Norshad
JF-Expert Member
- Jun 3, 2013
- 5,216
- 12,604
Unaishi katika nyumba ya kupanga, hauishi pekeyako, wapangaji mpo wengi na baadhi yao ni mabachela..( wasela) umeoa na mkeo unampenda sana, na katika kupenda huko una wivu nao kinoma...
Kipato chako ni cha kawaida na kwa maana hiyo ni mpaka utoke ndipo rizki ipatikane, ktk eneo mnaloishi kuna tatizo sugu la Maji na yakitoka watu humaliza shughuli za utekaji maji, kufua na mambo mengine ndipo shughuli zingine ziendelee,
Sasa siku moja umeondoka mapema umeelekea kazini na ndio siku ambayo maji yanatoka na wakati unaondoka umemuacha mkeo anachota maji, (USILOLIJUA WAKATI HAUPO SASA HUKU NYUMA) wakati umeondoka na mkeo akiendelea kuchota maji pia yupo mpangaji msela mmoja anafua naye pia anachota maji
mkeo anajaza vyombo vyote mpaka ndoo ya kuogea na kisha anamuomba yule braza msela ndoo ya kuogea akaogee na jamaa anamwambia achukue hamna shida
wakati amemaliza maji yamekatika na jamaa ndio anajiandaa kusepa zake mkeo anarudisha ile ndoo lakini akiwa amesahau kutoa chupi yake ndani ya ndoo huku akiwa na khanga moja tuu anapofika ndani kwake anakumbuka kuwa amesahau chupi ndani ya ndoo ya msela na kaiweka ndani sebuleni,
Anarudi anamwambia msela nimesahau nguo yangu ya ndani katika ndoo yako jamaa anamwambia pita kachukue ndo ipo sebureni kwake na wakati huo wewe kuna kitu umesahau unarudi nyumbani unamkuta mkeo anatoka sebureni kwa jamaa ana khanga moja na chupi mkononi....
je kama ni wewe ungechukua hatua gani?