Kama sio DR. Slaa, Godbless Lema ndiye Rais 2015

ni usalendo wa hali ya juu!!!!najua tunao kina lema wengi tu espacially kipindi hiki,ila hawana pa kuoneshea uzalendo wao,nawaalika wazalendo wote tuungane tulizike hili jitu lenye meno marefu(ccm)
 
jamani wa2 wengine sijui wanawaza kwa ku2mia nn Lema awe rais wa Tz?????????????????????????? labda awe rais wa wewe na familia yako we na mkeo na watoto wako mshumbusi
 
Lema ni mpambanaji shupavu anajiamini na anajua kutetea hoja yake na mwenye ushawishi mkubwa sana,tumpe muda kama ataendelea hivyo hivyo ipo siku atafanikiwa na kufanya makubwa zaidi ya aliyo fanya na anayofanya.Unapo fikia kumpa mtu kura ya kuwa raisi inabidi kuomba na kupewa maona ya kuchagua kiongozi bora na si bora kiongozi.
 
Yaani Lema ndiye awe rais, wa kitu gani hasa? Kama ni rais wa waropokaji hapo sawa, lakini kama unaongelea kuwa Rais wa Tanzania big NO.
The unseen is illustrated by the seen.
 
jamani,tuache utani tujadili facts,Wasomi wangapi wamekuwa vituko tu,nchi hii ipo mahali pabaya kwasababu ya wasomi haohao mnaowasifu.

mimi nawakumbuka akina kikwete,profesa kapuya, Maige, ikerege,chami na wengine wengi tu wamefanya nini pamoja na elimu zao kuwa kubwa?

inakuwa sawa na Zamani watu waliamini sana kuwa watu wenye Vipara walikuwa na busara sana ikaja kuonekana baadae kwamba sivo kabisa.

Simaanishi kuwa agombee, lakini nakubali kuwa anafaa kuwa Rais iwapo tu Chama chake kitamridhia.
kuna haja gani kuwa na mtu kama Zitto mtu anayeweza kupokea rushwa akawasaliti watu wake?kisa eti ana elimu No no no!!!

Mzalendo wa kweli na jasiri sio bitozi au sura nzuri,mtu ataekuwa tayari kusikiliza shida za wananchi akajishusha na kuzitatua huyo hasa!!!wa-tz wanamtaka.
 
Pamoja mkuu:
Embu tujiulize kidogo, kwa style hii taifa linaenda kudondokea wapi, kama sio kwenye matope mazito ya volkano!
Upofu wa mapenzi, watanzania wanaona chui(chadem), lakini wanamfuata kumkumbatia wakijiaminisha ni kondoo, yote haya ni huku kujeruhiwa na simba (ccm) kunatuchanganya akili, wezi wengine na wajanja wengine wanatumia mateso na unyonge wetu kutokana na uozo wa ccm, kutulubuni na kututawala! Lakini ni dhambi kubwa kumuongoza kipofu shimoni kwa sababu tu ya udhaifu wake, na usitarajie huonekani, UNAONEKANA NA UTAADHIBIWA INAVYOSTAHILI. "mchunguzeni kwa makini sana anayelia sana msibani"
Tunataka kiongozi mzalendo na mbunifu kwa nchi yake, huyu HAJAWAI KUWEPO KWENYE KITU KIITWACHO SIASA, siasa ni ya WANASIASA si VIONGOZI. Alafu chonde sana, tofautishe wanasiasa na wanaharakati, wanaojiita wanaharakati ndani ya vyama vya siasa ni sawa na wapumbavu. Kwasababu, mwanasiasa yoyote ni lazima atafungwa na kanuni na taratibu za siasa zilizopo. Lakini mwanaharakati hafungwi na chochote kile ila MANTIKI katika kupigania UTU katika kuleta usawa kwa jamii.
MSIHARIBU MSAMIATI HUU.
Wanasiasa wote ni vibaraka wa ukoloni mamboleo, mimi nimesema!
Mungu wetu anaita!

Mkuu nimeipenda sana hoja yako!
 
