Kama ningekuwa Mgombea....

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
1,529
Ningekuwa mgombea ningehakikisha yafuatayo yanakuwa ngao yangu kwenye kampeni.

1. Kurudisha na kuimarisha Heshima na Hadhi ya Mwananchi na Taifa la Tanzania.
2. Kurudisha na kuimarisha Heshima na Hadhi ya kazi na kufanya kazi kwa Watanzania wote, vijijini na mijini.
3. Kuimarisha Ufanisi na Ustawi wa Jamii katika kupiga vita Ujinga, Umasikini, Njaa na Maradhi.
4. Kubuni mbinu za kumpunguzia mzigo mwananchi wa kawaida(haswa wenye vipato vya chini na wakulima)au kama tunavyowaita Walalahoi.
5. Kuhakikisha kuwa Sheria, Katiba na Kanuni zilizowekwa zinafuatwa ipaswavyo na vyombo vyote husika na Wananchi. Aidha kuweka maamuzi na mipango ya Serikali wazi kwa wananchi wote, kwa kuwa wao ndio waliotoa dhamana.
6. Kuwaelimisha Wananchi haki zao,wajibu wao na sehemu yao katika Taifa.
7. Kuhakikisha kuwa vita dhidi ya Rushwa, Ubadhilifu, Udini, Ukabila na kutowajibika kwa watendaji wa Serikali na tasisi zake vinaendelezwa kwa kushirikisha Wananchi.
8. Kuhakikisha kuwa njia kuu za Uchumi zinaboreshwa na kutumika kwa manufaa ya Taifa.
9. Kuhamasisha na kuhakikisha kuwa Uzalishaji mali(Kilimo, Viwanda,Uvuvi, Ufugaji, Biashara, Madini, Utalii na Maofisini) unafanyika kwa dhati, Kisayansi,kiushindani, kiuwajibikaji na kwa ubora.
10. Kuhakikisha kuwa Huduma za Msingi zinafikishwa kwa Wananchi:- Afya, Elimu, Maji safi, Barabara na Chakula
.
 
Ungekuwa unaweza ungeshayafanya.

Wachambuzi wa kwenye makochi ya kujipinda kinyume.

Maili elfu tano toka eneo la tukio, waliko hawaruhusiwi kugombea, maana hawajulikani wametokea dunia gani, ilibidi wadanganye kwamba kwao wamefukuzwa ili wapewa kipande cha uwepo na namba ya manamba.
 
hizi nazo ni kampeni nimepeni kura, mabomba yote yattoa maziwa.
 
Ungekuwa unaweza ungeshayafanya.

Wachambuzi wa kwenye makochi ya kujipinda kinyume.

Maili elfu tano toka eneo la tukio, waliko hawaruhusiwi kugombea, maana hawajulikani wametokea dunia gani, ilibidi wadanganye kwamba kwao wamefukuzwa ili wapewa kipande cha uwepo na namba ya manamba.

... afadhali yeye aliyechambua kwa usahihi na kuonyesha upeo wa hali ya juu KILIKO wewe unayebeza hayo ya REV K. Sasa wewe umewahi kuifanyia nini Tanzania kwa uwepo wako nchini ukiacha ushirika wako kwenye supu za utumbo? Au na wewe ni USEFUL IDIOT?
 
...Au na wewe ni USEFUL IDIOT?
Mimi "useful idiot" na nyinyi wenye akili msio na faida, yupi bora?

Anachambua halafu iweje, akafanye anayochambua. Achambue amekaa kwenye jamvi, anachambua karanga? Nimeifanyia nini Tanzania, naijenga Tanzania kwa zaidi ya maoni na chambuzi tu. Wanasema maoni ni kama matundu ya nyuma, kila mtu ana lake. Tenda. Unachambua uko Udachi?

Ningekuwa mgombea ningehamasisha... ningehakikisha... ningeimarisha...ninge ninge... rudi ugombee!
 
