MTK
JF-Expert Member
- Apr 19, 2012
- 8,927
- 6,850
Namtofautisha G. Lema na wanasiasa bali mwanaharakati aliyekamilika. Mtu mwenye uwezo wa kuhoji chochote bila kuogopa mtu.
Nakumbuka alihoji kushinda kwa kesi ya Zombe bungeni, Ulongo wa waziri mkuu na kuwasihi polisi kuangalia uma zaidi ya watawala. Hakukubali uhuni kwenye uchaguzi wa meya wala mwafaka wa kijinga.
Pili anamsimamo kitu ambacho wanasiasa wengi wanakikosa. Pamoja na kuvuliwa ubunge na kujaribu kuvutwa Lema yuko palepale. Ni tofauti sana ona wanasiasa kama Kafulila na Hamadi wabunge wa mahakama walivyopoa wakimwangalia JK Kwa jicho la upole ili aongee na majaji vizuri. Unamkumbuka Zito wa awali na yule wa baada ya kuwekwa kwenye Tume ya kuchunguza mikataba ya madini. Tume ile ilifanya kazi moja tu kumnyamazisha kabisa zito na kumuweka karibu na JK Na ilifanikiwa 100%.
Namfananisha na hayati Chacha Wangwe. Aliwahi kukataa dhamana kuwa bora afie jela kwani mikesi imekua mingi na inampotezea muda. Lema hana kiburi bali anamsimamo
Kikubwa zaidi hana papara kama wengi wanavyozani ndiomaana wakatiwote si mtu wa kutumbulia macho madaraka makubwa ndani ya chama au nchi yake japokuwa anajina na uwezo mkubwa. Kama ilivyo kwa Zitto au M.
Sijui elimu yake lakini ata kama ni form 4 poa tu kwani kawawa alikuwa waziri mkuu
hakuna mwanasiasa aliyehimili mikikimikiki kama G. Lema. John Mnyika sawa ila hana madhara kwenye harakati na hajapata misukosuko tukampima.
Nchi hii imejaa wezi wa mali ya uma na wanaiba waziwazi bila kificho tunaitaji mtu anaweza kukemea waziwazi bila kutumia nahau au tafsida. Mtu mwenye msimamo mkali na mzalendo kama G. Lema.
Kinachotakiwa kwa Tanzania mama yetu tunayoipenda ni uongozi wa kizalendo na utashi wa kuwahurumia na kuwatumikia wananchi, kama ikibidi GJL ateuliwe kuwa mgiombea wa urais 2015, sifa za utashi wake wa kuwapigania wanyonge anazo kede kede, So be it! CV za page 10 na shahada magumashi hazimsaidii lolote nyaya yangu kule kanyigo BK, hebu tafakari kidogo kuhusu PAUL CHIZI wa ATCL, ni mtaalamu kweli kweli, CV kabambe lakini je sare za warfanyakazi 15 tu kwa shilingi milioni 80 kweli????????????????????????????!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Eh Mungu inusuru Tanzania yetu.