Kama ni Kweli Hili la Chuo cha DIT, Basi Watanzania wasahau Elimu ya Juu.

Mwamba1961

JF-Expert Member
Dec 10, 2016
624
408
Nimepitia maeneo ya DIT kumwona mtoto wa rafiki yangu asomaye chuoni hapo akiwa mwaka wa kwanza. Mimemkuta kajiinamia kama anaongea peke yake.

Nilivyomuuliza kulikoni kanijibu nina hati hati ya kurudia mwaka. Nikamuuliza umefeli? Akasema hapana,nmechelewa kumalizia ada ya chuo.

Nikamuuliza,umechelewa au hujalipa? Akaniambia hivi...wakati najoin mwaka jana,nililipa nusu kama ilivyokawaida ya wanachuo tunaokosa mikopo na nusu iliyobaki nmelipa juzi lakini wahasibu wamegoma kupokea bank slip kuwa hadi niende kwa registrar, nmeenda kwa registrar kasema hawezi tena kuruhusu isipokuwa nirudie mwaka! Nikabaki nashangaa.

Hivi mtu amelipa tayari pesa iko ndani ya akaunti ya chuo,anaambiwa arudie mwaka kisa kachelewa kulipa kwa wiki mbili!!! Sio kuwa mwaka umeisha na wala si kama ni wakati wa mitihani kazuiwa hadi alipe bali kachelewa kulipa na sio kwamba hajalipa!

Sasa binafsi nmebaki nimeduwaa, hivi watanzania kwa pesa yetu ya kudunduliza mzazi kajichanga, kanyimwa mkopo amejibana akakamilisha bado tena mtoto anapata frustrations za kurudishwa aanze tena upya!!??

Nimejiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu! Hii ni kumkomoa au kumsaidia? Hii itakuwa ndo kumsaidia mtoto wa mtanzania apate elimu ya juu au wanaotakiwa wasome ni wale watakaopata mikopo na watoto wa matajiri tu?

Kabisa nimekosa majibu na nimeishia kumshauri akamuone mkuu wa chuo labda hajaelewa kilichosemwa maana itakuwa hatari.
 
Yaani badala wewe kumsaidia kwa kwenda kuonana na Registrar na kupata taarifa kamili unakimbilia kuja kulalamika hapa JF!!! Hivi watz nani katuloga?? Yaani udaku udaku tu... sasa umemsaidia nini mtoto wa rafiki yako?? Halafu unaonekana ni mzee kwelikweli tangu 1961?? Huna cha kusaidia??
 
umemchana mkuu
 
Huyo dogo niende nae mimi kwa registrar, tena naanza nae kwa dean of faculty, nikitoka hapo kama itashindakana, kwa principal, sijui ikishindikana kwa bodi ya wakurugenzi, acheni mchezo kabisa.
 
Pole kwa huyo mwanafunzi.
Mimi mwenyewe lilinikuta mwaka 2011 MUCCOBS/MOCU. Nilirudia mwaka kwa kushindwa kulipa ada kwa wakati.
Nasikitika kujua kuwa bado lipo nilidhan labda vyuo vilishafanya mabadiliko.
Naona Ruaha wanalipa faini kwa kuchelewa kulipa ada. Bora hii kuliko kulazimishwa kurudia mwaka.
 
Yaani badala wewe kumsaidia kwa kwenda kuonana na Registrar na kupata taarifa kamili unakimbilia kuja kulalamika hapa JF!!! Hivi watz nani katuloga?? Yaani udaku udaku tu... sasa umemsaidia nini mtoto wa rafiki yako?? Halafu unaonekana ni mzee kwelikweli tangu 1961?? Huna cha kusaidia??

Tulishalimaliza ila leonimeliweka ila watu wengine wajue matatizo tunayoyapata / yanayoyapata wana chuo ..

Mwamba1961 ni jina tu, mimi ni kijana
 
Vyuoni kama kuna mtu anatakiwa kuwa na busara basi ni REGISTRAR tena awe na busara kuliko hata DEAN maana wanafunzi yanawakumba mengi sana

Umenikumbusha,, Vyuo vingi REGISTRAR ni watata saaaana...
 
Yaani badala wewe kumsaidia kwa kwenda kuonana na Registrar na kupata taarifa kamili unakimbilia kuja kulalamika hapa JF!!! Hivi watz nani katuloga?? Yaani udaku udaku tu... sasa umemsaidia nini mtoto wa rafiki yako?? Halafu unaonekana ni mzee kwelikweli tangu 1961?? Huna cha kusaidia??
Itakuwa mtoto wake sio wa rafiki yake.
 
Msaada jamani hivi inawezekana kutoka chuo cha private kuhamia cha serikali na mchakato ukoje kama inawezekana?
 
Inawezekana kabisa, nimewahi kuhama kutoka Mwenge university nikaenda udom na nimemaliza chuo bila shida.
 
Back
Top Bottom