... kazi kwelikweli! ndo maana jamaa flani alikumbushia necessary na sufficient conditions katika harakati za kuleta maendeleo ZIKIWA NI PAMOJA NA WATU.
Mkuu Tindikali, mineno yako kiboko! Mitazamo yako na fikra hizi za matundu uloandika hapa yanikumbusha dizaini ya watu ambao ni kikwazo kikubwa katika harakati za maendeleo Tanzania. Ur mindset is sickening!
 
Tindikali,
Mkuu hapa unachemsha tena vibaya sana kwa sababu nakumbuka ndio ulikuwa mtazamo wa vijana wengi wa mjini kutokwenda shule kwa fikra kama hizi - Shule itanisaidia nini?. yaani walikuwa na upeo mdogo sana wa kutazama vitu kama Elimu.
Kwa mtazamo wako basi hata vitabu vya ELIMU wewe huwezi kuvisoma ukitaka kuwaona hao wasomi wenyewe wamewahi kufanya nini na sio kukaa mezani ..
 
...Kwa mtazamo wako basi hata vitabu vya ELIMU wewe huwezi kuvisoma ukitaka kuwaona hao wasomi wenyewe wamewahi kufanya nini na sio kukaa mezani ..
Hao wametoka mezani wakenda fanya tafiti, wamekusunya hela wamechapa vitabu, wamehariri. We unasema "ningekuwa mgombea ningehamasisha, ningehakikisha, ningeimarisha..." umekaa kwenye kiti cha kubinjuka nyuma unachambua na kuchakachua uchaguzi. Tena kura hupigi, uko Kyubeek na Helinski mwisho wa dunia huko jua limezamia likapotea moja kwa moja usiku mwaka mzima. Utatusaidia uongozi kweli wewe? Ningekuwa mgombea? Gombea.
 
Mimi "useful idiot" na nyinyi wenye akili msio na faida, yupi bora?

Anachambua halafu iweje, akafanye anayochambua. Achambue amekaa kwenye jamvi, anachambua karanga? Nimeifanyia nini Tanzania, naijenga Tanzania kwa zaidi ya maoni na chambuzi tu. Wanasema maoni ni kama matundu ya nyuma, kila mtu ana lake. Tenda. Unachambua uko Udachi?
Ningekuwa mgombea ningehamasisha... ningehakikisha... ningeimarisha...ninge ninge... rudi ugombee!

Yes Tindikali na kuunga mkono ktk hili
HILI UMEONGEA LA MAANA SANA,uchambuzi ulishamarizika zamana kuwa kiongozi mzuri anatakiwa kuwaje na kufanya nini.Hapa cha msingi ni vitendo tu ,
 
Rev. Kishoka
user-offline.png

Hii imekaa kisiasa zaidi sababu haya maneno tumeshayasikia sana. Je unaweza kuja na detail ya maelezo japo ya eneo moja utafanya nini na kufanya mabadiliko gani.
 
Je unaweza kuja na detail utafanya nini na kufanya mabadiliko gani.
Unamuuliza atafanya nini kwani kakwambia anagombea?

Mbona unamwekea maneno mdomoni? Katushirikisha kwenye njozi zake za uchambuzi tu. Angekuwa, angeligombea, angetaka, angekuwepo. Hayupo! Huyu ni mwandishi tu, anatuma makala kwa barua pepe hapa na pale, mchambuzi, anachakachua fikra, matendo sifuri yenye masikio. Yuko kwenye tarakilishi anasema angegombea. Kama unajua cha kufanya ukigombea, gombea!
 
Najua hagombei lakini kaamua kujiweka kwenye position ya mgombea na kutoa hints za maelezo yake. Tuko hapa kujadiliana na kukubali kukosoana kama si kurekekebishana kwa hoja

Sijamuwekea maneno mdomoni labda nirekebishe sentesi ya swali langu may be na wewe unaweza kuelewa swali langu hasa sio kwa mleta mleta mada tu wagombea wote wenye maneno haya matamu bila kuwa ufafanuzi.
Je Unaweza kuja na detail japo eneo/sekta moja ungefanya nini na kufanya mabadiliko gain?

