Kama ni kweli hili la DIT, basi watanzania wa kudunduliza wasahau elimu ya juu

kandawe

JF-Expert Member
Jun 24, 2013
1,137
810
Wanabodi, ni jioni hii nimepitia maeneo ya DIT kumwona mtoto wa rafiki yangu asomaye chuoni hapo akiwa mwaka wa kwanza. Mimemkuta kajiinamia kama anaongea peke yake.

Nilivyomuuliza kulikoni kanijibu nina hati hati ya kurudia mwaka. Nikamuuliza umefeli? Akasema hapana,nmechelewa kumalizia ada ya chuo.

Nikamuuliza,umechelewa au hujalipa? Akaniambia hivi...wakati najoin mwaka jana,nililipa nusu kama ilivyokawaida ya wanachuo tunaokosa mikopo na nusu iliyobaki nmelipa juzi lakini wahasibu wamegoma kupokea bank slip kuwa hadi niende kwa registrar, nmeenda kwa registrar kasema hawezi tena kuruhusu isipokuwa nirudie mwaka! Nikabaki nashangaa.

Hivi mtu amelipa tayari pesa iko ndani ya akaunti ya chuo,anaambiwa arudie mwaka kisa kachelewa kulipa kwa wiki mbili!!! Sio kuwa mwaka umeisha na wala si kama ni wakati wa mitihani kazuiwa hadi alipe bali kachelewa kulipa na sio kwamba hajalipa!

Sasa binafsi nmebaki nimeduwaa, hivi watanzania kwa pesa yetu ya kudunduliza mzazi kajichanga, kanyimwa mkopo amejibana akakamilisha bado tena mtoto anapata frustrations za kurudishwa aanze tena upya!!??

Nimejiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu! Hii ni kumkomoa au kumsaidia? Hii itakuwa ndo kumsaidia mtoto wa mtanzania apate elimu ya juu au wanaotakiwa wasome ni wale watakaopata mikopo na watoto wa matajiri tu?

Kabisa nimekosa majibu na nimeishia kumshauri akamuone mkuu wa chuo labda hajaelewa kilichosemwa maana itakuwa hatari.
 
Naonahili suala lina watu wao... usiwapalie mkaa wenzio wakati wewe huoti moto. mambo ya chuo..ni ya chuo, xo better go to administation that is the right place to speak out ur complaints. Pobably aliyekupatia information kajiegeshea yeye
 
Tupaaze sauti zetu kupinga uhuni wa aina hii.
Kanuni za ulipaji ada hazielekezi kupigisha mactime mwanafunzi akichelewa kulipa tuition fees.
Taratibu zilizopo ni pamoja na kuzuiwa kufanya mitihani au kuzuiliwa matokeo.
 
Prof. Christian Wambura Nyahumwa ndio mkuu wa taaluma chuoni DIT. Inasemekana anakaribia kustaafu, hivyo zinatafutwa hela ya kustaafia kwa kila njia. Wanyonge tutafute pa kwenda maana haieleweki tunasaidikaje. Hapo ni Mpaka Mhe. Rais mwenyewe aseme neno au atoe maelekezo, vinginevyo mzazi na mwanafunzi wataumia.
 
Wanabodi, ni jioni hii nimepitia maeneo ya DIT kumwona mtoto wa rafiki yangu asomaye chuoni hapo akiwa mwaka wa kwanza. Mimemkuta kajiinamia kama anaongea peke yake.

Nilivyomuuliza kulikoni kanijibu nina hati hati ya kurudia mwaka. Nikamuuliza umefeli? Akasema hapana,nmechelewa kumalizia ada ya chuo.

Nikamuuliza,umechelewa au hujalipa? Akaniambia hivi...wakati najoin mwaka jana,nililipa nusu kama ilivyokawaida ya wanachuo tunaokosa mikopo na nusu iliyobaki nmelipa juzi lakini wahasibu wamegoma kupokea bank slip kuwa hadi niende kwa registrar, nmeenda kwa registrar kasema hawezi tena kuruhusu isipokuwa nirudie mwaka! Nikabaki nashangaa.

Hivi mtu amelipa tayari pesa iko ndani ya akaunti ya chuo,anaambiwa arudie mwaka kisa kachelewa kulipa kwa wiki mbili!!! Sio kuwa mwaka umeisha na wala si kama ni wakati wa mitihani kazuiwa hadi alipe bali kachelewa kulipa na sio kwamba hajalipa!

Sasa binafsi nmebaki nimeduwaa, hivi watanzania kwa pesa yetu ya kudunduliza mzazi kajichanga, kanyimwa mkopo amejibana akakamilisha bado tena mtoto anapata frustrations za kurudishwa aanze tena upya!!??

Nimejiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu! Hii ni kumkomoa au kumsaidia? Hii itakuwa ndo kumsaidia mtoto wa mtanzania apate elimu ya juu au wanaotakiwa wasome ni wale watakaopata mikopo na watoto wa matajiri tu?

Kabisa nimekosa majibu na nimeishia kumshauri akamuone mkuu wa chuo labda hajaelewa kilichosemwa maana itakuwa hatari.
Registration was over since last Saturday
 
Haya semeni sasa!
Usajili umeisha ndugu na tangazo lilitolewa mapema sana piga hesabu chuo kilifunguliwa tarehe 20/03/2017 walitoa wiki mbili za registration na registration ilifanyika had wikiendi yaan jmos na jpili kama ni tatizo la kifedha angetoa taarifa mapema
 
Back
Top Bottom