Kama sio DR. Slaa, Godbless Lema ndiye Rais 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama sio DR. Slaa, Godbless Lema ndiye Rais 2015

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by William Mshumbusi, Jun 6, 2012.

 1. William Mshumbusi

  William Mshumbusi JF-Expert Member

  #1
  Jun 6, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 874
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Namtofautisha G. Lema na wanasiasa bali mwanaharakati aliyekamilika. Mtu mwenye uwezo wa kuhoji chochote bila kuogopa mtu.
  Nakumbuka alihoji kushinda kwa kesi ya Zombe bungeni, Ulongo wa waziri mkuu na kuwasihi polisi kuangalia uma zaidi ya watawala. Hakukubali uhuni kwenye uchaguzi wa meya wala mwafaka wa kijinga.

  Pili anamsimamo kitu ambacho wanasiasa wengi wanakikosa. Pamoja na kuvuliwa ubunge na kujaribu kuvutwa Lema yuko palepale. Ni tofauti sana ona wanasiasa kama Kafulila na Hamadi wabunge wa mahakama walivyopoa wakimwangalia JK Kwa jicho la upole ili aongee na majaji vizuri. Unamkumbuka Zito wa awali na yule wa baada ya kuwekwa kwenye Tume ya kuchunguza mikataba ya madini. Tume ile ilifanya kazi moja tu kumnyamazisha kabisa zito na kumuweka karibu na JK Na ilifanikiwa 100%.

  Namfananisha na hayati Chacha Wangwe. Aliwahi kukataa dhamana kuwa bora afie jela kwani mikesi imekua mingi na inampotezea muda. Lema hana kiburi bali anamsimamo

  Kikubwa zaidi hana papara kama wengi wanavyozani ndiomaana wakatiwote si mtu wa kutumbulia macho madaraka makubwa ndani ya chama au nchi yake japokuwa anajina na uwezo mkubwa. Kama ilivyo kwa Zitto au M.

  Sijui elimu yake lakini ata kama ni form 4 poa tu kwani kawawa alikuwa waziri mkuu

  hakuna mwanasiasa aliyehimili mikikimikiki kama G. Lema. John Mnyika sawa ila hana madhara kwenye harakati na hajapata misukosuko tukampima.

  Nchi hii imejaa wezi wa mali ya uma na wanaiba waziwazi bila kificho tunaitaji mtu anaweza kukemea waziwazi bila kutumia nahau au tafsida. Mtu mwenye msimamo mkali na mzalendo kama G. Lema.
   
 2. Havizya

  Havizya JF-Expert Member

  #2
  Jun 6, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,573
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Ubarikiwe mtoto wa Lema Godbless.
   
 3. MNAMBOWA

  MNAMBOWA JF-Expert Member

  #3
  Jun 6, 2012
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,983
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Hata kama ni uhuru wa mawazo urais c wa majaribio angalia sana kumpa mtu dhamana ya
   
 4. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #4
  Jun 6, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,945
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  ni godbless na wala siyo godsbet
   
 5. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #5
  Jun 6, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  Tuna tatizo sana Tanzania, rais ni zaidi ya uanaharakati

  Ni sawa na kusema Che Guevara awe rais etc

  Mimi Lema ningesema awe waziri wa wizara sugu na awe anarotate kwenye kazi
   
 6. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #6
  Jun 6, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  yote hii ni kwa sababu ya JK..yaani ameufanya urais umekuwa rahisi mno kuupata na hata kuufikiria kuupata...
   
 7. J

  Johnbosco Mligo Member

  #7
  Jun 6, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hongera kwa kumsifu mtu akiwa hai. Maana watu wetu wamezoea kumsifu mtu akiwa kwenye Jeneza. tukiwa na raisi wa namna hii nchi hii itakwenda!
   
 8. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #8
  Jun 6, 2012
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,074
  Likes Received: 1,811
  Trophy Points: 280
  Naheshimu mawazo yako mr mshumbusi... but yapo far away from reality
   
 9. Comi

  Comi JF-Expert Member

  #9
  Jun 6, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 3,347
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  Lema anafaa kuwa aidha waziri mkuu au waziri asiyekuwa na wizara maalum kwani akiwa rais ni ngumu sana yeye kuwa mtendaji mkuu
   
 10. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #10
  Jun 6, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Mkuu mshumbushi hata Mimi nipo CDM lakini wewe unataka kuleta matatizo na hii thread Ngoja wakina Ritz , Zomba , mafilili na Rejao waamke upambane nao mwenyewe Mimi sitii tena mouse yangu kwenye hii thread
   
 11. William Mshumbusi

  William Mshumbusi JF-Expert Member

  #11
  Jun 6, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 874
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Wanaowaza uraisi na madaraka ndani au nje ya CHADEMA huu uzi utawauzi sana au kuwagombanisha na Lema.

  Nimeangalia hali ya nchi ilipofikia. Nani mwenye ujasiri na akipata bunduki anaweza kumuua nyani kwa kumwangalia usoni.

  Zitto haaminiki uliza aliosomanao chuo alivyowageuka wenzake na kupuuza madai ya wanachuo baada ya kupata madaraka chuo kikuu.

