Kama si mzee Aboud Jumbe kusingekuwapo na CCM


Mkuu, kuhusu mwalimu kufanya makosa pia, liko waazi kabisa hatayeye alikiri mara nyingi kuwa hakuwa malaika, ila nilichosema ni uibilisi ni hila za kutaka kubadilisha kabisa baadhi ya mazuri ya mwalimu aonekane siyo lolote katika nchi yetu kama ambavyo unataka watu waamini. Huko kuficha kusiwe kwa hila... kuwe na wema kabisa. Nimesoma maandishi ya watanzaia wengi tu kuhusu mwalimu, waliotutangulia umri na walifanya kazi na mwalimu kama vile Dk Salim Ahmed Salim, wewe huwaamini hao! unawaamini kina DOURADO tu!?
Na hapa umezidi kujifunua hila zako,.. Hivi Mwalimu kufanywa mwenye heri kunakuhusu nini wewe? au inatuathiri nini sisi kama taifa? hayo mambo ya imani za watu tuwaache waendelee nazo bwana. wewe ni mkatoliki? kama anatangazwa kuwa mwenye heri ni kwa wakatliki ndio maana wao ndio wanaongoza zoezil hilo, au kama wewe ni mkatoliki nenda kanisani huko katoliki kawalalamikie kuwa hafai.
Nakuomba uache tabia ya kuwaza kwa kutanguliza dini dini kwenye masuala ya taifa letu, itatuharibia bure nchi yetu nzuuri, dini zenyewe hizi tunazoziwaza kila dakika tumeletwa tu na watu weupe, tuendelee nazo kwenye nyumba za ibada tu....ndiko zinakostahili.
 
KELA72.
...mezani bado imefanywa ilalie upande mmoja....tu?, kama bilisi anavyopamba maovu yake yaoenekane mazuri na watu wasiojuwa kitu hujiramba mikono kwa utamu wake. Bado unaongeza list ya watu waliofanyiwa 'uhuni' na Mwalimu, kama SALIM, ambaye hamsahau Mwalimu kwa kufitini akakosa nafasi ya ukatubu wa UN( SOMA UNITED NATIONS AND 50 YEARS-MAYERS) hawa mabingwa wa kimataifa wa "biographies" watakupa utandu na ukoko of this good for nothing man of yours.
 

Mwalimu alifitini vipi Salimasipate ukatibu wa UN?

Mwalimu angepata faida gani kwa mtu wake kukosa nafasi hiyo?

Unajua sababu ya kweli iliyomkosesha Salim ukatibu wa UN?
 
Jumbe alikuwa awe dikteta ni habari za ndani za CIA ,hivyo aliwahiwa na mapema ,Nyerere nae ni dikteta vilevile aliwapeleka watu kuliwa na Simba kwa bango la kujemga vijiji na siasa za ujamaa kwa nguvu.

Wote hadi hawa tulio nao bado ni madikteta ingawa udikteta maana unapolazimisha matokeo ya uchaguzi kwa kutumia usalama wa taifa vifaru majeshi na kuilazimisha tume itangaze uwongo huo ni udikteta ,punda ndio walewale.
 

Naona umeamua kweli kusambaza magugu shambani! Hivi wewe kila mtu akiandika kitu unamuamini? He!, Salman Rushdie alie andika kuwa "kitabu fulani kitukufu" ni aya za kishetani unaamini alichokisema? tena yule Dk kabisa.
Salimu mwenyewe hajawi kusema kuwa alitendwa hayo, nyie mnayatoa wapi hayo??
Uzushi na mahila yenu myaache, na nimeshasikia kuwa kuna kuna kikundi kinawalipa ili mzidi kuieneza mbegu hiyo chafu kwa jamii. Ngoja nitafuatilia ntajifanya mmoja wenu ili nipate ukweli wa kuwaanika.
 

Granted kwamba Nyerere alikuwa hivyo ulivyomchora.Nina maswali machache kama ifuatavyo ili niweze kuelewa zaidi hii hoja ambayo watu wengi hapa karibuni wamekuwa wakileta:
1.Je, ikawaje hadi akateka akili na mioyo ya watu wooote waliomzunguka hadi akafaulu kuwafanya mouthpiece yake wakatangaza sifa zake yeye tu na kufunika za wengine?

2.Was he that powerful all by himself au kulikuwa na nguvu fulani iliyokuwa nyuma yake? Na kama ilikuwepo ni ipi?

Mimi nadhani Waafrika tumejikuta tukiwa na tatizo moja - kukubali kila tunachosikia bila kufanya upembuzi wake na matokeo yake tunaendeleza upotoshaji wa ukweli.We have been and we will continue to be gullible even for things that are so obviously absurd!
 
Last edited:
KELA 72
"The animal side of J.K.Nyerere" na kama utakuwa na nafasi soma maandishi ya W. E. Smith, na nyaraka (archives) za W. DOURADO. Halafu urejee katika mjadala na mtazamo huo huo uliokuwa nao kwa baba yako wa taifa.