Swali naweza kurirekebisha na jiulize wewe , mimi wale na wao

Chagua Decision making position of your choice(Uwaziri,Ukurugenzi wa shirika, ect) tueleze ungefanya nini?

Huyu ni mwandishi tu, anatuma makala kwa barua pepe hapa na pale, mchambuzi, anachakachua fikra, matendo sifuri yenye masikio. Yuko kwenye tarakilishi anasema angegombea.

Mwandishi tu? Una maana gani? Na je wewe ni nani tu .Wote wanapost na kuchangia mada hapa JF ni waandishi in one way or another . Na naaamin kila mtu kabla ya kuandika anafikria na kuchambua kile anachoadika. Lakini malengo yetu yanatofauti sijui wewe Tindikali lengo lako ni kujenga au kubomoa.

Kama unajua cha kufanya ukigombea, gombea

Sijui niseme ni jazba.
Wasafiri wote tunajua mwisho wa safari kutoka mwanza tunatakiwa kufika Dar. Lakini ni kwa usafiri gani, na ni njia gani tutapita ndo nilichokuwa nahoji. Haina maana Rev kishokakutoa mawazo yake au kuhoji kuwangu mimi naweza kuwa rubani, au dereva wa gari moshi au dereva wa FIAT. Lakini tuna idea japo kidogo ya maeneo haya ndo maana tunahoji, kutoa changamoto ya mawazo mbadala na kubadilishana mawazo
 
Unamuuliza atafanya nini kwani kakwambia anagombea?

Mbona unamwekea maneno mdomoni? Katushirikisha kwenye njozi zake za uchambuzi tu. Angekuwa, angeligombea, angetaka, angekuwepo. Hayupo! Huyu ni mwandishi tu, anatuma makala kwa barua pepe hapa na pale, mchambuzi, anachakachua fikra, matendo sifuri yenye masikio. Yuko kwenye tarakilishi anasema angegombea. Kama unajua cha kufanya ukigombea, gombea!

Umenena vema mkuu...wako wengi kweli humu....wao ndo wakubwa wa kusema, mabingwa wa kukosoa..mahiri wa kuandika...na wakali mno wakikosolewa...wengi sana..na ninawajua wengi tu...wakimaliza kubeba mabox, huku wakiwa hoi bin taaban, wanakamata computer nakuanza kuandika kila wanachoona kinafaa...ukimkosoa tu, lahaulaaa! utaona tu wakati mwingine wanakuja na vijineno vyao uchwara vya kiingereza visivyo na kichwa wala miguu, wanavicopy toka kwenye internet au kuvikariri toka kwenye movie...mara useful idiot,,,lakini wapi..hawajui what is actually happening on the ground....hayo ya Kishoka kila mwanasiasa hapa tz anayasema, tena mazuri zaidi..endeleeni na lile la dual citizenship maana kidogo ndo mnalielewa kwani lazungumzwa zaidi mlipo kuliko huku, huku ni makubwa zaidi
 
Tumegombana na wanasiasa na sasa tumeanza kulimana sisi wenyewe, JF Oyee Oyeeee!

Piga, ua, tatizo la Tanzania sio kutokujua bali ni kuonyesha kwa matendo. Maneno mazuri tumeyasikia sana lakini bado tunaendelea kuwa maskini.

Haya ya kwamba ningelikuwa, tuyaache na tuanze ya kwamba ninafanya hili na lile.
 
Rev Kishoka.

Kila Mgombea Uongozi hapa, kuanzia Diwani , Mbunge na U Rais wote wanakuja na lugha na mitizamo kama hii! Hili nimeliona kwa muda mrefu na mara nyingi na ki ukweli, kuwa mwana siasa ni kipaji maalum. Uwezo wa kutoa matamshi bila utekelezaji kila inapofika uchaguzi na matamshi hayo kukupa kuchaguliwa ...ni jambo la ajabu na kushangaza. Lakini wanarudi tena kipindi kijacho .... wanarudia vile vile ... finger crossed ... moyoni wakijiuliza ... au wameamka na kushtuka? Lakini wapi, kwa mara nyingine tena wanashinda kwa kishindo wanasonga mbele yatayari kurudi tena next time ....!

Mchungaji!

Hizo point kumi zinatekelezeka tu kama nchi zote za uhisani kwa bajeti yetu zitasitisha mchango wao kwa 100%. Hili limesha semwa sana lakini kiukweli Potentials za Watanzania ni kubwa, hazitafunguka kwa utekelezaji wa namna yeyote zaidi ya induction of massive painful _stress intentionaly or unintentionaly!!

Hata hivyo ingawa hili ni swala la majadiliano lakini ... for the sake of survival of this national ... kiukweli kabisa THAT IS WHAT IS GOING TO HAPPEN!!
 
Mfano mdogo wa detail in elimu. kama ningekuwa kwenye maamuzi.
Maeneo tofauti yana mahitaji tofauti. Wilaya ya maswa imekuwa nyuma kielimu na kushika mkia so sidhani sera ya ya sekondai kila kata inafaa kwa wilaya ya maswa na nyingine nyingi. Wilaya hizi zinatakiwa kuweka mkazo zaidi kwenye Quality na si Quantity.

Ningebadilisha mitaala kwenye Elimu hasa ya primary na sekondary .Ningewezesha shule katika wilaya kuwa na masomo optionalyao . Masomo haya yangefundishwa darasa la sita na saba Na vile vile form 3 na four. Kwa kipindi cha mwanzo kutakuwa hakuna mtihani kwa masomo haya yanayendana na mazingira
Mfano shule za wilaya zenye wafugaji wengi kungekuwa na somo la ufugaji, Wilaya zinazofana na lushoto kungekuwa na somo na matunda au mboga mboga. Wilaya kama Mafia, ukerewe labda wangekuw ana somo la uvuvi. Sehemu nyingine kungekuwa na masomo la ufugaji nyuki, upandi miti na mistu.

Masomo mengine yamsingi yatabaki kufundishwa kama kawaida.

Mabadiliko haya yatasaidia kuwawezesha wanaomaliza japo elimu ndogo ya kumudu mazingira watakayokuwa wanaishi.Hasa wale watakoshindwa kuendelea ambao tunawasahau na ni asilimia kubwa.

Kuna wakimbiji wazuri sana wilayani mbulu lakini hawapewi nafasi ya ku excel wakiwa shuleni. vipaji vyao havipwei nafasi. wanafuzi wanaingia kwenye mtihani wa practical chemistry, biology.wakati hawana maabara. Kama ningekuwa muamuzi kwenye elimu sea yangu ingekuwa Elimu inayoendana na mazingira.

Huu ni mfano wa detail niliyokuwa nategema wa ma geat thinkers wote tuje na changamoto tungefanya nini in detail katika any decision making post of your choice
 
Umenena vema mkuu...wako wengi kweli humu....wao ndo wakubwa wa kusema, mabingwa wa kukosoa..mahiri wa kuandika...na wakali mno wakikosolewa...wengi sana..na ninawajua wengi tu...wakimaliza kubeba mabox, huku wakiwa hoi bin taaban, wanakamata computer nakuanza kuandika kila wanachoona kinafaa...ukimkosoa tu, lahaulaaa! utaona tu wakati mwingine wanakuja na vijineno vyao uchwara vya kiingereza visivyo na kichwa wala miguu, wanavicopy toka kwenye internet au kuvikariri toka kwenye movie...mara useful idiot,,,lakini wapi..hawajui what is actually happening on the ground....hayo ya Kishoka kila mwanasiasa hapa tz anayasema, tena mazuri zaidi..endeleeni na lile la dual citizenship maana kidogo ndo mnalielewa kwani lazungumzwa zaidi mlipo kuliko huku, huku ni makubwa zaidi

... changanya na zako!
 
Back
Top Bottom