Mshumbuzi,

Hilo lako la kumpigia mtu debe kwa kukutekenya kwa hoja moja-mbili-tatu tu hivi, na ukamsamehe hata kama kakimbia shule, ni jambo la kusikitisha sana. Ila tu naomba ukumbuke, huu ni mwaka 2012 na sio 1963
. Telegram sio tena barua ya haraka, kuna internet 4G na zaidi. Tunahitaji mtu ambaye angalau anaweza kutafiti matatizo yetu kwenye mitandao ya ki-academia. Form 4 hayawezi hayo.

Of note; naona jina 'lako' hulifahamu vizuri, ni Mshumbuzi na sio Mshumbusi.

Jamani sasa anasoma lakini au hamjui
 
sasa hivi hatutakiwi kuanza kuzungumza majina ya nani anafaa kuwa rais! tunatakiwa tuanze kuzungumzia matatizo ya taifa letu vipaumbele vyetu na namna ya kuyatatua! tukishayafahamu yote hayo ndio tufikirie nani anaweza kubeba jukumu hilo la utekelezaji! kukimbilia kutaja majina ndiko kulikotupatia rais ambaye alipoulizwa kwa nini taifa ni maskini bila aibu alijibu "sjiu" lakini kama tungekuwa tumeainisha matatizo na vipaumbele tukampata rais kwa misingi hiyo kwa vyovyote angejua matatizo yetu na hasa umaskini na vipaumbele vya kutatua vipoje!!
 
Nadhani na wewe unaumwa ugonjwa wa Kikwetephobia..

Mtu kama Lema upeo na ufahamu wake ni mdogo sana sio kila mtu anaweza kuwa Rais.

Angalia hata michango aliyokuwa akichangia Lema bungeni huwezi kumkuta Lema akichangia bajeti ya Wizara ya Fedha au Wizara ya Afya, yeye ni maandamano tu na kupigana.
wewe michango yako hapa JF kwani ipoje??si ni ***** tu kila siku??
 
Lema na urais wapi na wapi!
A%20S%20thumbs_down.gif
 
Hilo jina unalotumia la "kaliua urambo" ni jina mahali unapotokea ambapo ni tabora na watu wa huko kaliua mm ninawafahamu maana ni vilaza sana ndio maana kila siku wanatawaliwa na juma kapuya(gamba) yani nyie huko ni mazoba kupindikia ndio mana sishangai kuona unamponda leama maana siasa za lema kwa vilaza kama nyie ni vigumu sana kuzielewa.

nyie msio mazoba mbunge wenu nani?,au Raisi wako nani? au unadhani kura yako moja ndo itampa Lema Uraisi?,ubunge wenyewe kwa sababu watu makini walikuwa bado hawajaamka kujua upinzani unaweza kuchukua nchi 2015 hata upinzani vichwa makini vitaongezeka wabunge wenu hao wa visasi na vurugu hawatarudi,tunahitaji watu makini kama zitto,mnyika,lissu etc

 
Kweli taasisi ya u-Rais imeshuka viwango. Natambua kazi kubwa inayofanywa na CHADEMA kuleta mageuzi nchini, lakini Lema simuoni kama katulia kuweza kuwa kiongozi makini serikalini. Kupigania wanyonge, anaweza sana lakini simuoni kama mtu mwenye mpangilio na mikakati muafaka ya uongozi.
 
kwa kweli mimi na CDM, nampenda sana Lema na nilikuwa mmoja wa waliompa kura kuwa mbunge Arusha, ila kwa suala la Urais nadhani bado sana, labada kwa uwaziri.
 
Inaonyesha ni jinsi gani they are stupid.....jiwe liongoze watu, nosense...
Mkuu Remmy kauli zingine zinaonekana za kisiasa lakini inakuwa kama matusi kwa watanzania. Kwani wakisema kwamba tunaweka watu makini ambao watashinda/wanashinda kuna ubaya gani badala ya kusema ati hata ukiweka jiwe litashinda. Jiwe likishinda hivyo litawatawala wapiga kura!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom