upinzani wala jumuia za kijamii. Kiongozi wetu jembe anayo maono, si vyema kukwazwa na vibwagizo vya demokrasia za majukwaani au makelele ya kila uchao hata hajapata wasaa wa kusimamisha agenda yake na mizizi kuota. Tena ingefaa siasa za majukwaani zikome kwa mwaka mzima au hata miwili; kama jembe anatufikisha kwa njia ya mkato shida iko wapi? demkrasia ni njia na udikteta ni njia pia, lakini ya mkato. Suala hapa ni kufika na kama hatufiki si itakujaonekana tu? si kila mwananchi atajionea mwenyewe? kuna haja gani kuwalazimisha watu kuvuka daraja ambalo hawajalifikia? Watanzania sio wajinga wa kufanya kujulishwa matatizo yao; wanayajua kama yapo
 
Ndani ya miaka 5 tunahitaji kupitia mifumo yote ya tawala za dunia, udikteta ni mojawapo.
Ni Kweli kuwa udikteta wa Kujali watu maskini unawahudhi mabepari wachache madikteta.
Toka enzi ya Mzee Mkapa madikteta wamekuwa wengi si tu kwa sekta za umma bali kwenye vyama vya siasa,NGOs,sekta Binafsi na nk. wote hawa wamejifanza miungu watu na kujiita wawekezaji.
 
Wanabodi,
Mnaonaje mkiungana na mimi, tumshauri rais wetu ili kuyanyoosha mambo yake vizuri, awe na mamlaka ya kufanya kila anachotaka, mnaonaje kama tutamshauri asitishe utawala wa sheria kwa muda, badala yake aongoze kwa kutumia presidential decrees pekee?!.
Mungu Ibariki Tanzania,
Mungu Mbariki Rais Wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli.

Paskali
Wajameni, ushauri huu si ni bado uko valid?, mnaonaje, tukiungana kumshauri rais, aiweke pembeni katiba kwa muda, ili isimkwamishe, na badala yake atumie presidential decrees kuinyoosha nchi hii, ikiishanyooka ndipo tuirudie katiba?!.

Paskali
 
Magufuli acha woga wa kujifichaficha nyuma ya vyombo vya usalama, kama wewe ni jasiri tangaza hali ya hatari upate uhalali wa kutawala kiimla.

Kama wewe ni jasiri, achana na udikteta uchwara, watangazie raia wa taifa hili kuwa nchi iko chini ya dikteta hivyo haki zao za msingi zimefutwa.

Achana na amri za kukurupuka na mihemko na hivyo kufanya vyombo vyetu vya usalama kulazimika kuvunja sheria kwa kutii amri batili.

Katiba yetu inakuruhusu, hivyo jipe madaraka kikatiba ufanye unavyotaka na hakuna mwananchi atayekulaumu...
Mkuu Mag 3, nimekuleta hapa maana kwa kiasi fulani tunafanana!.

Pasco
 
Wanabodi,

Tanzania ni nchi inayofuata utawala wa sheria, hivyo itaongozwa kwa mujibu wa sheria taratibu na kanuni!, no one is above the law!. Katika kufuata sheria hizo, taratibu na kanuni, pia kuna mamlaka ambayo katiba imempa rais wetu wa JMT kuyatekeleza at his pleasure, yaani vile rais atakavyoona inafaa, ikiwemo presidential appointments powers, and the power to hire and fire civil and public servants!.

Hata kama Dr. Magufuli ni rais wetu, haina maana ana inherent powers kuamua chochote na watendaji walio chini yake kazi yao ni kusema tuu "'YES!", "ndiyo mzee!". Wasaidizi wa rais, wanawajibu wa kumsaidia rais kjutimiza majukumu yake kwa mujibu wa katiba kama alivyoapa kuilinda na kufanya kama anavyojisikia yeye!.

Kwa hali ninayoina sasa, Magufuli anakoelekea, asipodhibiwa, very soon kuna watu sio tuu watalia, bali tutaumia!. Jee kuna ubaya tukimshauri rais wetu, kama huu Sio Udikiteta?!, then ni bora sana, Mhe. Rais aka "Futilia Mbali Utawala wa Sheria kwa muda, akaiweka pembeni katiba, kwa kuamua kutangaza hali ya hatari?!", na badala yake akuamua kuongoza kwa kutumia Presidential Decrees!, yaani kina anachokitaka rais na kukisema kinaandikwa na kinakuwa sheria!, kiukweli akilifanya hili, atafanikiwa sana kuinyoosha nchi hii ambayo kiukweli imepinda sana!.

