Kama sio Mwalami basi angeniua mbwa yule

Kama sio Mwalami basi angeniua mbwa yule

DK Mweluvu

Member
Joined
Mar 3, 2020
Posts
92
Reaction score
135
Salaam wanabodi

Aisee katika pitapita za mjini nikakutana na zile Gereji za barabarani. Yaani magari yanapaki beside barabara na fundi gereji wanaendelea na matengenezo kama kawaida.

Sasa mimi na haraka zangu nikashika bonet ya gari moja(Difenda)Bonet ilikuwa wazi na fundi anaendelea na matengenezo. La haulaa bonet ikashuka na kumponda fundi na mnajua vile bonet ya difenda imejaa chuma ni nzito haswa sio kama hizi za spacio, crown za Extrovert mnaelewa wakuu.

Basi bwana fundi yule akatoka mbele kajaa sumu, kanuna sura imevimba kama Andazi la mama bonge wa buza. Na jamaa ni pande la mtu kama JITU LA MIRABA MINNE sijakaa sawa jamaa akaniweka kitasa ni Ndoige moja nzito nikawa nahisi niko dunia mpya. Kabla sijapoa akasukuma ngumi nyingine hapo nishalewa kama mlevi wa gongo za kisukuma.

Bado sijatulia sina akili hata moja kama Chizi Maarifa nikasikia sauti za wamama wanalia "Jamani utauaa" kwani lile jamaa linaelewa sasa? Nikasikia tena "Mwalami mshikeni jamani uwiiii" Apo namimi nishavimba kama vitumbua vya mama musa wa sahara.

Basi huyo Mwalami ndo akalishika lile jitu na mafundi wengine wakaongezeka ndio wakalimudu kulizuia. Nami akili zikaanza kurudi moja baada ya moja

Kilichofata:
Narudi hapa. Ngoja mama chanja anikande Uso kwanza. Nimemwambia nimeangukia meza uko kazini kaniamini. Angejua vitasa nilivyochezea.....

Nawasilisha.
 
images (4).jpeg
 
mm naomba kujua kama maeneo yale utapita tena ama vp? Pole sana. Wanaume tumeumbwa Mateso. Hayo nayo ni Mateso
 
Back
Top Bottom