Kama ni kweli kwamba Serikali sasa imedhibitiwa na mitandao ya waharifu, Wanyonge waishije?

Criterion

JF-Expert Member
Jan 8, 2008
11,798
11,881
Nimefuatilia masuala kadhaa, yanakipeleka kuwaza mustakabari wa Wananchi wanyonge na vizazi vyao uko namna gani.

1. Kisa cha Mfanyakazi wa Wizara ya Afya aliyekamatwa na polisi kule mpwapwa akanyang'anywa fedha zake, akateswa, akatishiwa, akaandikiwa karatasi na kulazimika kuisaini bila kuisoma, na kuruhusiwa kutoka bila dhamana. Baadaye hao watesi wake wanapata taarifa za kila mahala alikopitia including TAKUKURU, akaenda ku report kwa OCD and DC, bila mafanikio.

2. Nainafuatilia kesi ya Mbowe na walinzi wake. Maelezo ya walinzi wake na mkanganyiko wa mashahidi upande wa pili.

3. Nimesoma andiko la Passport kutolewa kwa raia wengi wa kigeni kwa mazingira ya rushwa.

4. Nimefuatilia namna visecretarial centres vilivyowekwa karibu na ofisi za uhamiaji ambako waombaji huelekezwa kwenda kusaidiwa kuomba namna ambavyo vingine vinatumika kudai rushwa tena kwa nguvu la sivyo, maombi ya mwombaji yanapotumwa, yanakuwa hayana mtu wa kuyafanyia kazi.

5. Nidhamu ya kazi katika ofisi za umma kushuka, kiasi kwamba katika baadhi ya hospital za umma ukienda na mgonjwa unatakiwa wewe utafute watu wa kukusaidia kumbeba na mara nyingine, relatives wanaambiwa watafute wheel chairs, as if watu wote ni wenyeji.

6. La kuhuzunisha ni pale TAKUKURU, wanapoambiwa na Mheshimiwa Rais kuchukua hatua dhidi ya watuhumiwa kwenye report za CAG. Kwamba kazi yao ni n ini? Kama wanachukua hatua kwa amri ya rais, utaepukaje mawazo kwamba hawataweza kutetea serikali ipasavyo maana nia yao ni kutokuchukua hatua?

7. Upimaji na ramani wanakaa ofisini , kwenda kupima viwanja hadi wallipwe na mpimiwaji wakati wanalipwa mshahara kwa kazi hizo? Wanashindwa nini kupima maeneo kwa mjibu wa mipango mji lili watu wanapotaka kujenga wakabidhiwe maeneo hayo kwa gharama zinazoeleweka?

8. Maamuzi ya viongozi kutokujali matatizo ya wtu wanyonge na yanayolenga kujihami na kulinda mafisadi.

Sasa katika mazingira kama haya na mengine mengi ambayo sijayaandika, Mwanachi mnyonge aishi namna gani? Haki yake anaipata wapi? Nani atamtetea katika mfumo fisadi unaotamalaki? Polisi, ni kama mnavyosikia. PCCB kama mnavyoona. Kila mahala!. Sasa Huyu mtu bila shaka ni Yatima ama mtoto wa kambo. Ili aendelee kuishi, afanye nini? Tupeane maarifa jamani.
 
Back
Top Bottom