Rais alipoamuru zile pesa "private money", zilizochangwa na private entities, zikiwemo public corporation, kama sehemu yao ya CSR kuwakirimu wabunge wapya kwa mlo wa usiku!, alitumia sheria gani na mamlaka gani?!. Yaani rais anaweza kuamuru private money toka private entities watumieje fedha zao?!, kwa mamlaka ipi!?, kupitia sheria ipi, kanuni ipi na taratibu zipi?!. Huu kama sio udikiteta ni nini?!. Rais anafanya udikiteta anashangiliwa?!, ni Tanzania pekee!.

Rais alipoamua hayo, wengi wameishia tuu kusifu, kushangilia na kupiga makofi, hakuna aliyejiuliza, au kuhoji, rais ametoa agizo hilo kwa mamlaka gani?!, alafu hapa tukisema Magufuli ni dikiteta tutakuwa tumemuonea?!.

Nijuavyo mimi japo rais ni rais wa nchi, na ndiye mamlaka kuu ila hiyo mamlaka sio kwenye kila kitu bali kwa kupitia chaneli rasmi, mfano serikali ina mihimili mitatu, serrikali, bunge na mahakama, sasa ni kwenye serikali kuu na serikali za mitaa pekee, ndiko rais ana mamlaka kuu ya "inherent powers", ambayo ni mamlaka kamili yanayoitwa "eyes on and hands on", anaweza kufanya lolote bila kuulizwa na yeyote!. Serikali ni yake anaweza kuifanya vyovyote apendavyo.

Kwa mhimili wa bunge na mahakama, rais pia ana mamlaka ya eyes on na hands on, only through wakuu wa mihimili hiyo, mahakama kupitia kwa Jaji Mkuu, na Bunge kupitia kwa Spika, hii inamaanisha rais hawezi kuamua jambo linalolihusu Bunge bila kupitia kwa Spika, au Jambo linaloihusu mahakama bila kupitia kwa Jaji Mkuu, mfano lile katazo la kuwakataza watumishi wa umma kusafiri nje bila kibali cha chake kupitia kwa Katibu Mkuu Kiongozi, lilipaswa kuuhusu mhimili wa serikali tuu, mhimili wa Bunge waombe kibali kwa Spika kupitia kwa Katibu wa Bunge na mhimili wa Mahakama uombe kibali kwa Jaji Mkuu kupitia kwa Msajili wa Mahakama!. Kitendo cha Spika na Jaji Mkuu kutakiwa kumpigia magoti Katibu Mkuu Kiongozi, sio tuu ni dharau kwa viongozi hao, bali ni mkuu wa mhimili mmoja kuingilia mihimili mingine!, huu pia ni udikiteta ulionyamaziwa!.

Tunapokuja kwenye mashirika ya umma na makampuni , hizi japo zinamilikiwa na serikali, ni private bodies, zenye mamlaka zake zinazojitegemea kupitia bodi zake, hivyo mamlaka ya rais ni "eyes on, hands off", serikali inaweza kuchungulia tuu kile kinachoendelea ndani ya taasisi hizo, kwa rais kuwateua wakuu wa taasisi hizi na wenyeviti wa bodi, na sio kutia mkono nani ya uendeshaji wa taasisi hizo. , ikibidi kutia mkono then ni kupitia kwa wizara husika, kuilekeza bodi husika kuileza menejimenti ya shirika husika au kampuni husika!.

Mashirika haya yanatenga fungu fulani za kufanya shughuli za CSR ili ku achieve specific objectives fulani kwenye strategic plans zao!. Kama Bunge ambalo ni taasisi huru na mhimili unaojitegemea, liliomba udhamini wa sherehe ya mlo wa usiku toka kwenye mashirika na makampuni, kisha mashiika na makampuni hayo wakaona ombi la bunge lina fit kwenye zile CSR zao, wakatoa fedha zile, rais anakuwa hana mamlaka kabisa ya kuingilia bunge na kuamuru different use ya private money?!. Rais alichofanya ni udikiteta tuu na ubabe tuu.

