Kama SADC Wangekuwa Sio Wanafiki Kama Ecowas, Leo Mugabe Asingekuwa Raisi

Synthesizer

Platinum Member
Feb 15, 2010
12,265
21,443
Upende usipende, lazima ukiri kwamba Ecowas ni wanaume na hawataki unafiki, tofauti sana na chombo hiki kattika eneo letu, SADC.

Siku zote nimewaona SADC kuwa ni wanafiki waliopo kwa ajili ya kutetea maslahi yao binafsi badala ya haki za wananchi katika eneo la kusini mwa Afrika.

Katika uchaguzi wa Zimbabwe mwaka 2008, Mugabe alipoona anakaribia kupoteza kiti cha Uraisi kwa MDC, kwa makusudi alizuia matokeo ya uchaguzi kuendelea kutangazwa, kwa muda wa wiki tano, wakaiba kura na baadaye kutangaza kwamba Changarai wa MDC alishinda lakini kwa idadi ya kura ambazo zingemuwezesha kuwa raisi wa Zimbabwe. Mugabe akaamuru uchaguzi urudiwe, na akijua kilichotokea akatumia nguvu za jeshi kupiga, kutisha na hata kuua wafuasi wa MDC ili kuifanya ZANU ishinde, hadi MDC wakajitoa kwenye uchaguzi!

Kila mtu alijua kilichofanyika, pamoja na SADC, na kuficha aibu SADC wakasema Mugabe aunde serikali ya kumshirikisha Changarai. Hapo ndipo wenye akili tulipokuja kuuona unafiki wa SADC.

Sasa SADC wanapaswa wajifunze kwa Ecowas kwa kile kilichotokea Gambia. Wanatia aibu.
 
Lakini ECOWAS hawajamtoa mtu ambaye alichaguliwa na wananchi. Wamemtoa aliyeshindwa akagoma kutoka madarakani.
 
Lakini ECOWAS hawajamtoa mtu ambaye alichaguliwa na wananchi. Wamemtoa aliyeshindwa akagoma kutoka madarakani.

Hujaelewa Mkuu. Katika uchaguzi ule Mugabe alishindwa, ikabidi matokeo yasimamishwe kutangazwa. Ni mbinu ambayo ilitumika pia katika uchaguzi wa Zanzibar. Ukweli ni kwamba ndicho Jecha alichofanya.
 
Back
Top Bottom