Ndugu kwa heshima na taadhima, btw, is Wolfgang Dourado still alive? if yes yuko wapi na anafanya nini?
Samahani kwa kuingilia mjadala..( ni kupitia mijadala tunapata updates pia )
 



sielewe upeo wako upo vipi na Ulimwengu tunao ishi lakini kwa kusaidia nitakuomba nenda kasome na uangalie Video za aliyekuwa kiongozi kipenzi wa Ujarumani na karibu nchi nyingi za ulaya. ADOLF HITLAR ni vipi alitokea kuteka akili za mamilioni ya watu na kupendwa sana rikodi yake hakuna kiongozi hadi leo aliyeifika , amebaki kipenzi cha wengi ijapokuwa wanaficha hisia zao sasa unapozungumzia nyerere kuna mambo unashindwa kujikumbusha au huyajuwi kwa udani ijapokuwa wengi mnahisi hana dosari.

[ame=http://www.youtube.com/watch?v=kuxkq1zIWDY&feature=related]YouTube - HITLER speech difficult[/ame]
 
Ndugu kwa heshima na taadhima, btw, is Wolfgang Dourado still alive? if yes yuko wapi na anafanya nini?
Samahani kwa kuingilia mjadala..( ni kupitia mijadala tunapata updates pia )
DOURADO YUPO ZANZIBAR, ni Jaji mstaafu
 
"MAJIVUNO ni waziri wa nchi ya KUSADIKIKA,....alikuwa na Majivuno kweli kama jina lake na aliamini kuwa kidole chake kimoja kidogo kina akili nyingi kuliko miili na vichwa vya WASADIKIKA wote"- SHAABAN ROBERTS

LABDA MUAMBIWE KWA MIFANO: muelewe, Nyerere alikuwa kama huyu Majivuno na Watanzania kama ww na wenzako ndo wasadikika
 
suala la kuamini na kutoamini hilo ni la mtu binafsi, hivyo ndivyo waandishi wa historia wa u.n walivyoandika. Haya ya salmani usiyalete yanagusa imani za watu, na moto wake hauzimiki plz
 

Nadhani kuuliza siyo ujinga na ndiyo maana nimeuliza maswali.
Nakubali kuwa mie na watanzania wengine ndio wasadikika.Je wewe na wenzako mko upande gani na kwa kuwa huo upande mmefanya nini kutusaidia siye wasadikika nasi tuwe "upande wenu" kama unaamini huo ndio upande sahihi.

Nadhani hata wewe pia uko kwenye kusadikika maana hadi sasa hali iliyopo hata kama huitaki ndiyo hiyo ya kusadikika.
 
Mkumbushe kuwa HITLER alikuwa na watu wa propaganda kama kina JOSEF GEOBBELES, Mwalimu alikuwa zaidi ya Hitler yeye hakuhitaji watu hao kwa kuwa alishawafanya watanzania mazuzu kwa kuwawekea redio moja no television na magazeti mawili matatu ambayo anasema na kuandikwa yeye tu. sasa hebu fikiria toke unazaliwa redio yako RTD, gazeti lako uhuru na mzalendo n.k yote ya serikali, hata angejitangaza nabii mngeamini.
 
ww mimi ni KARAMA katika kusadikika.
 
Yamekuwa haya tena... Nyerere kaingia vipi ktk mjadala wa Jumbe anatakiwa kusifiwa?..
Nadhani sifa za Mwinyi Aboud Jumbe ndizo zilitakiwa zaidi ili nasi tupate kumfahamu vinginevyo!
 
Yamekuwa haya tena... Nyerere kaingia vipi ktk mjadala wa Jumbe anatakiwa kusifiwa?..
Nadhani sifa za Mwinyi Aboud Jumbe ndizo zilitakiwa zaidi ili nasi tupate kumfahamu vinginevyo!

Siyo ajabu JF!
Mnaanza kuzungumzia tembo na ukubwa wake, mnaishia kubishana kuhusu ngedere na nyani kama wanafanana na binadamu au lah!
 
junius,mkandara,

..mahakama kuu ya Zanzibar pamoja na Baraza la Wawakilishi vilianzishwa wakati wa utawala wa Alhaji Aboud Jumbe Mwinyi. kabla ya hapo mambo mengi yalikuwa yakiendeshwa kimapinduzi-pinduzi. Baraza la Mapinduzi na wajumbe wake walikuwa na nguvu za ajabu Zanzibar.

..Aboud Jumbe alikuwa Mwenyekiti wa ASP wakati chama hicho kinaungana na TANU. kwa msingi huo anastahili sifa na kuenziwa kama muasisi wa CCM akiwa Makamu Mwenyekiti mwanzilishi wa chama hicho.

..ningefurahi kama wanahistoria wangetuelimishi kuhusu kisa cha Aboud Jumbe kuondoshwa madarakani. mpaka sasa hivi hakuna mahali ambapo mkasa ule umeelezwa hatua kwa hatua, kinagaubaga.

NB:

..kuna mtu anaweza kutueleza sababu zinazomfanya Mzee Jumbe asirudi kwao Zenji, badala yake amejibanza huku Tanganyika?

..kuna mahali nimesoma kwamba Mzee Jumbe ameacha wasia kwamba mauti yakimfika hataki mazishi ya kitaifa na heshima za kijeshi. sijui kama habari zile ni za kweli au la.
 
Mkuu kumbuka hata kina jumbe walimtosa field marshal tito okero.kuna mabo mengi sana yanayouhusu hizi nchi mbili yamefichwa sio hilo la istoria ya aboud jumbe tu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…