Hata kama rais ameona matumizi yale yalikuwa ni anasa tuu, hana mamlaka ya kuliingilia bunge, bali ana uwezo wa kumuita Spika na kumuomba Bunge likatae fedha za michango hiyo, na kuzirudisha kwa wenyewe waliochanga ili zipangiwe CSR nyingine, na rais kama rais alihitaji hizo fedha zipelekwe kuhudumia wagonjwa Muhimbili wenye uhitaji mkubwa zaidi wa vitanda kuliko mlo wa wabunge, rais naye angeomba fedha hizo toka mashirika au taasisi hizo kama wanavyofanyaga kuomba fedha kuifadhili CCM nyakati za uchaguzi!, lakini sio kuliingilia bunge na kuamuru hayo matumizi mengine kwa fedha hizo, au bunge baada ya kuipokea michango hiyo, bunge ndilo lingeamua badala ya kufanyia sherehe, wakanunulie vitanda vya wagonjwa lakini sio rais kutoa amri kuingilia mihimili mingine!, huu ni udikiteta!.

Baada ya kufanikiwa kwenye hili na kupongezwa, leo rais wetu ameibuka na jingine kubwa zaidi, hili ni kufuta paredi ya uhuru!. Swali ninalojiuliza hivi kumbe paredi ya uhuru ni miongoni mwa sherehe zinazoadhimishwa at the pleasure of the president?!. Nilifikiri hii ndio the no 1 state event na ipo kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni?!, hivi ni kweli rais wa nchi anaweza tuu kuamka asubuhi na kuamuru maandimisho ya paredi ya uhuru yafutwe kwa kauli ya mdomo just like that?!, na watu wemenyamaza?!. Japo rais anayo mamlaka kuifuta public holiday yoyote na kuigeuza ni siku ya kazi, au kuitangaza siku yoyote kuwa ni siku ya mapumziko, tangozo hilo hutolewa kwa a decree, tarifa ya rais kuifuta paredi ya uhuru, haina decree yoyote!. Hata kama rais anayo mamlaka hayo kikatiba, hawezi kuamka tuu asubuhi na kutoa tamko, bila decree!, sasa kitakachofuatia tamko hili, ndipo decree itatayarishwa na kuwa backdated, kisha Kurugenzi ya Mawasiliano itatuleta hiyo decree siku nyingine!. Hili likitokea, nauita ni uhuni!.

Mnaonaje mkiungana na mimi, tumshauri rais wetu ili kuyanyoosha mambo yake vizuri, awe na mamlaka ya kufanya kila anachotaka, mnaonaje kama tutamshauri asitishe utawala wa sheria kwa muda, badala yake aongoze kwa kutumia presidential decrees pekee?!, mambo yakiisha tengamaa, ndipo turudishe utawala wa sheria?!.

Najua kuna watu humu wanaweza kulitafsii bandiko langu hili na chuki binafsi!, nawaomba sana wanisome hapa!, mimi ni mmoja wa waliosema kuwa Mgombea wa CCM atakuwa ni John Pombe Magufuli tena kwa sababu maalum. Angalia kwa makini bandiko hili ni la lini

Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 ni John Pombe Magufuli-Aug 15, 2014
Na baada ya CCM kumpitisha rasmi Magufuli, nilipandisha bandiko hili
Ushauri wa Bure Kwa Lowassa: Kwa Vile ni Magufuli, Kubali Yaishe!.
Na baada ya ushindi wa Magufuli, nilipandisha uzi huu
Ushauri Wa Bure kwa ENL, Chadema na UKAWA, Tukubali Kushindwa, Tuyakubali Matokeo...
If You Can't Beat Them, Join Them!, He is a Worst Dictator!.

Rais Magufuli ni Simple, Genuine & Down To Earth-He is Simply "A Man of The People!".
Magufuli Kama Nyerere:Ni Mtu wa Watu, Hapapasi, Hamung'unyi, ni vitendo Bila Kuchelewa!.
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kweli Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?!.
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata ...
Mungu Ibariki Tanzania,
Mungu Mbariki Rais Wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli atimize majukumu yake kwa mujibu wa katiba.

Paskali
Hii ni rejea kuhusu the doctrine of separation of powers.

Bwana Mayalla

Mimi siyo mwanasheria ila ninaomba nikuulize.

Jee zile pesa zilikusanywa[pokelewa] na nani? Jee wahusika yaani waliotoa na waliolengwa walilalamika kuhusu hilo? Hivi yale matumizi ya pesa hizo hayakuwa na manufaa kwa umma?

Kuhusu mashirika ya Umma si sahihi kusema kuwa ni private bodies, zile ni parastatals ambazo zote ziko chini ya hazina.