  John mnyika ni mtulivu na busara lakini hajapata msukosuko na vishawishi kupima uzalendo wake

  Mbowe anabusara, mvumilivu na siasa za kati kiasi. Sa nji hii inaongozwa na wendawazimu ambao kwa kutumia busara hawawezi kukuelewa.

  Kama majambazi kama Mkapa na Rowasa wanakuwa maraisi kwanini Lema aushindwe.

  Kama Slaa akisema hagombei raisi atakaetufaa ni G lema
   
 12. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #12
  Jun 6, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  CHADEMA ni chama changu lakini kwa hili nataka niwaambie kuwa Lema hajafikia standards za kuwa waziri... thinking yake iko very narrow...talk about Mnyika ,Mdee or Zitto i will understand the subject...
   
 13. kuku dume

  kuku dume JF-Expert Member

  #13
  Jun 6, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 415
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Like Lema like Martin Luther King.
   
 14. Prisoner 46664

  Prisoner 46664 JF-Expert Member

  #14
  Jun 6, 2012
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 1,955
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  Either umetumia next level ya intelligence kutuhadaa kuwa hufahamu jina lake vizuri(nakupongeza)..au kweli hulijui,which makes it look awkward sababu tayari unajua mengi aliyofanya.

  Either way,sio mbaya mkuu..Lema ni kiongozi shupavu na sote tunamkubali. Baada ya CCM kuwa chama cha upinzani hapo 2015 hakika yabidi akabidhiwe sehemu nzuri ya usimamizi kwenye serikali ya vuguvugu la mabadiliko.

  M4C..now and always.
   
 15. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #15
  Jun 6, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Naona mtoa mada hamjui mtu anayemsifia.

  CDM bwana wao wana kauli kwamba hata ukiweka jiwe litashinda! Hii kauli siipendi
   
 16. m

  muafaka Senior Member

  #16
  Jun 6, 2012
  Joined: Oct 30, 2009
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Subiri uchaguzi mbona unatupangia VIONGOZI!
   
 17. Kubwajinga

  Kubwajinga JF-Expert Member

  #17
  Jun 6, 2012
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,190
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mshumbuzi,

  Hilo lako la kumpigia mtu debe kwa kukutekenya kwa hoja moja-mbili-tatu tu hivi, na ukamsamehe hata kama kakimbia shule, ni jambo la kusikitisha sana. Ila tu naomba ukumbuke, huu ni mwaka 2012 na sio 1963
  . Telegram sio tena barua ya haraka, kuna internet 4G na zaidi. Tunahitaji mtu ambaye angalau anaweza kutafiti matatizo yetu kwenye mitandao ya ki-academia. Form 4 hayawezi hayo.

  Of note; naona jina 'lako' hulifahamu vizuri, ni Mshumbuzi na sio Mshumbusi.
   
 18. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #18
  Jun 6, 2012
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Napenzi yamekupofua huoni wala husikii kwa Lema, unamfananisha na Zitto duh! kweli kupenda upofu.
   
 19. JingalaFalsafa

  JingalaFalsafa JF-Expert Member

  #19
  Jun 6, 2012
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 759
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 45
  Pamoja mkuu:
  Embu tujiulize kidogo, kwa style hii taifa linaenda kudondokea wapi, kama sio kwenye matope mazito ya volkano!
  Upofu wa mapenzi, watanzania wanaona chui(chadem), lakini wanamfuata kumkumbatia wakijiaminisha ni kondoo, yote haya ni huku kujeruhiwa na simba (ccm) kunatuchanganya akili, wezi wengine na wajanja wengine wanatumia mateso na unyonge wetu kutokana na uozo wa ccm, kutulubuni na kututawala! Lakini ni dhambi kubwa kumuongoza kipofu shimoni kwa sababu tu ya udhaifu wake, na usitarajie huonekani, UNAONEKANA NA UTAADHIBIWA INAVYOSTAHILI. "mchunguzeni kwa makini sana anayelia sana msibani"
  Tunataka kiongozi mzalendo na mbunifu kwa nchi yake, huyu HAJAWAI KUWEPO KWENYE KITU KIITWACHO SIASA, siasa ni ya WANASIASA si VIONGOZI. Alafu chonde sana, tofautishe wanasiasa na wanaharakati, wanaojiita wanaharakati ndani ya vyama vya siasa ni sawa na wapumbavu. Kwasababu, mwanasiasa yoyote ni lazima atafungwa na kanuni na taratibu za siasa zilizopo. Lakini mwanaharakati hafungwi na chochote kile ila MANTIKI katika kupigania UTU katika kuleta usawa kwa jamii.
  MSIHARIBU MSAMIATI HUU.
  Wanasiasa wote ni vibaraka wa ukoloni mamboleo, mimi nimesema!
  Mungu wetu anaita!
   
 20. b

  big niga Member

  #20
  Jun 6, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  ....pumba zingine bwana utamlinganishaje lema na slaa wewe,lema hafai kuwa hata kiongozi wa nyumba kumi
   
Loading...