Kwa dhana yako ya 'hands off' kumekuwa na matumizi mabaya sana ya ‘resources’ za mashirika haya kiasi cha kutisha kutokana na uhuru vilivyopewa.
Kingine ni kwamba mashirika haya yameundwa kwa pesa za umma na yalipewa uhuru wa kujiendesha ili kuepukana na bureaucracy ya central govt hata hivyo ilitarajiwa kuwa serikali ingekuwa inapata dividends kutoka haya mashirika lakini kinyume chake ni kwamba mengi yalikuwa hayafanyi vizuri na mengi yalitegemea misaada toka hazina.
Uamuzi wa serikali kuamuru mashirika haya kuhamishia pesa zao BOT ni sahihi ni ilikuwa hivyo hapo mwanzo kwani riba yote itokanayo na pesa hizo hujulikana na hudhibitiwa [siyo kama wale walioweka pesa za umma kwenye fixed deposit kwa interest ndogo kuliko iliyoko sokoni]

Unadai kuwa mashirika haya yalikuwa na SP na BP zao lakini hebu niambie ni shirika gani limefanikiwa kutekeleza hizo SP na BP katika kipindi cha miaka 5? Mbona sijakusikia yale mashirika ya umma ambayo yalifikia kufanya mikutanyo yao ya bodi nje ya nchi?

Central Govt ina haki ya kuingilia kati kwenye mashirika yake na mara nyingi taarifa hizi hufikishwa bungeni kama utaratibu ulivyo na kama kuna malalamiko yoyote yale basi hiyo ilikuwa ni kazi ya wabunge na bunge lao ambapo mimi kwa maoni yangu wamekuwa wakifanya kazi nzuri sana,

Kuhusu kufuta au kupunguza gharama za sherehe za umma sioni tatizo kabisa kwani kwenye mazingira haya tuliyonayo haitii maana kuendekeza anasa za kiasi hicho huku wanafunzi hawana madawati, hospitali hazina dawa. Bajeti ya matumizi ya pesa hizi ilipangwa na serikali iliyopita hivyo sioni ubaya wa alichokifanya kwa niaba yetu [walipa kodi]

Na hata hivyo taratibu za kupeleka bungeni mabadiliko ya matumizi ya pesa hizo hupelekwa huko na huridhiwa na sijasikia wabunge wakilalamika.

Nchi hii ilifikia mahala pabaya na ukweli ilitakiwa rais kama JPM ambaye kwanza hashibikii cheo hicho , haogopi kufanya maamuzi magumu na ndiyo maana sijawahi kuona survey yoyote ile ambayo imefanya kutathmini utendaji wake kuwa chini ya 60%.

Tuacheni unazi, right or wrong serikali hii imebidi ifanye hivi ili kuinusuru nchi yetu.Kwa miaka hii haiwezekani kwa nchi ya kidemokrasia kuendeshwa kwa decree lakini kwa kweli hata ingekuwa hivyo ingekuwa sawa tu maana tulikuwa tumejisahau tukatengeneza mamilionea wezi kwa gharama ya wananchi?
Umesahau kuwa laxity ilizalisha mtu kuwa na uwezo wa kutengeneza m7 kila dakika kwa kuiibia serikali???

Naomba uchangiaji kwenye hili usijikite kwenye matusi na kejeli tuchangia kama vile motto ya JF 'those who dare speak'

Nawasilisha
 
Mkuu Abunuwas, kwanza naunga mkono hoja, hayo yote anayoyafanya, anayafanya kwa nia njema, yaani in good faith, lakini jee, amefuata sheria, taratibu na kanuni? .

Hili la taifa hapa lilipofika, tulimuhitaji sana mtu kama Magufuli, na hili nimelizungumza hapa,

Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!

Jambo la msingi ni is he doing the right thing at the right time and doing it right? .

Utumbuaji Majipu wa Rais Magufuli: Is It A Right Thing, At The Right Time, And Doing It Right, Or ?!

Pascal mimi ninakuelewa sana ila hata kama style yake kuna wakati ina ukakasi wa aina fulani lakini inabidi awe hivyo.
Ninaelewa pia concern yako kwamba mazoweya ya kukubali hali hii inaweza kutupeleka pasipo.Mimi ninadhani tungekuwa tunatoa alternative options kuliko kukosoa tu bila ya kutoa options hizo.
Can you imagine in a major port like dar 65 ships vanishing without a trace. Ufisadi umezunguka kwenye maeneo yote kama cancer na kila anapogeuka anakuta hali mbaya zaidi kuliko sehemu nyingine.
Ukweli ni kuwa mimi ninamuonea huruma sana maana amerithi nchi ambayo ina potential kubwa lakini umafia umeingia kwenye kila scope ya utendaji kiasi kwamba kutumia conventional means inakuwa ngumu.
Hata hivyo mimi ninavyofahamu kuwa yote haya tutayapata kwenye kikao cha bajeti Ambapo mapato na matumizi ya serikali yatatolewa na hapo ndipo tutakapo fahamu kama alivunja kanuni za matumizi. Hivi si tunafahamu kuwa rais anaweza kuwa impeached akiwa anavunja sheria? Sisi ambao tuko nje hatuoni vizuri lakini ningefurahi sana kama mbunge yoyote yule ambaye ni mwana JF angetusaidia
 
Mkuu Abunuwas, kwanza nakubaliana na wewe kabisa kuhusu ukosoaji kwa rais wetu mpendwa Mhe Dr John Pombe Joseph Magufuli, ufanyike constructively kwa nia njema ya kujenga na sio kubomoa kwa kukosoa tuu bila kuendekeza the right thing to do.

Hili la ukosoaji, pia nimeisha wahi kulizungumzia humu

Mwito Kwa Wana JF Kuhusu Ukosoaji wa Rais Magufuli

Paskali
 
Mkuu Abunuwas, kwanza naunga mkono hoja, hayo yote anayoyafanya, anayafanya kwa nia njema, yaani in good faith, lakini jee, amefuata sheria, taratibu na kanuni? .

Hili la taifa hapa lilipofika, tulimuhitaji sana mtu kama Magufuli, na hili nimelizungumza hapa,

Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!

Jambo la msingi ni is he doing the right thing at the right time and doing it right? .

Utumbuaji Majipu wa Rais Magufuli: Is It A Right Thing, At The Right Time, And Doing It Right, Or ?!
Paskali

Mkuu Paskali

Heshima kwako.

Kwanza nikubaliane na hojaji yako kwamba: Je utendaji wa Mh Raisi Magufuli unazingatia sheria na taratibu za nchi? Hakika hii ni hojaji matata. Tena ni hojaji endelevu.

Hata hivyo ishara za utendaji wake zinaonesha kwamba Mh Raisi Magufuli hafuati sheria kwenye baadhi ya maeneo ya utendaji wake. Huu ni ukweli. Ukweli Usemwe. Maana Msema Kweli ni mpenzi wa Mungu.

Ukweli mwingine ambao lazima usemwe umo kwenye hojaji hii: Je, kuna manufaa gani nchi ilipata kwa utendaji uliozingatia sheria uliofanywa na maraisi waliomtangulia Mh Raisi Magufuli?

Kimsingi hojaji hii ya pili ilipaswa iitangulie hojaji ya Paskali ili tupime vizuri faida na hasara za Maraisi wetu kutumia sheria. Maoni yangu ni kwamba sheria zetu hazijashiba sawa sawa. Ndiposa ni lazima, narudia, ni lazima sana kuwa makini tunapochagua vipimo na viashiria (measures and indicators) vya utendaji wa Mh Raisi.

50thebe
 
Mkuu 50Thebe,
Heshima mbele.
Naunga mkono hoja.
Paskali
 
Mkuu Abunuwas, kwanza nakubaliana na wewe kabisa kuhusu ukosoaji kwa rais wetu mpendwa Mhe Dr John Pombe Joseph Magufuli, ufanyike constructively kwa nia njema ya kujenga na sio kubomoa kwa kukosoa tuu bila kuendekeza the right thing to do.

Hili la ukosoaji, pia nimeisha wahi kulizungumzia humu

Mwito Kwa Wana JF Kuhusu Ukosoaji wa Rais Magufuli

Paskali
I salute you sir
Ps Wanajamvi, sababu kubwa ya kuingia JF ilikuwa ni. Ninaomba tulirudishe jamvi letu liwe kama linavyostahili.
 
Mkuu Paschal yote haya uliyasema mapema kwa utashi na maono makubwa lakini shida ni hii nani ataongea ukweli kama huu mbele ya jamii pasipo kutiwa nguvuni?Time will tell........big up
 
Back
Top Bottom