Kama ni kweli basi System ndo Tatizo

Hapo ndipo uliposhindwa na Kinana. Unapigana vita na Kinana binafsi badala ya kupigana na adui yako wa ukweli ambae si mwengine bali ni Mtanzania anaekunyima kura miaka yote. Fikiri.

Wakati wewe unapigana vita vya kusadikika na Kinana na CCM, Kinana yupo huko kwa wapiga kura anawakinaisha waipe kura CCM.

Kila unavyowaambia Watanzania CCM ni mbaya, Kinana ni mbaya, Watanzania hao hao wao wanakuona wewe ni fataani.

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?

Hajjat kweli kinana ni ryt person at a ryt time kwa ccm daaah yaaan sasa hivi jamaa wanaikatikia ngoma wamesahau mpaka ukawa duuh msonjo ni "mafioso" hatari
 
Naamini wewe kuna kitu unacho cha pekee umereta uchambuzi ambao ni kinga ya ccm na ninawashauri wenye nafasi zao ndani ya ccm wasome huu uzi na usitoke humu mapema kwa faida yao,kiukweli na nawashauri wazunguke mjini na vijijini wapate maoni,huyu jamaa anasifa lkn tanzania ya sasa sio aina ya rais wanaemtaka na pia watu hawamjui kabisa,pia wasje wakajidanganya kufananisha namna mkapa alivyoingia madarakani na hali ya sisa za sasa,kama ni system ndo imempendekeza wajipange vizuri viginevyo watatumia nguvu nyingi kumpeleka ikulu au hata kushindwa kabisa pili ccm watapoteza viti vingi vya wabunge kama hawatampitisha rais ambaye anaweza kuwaombea kura wabunge kitu mbacho bado itakuwa ni changamoto sn kwa ccm,kama mleta uzi kama anavyosema nenda kote ndani ya ccm ua ndani ya majimbo ya upinzani wanakwambia mtu pekee ambaye wanamkubali ni magufuli au kidogo muhongo lkn wengine wote wenye cv nzuri za elimu na utumushi lkn wapole hawakubaliki, angalizo watu wanamtaka mtu ambaye ni mkali wa kupambana na mfumo ulioshindikana na wakimkosa ndani ya ccm watamtafuta kwingine.kikwete na wale wenye nafasi lione hili mapema kabla hamjakosa usingizi maana mkapa alifanikisha mwk 1995 lkn siasa za wakati huo sio sawa na za sasa hiyo system mguvu ya umma itawashinda dunia imabadirika sana
Mkuu nimepitia mabandiko yooote hapa kuanzia juu hadi hili la kwako. Nimeona watu wanatoa analysis nzuri na zenye mashiko. Nimependa kuanzia Lord denning (Alfred Thompson Denning, Judge wa zamani wa Uingreza huyu aliyeheshimika sana) na wengine. Lakini nimependa zaidi zaid hii conclusion yako kwamba siasa za wakati huo siyo siasa za sasa hiyo system nguvu ya umma itawashinda. Hili ni jambo muhimu sana. Kama sysytem hai kuscan environment vizuri inaweza kuja kushangazwa na nguvu ya umma. Kuna sehemu mbalimbali tumeshuhudia system ikitaka kuweka mtu wao kwenye utawala lakini ikashindwa kwa sababu watu wamechoka, hawana tena utii kwa mamlaka hivyo wanaamua kufanya popular uprising matokeo yake system inajipoteza na kukubali kwamba yenyewe ni AGIP (Any Government In Power)!

System haiwezi kuibuka tu na mtu na ku uweka katika enzi hizi bila kwanza ku mgroom na kumpa uwanja wa kujulikana kwa watu ili iwe rahisi kwao kumpitisha na kushirikiana na nguv

Urusi na China ni tofauti kwa kuwa wao wanamtengeneza mtu ndani ya Chama (hizi nchi ni za chama kimoja japo urusi ina tuvyama) na hakuna jinsi mtu akishapitishwa na Chama lakini hapa kwetu ukimtengeneza wa CCM wananchi wanaweza kumkataa akaingia wa UKAWA ambaye hukumtengeneza bali ametengenezwa na nguvu ya umma.

umuhimu wa nguvu ya umma usibezwe hata kidogo.
 
umejenga hoja vizuri lakini umerudia makosa kama yale yanayofanywa na system, ya kudhani kwamba lazima raisi atoke CCM, hayo ni mapungufu makubwa ya sysytem. Tz in watu takribani 50mill CCm ina wanachama 5mill nje ya mfumo wa kiccm kuna watu wengi sana wenye uelewa uwezo na elimu nzuri hutaki unaacha, je hao system haiwahitaji?? pia twende mbele zaidi ya hapo system inatakiwa kuwafanyia vetting watendaji wote wa ngazi za kiserikali hata utoaji wa ajira umulikwe na system naomba kuwasilisha

Ukiwa ni mfuatiliaji wa siasa za dunia utagundua kitu kimoja kuwa kwenye nchi nyingi sana duniani kama sio zote systems zina mchango mkubwa sana kwenye kupatikana viongozi wanaoziongoza nchi izo. Hii ni kuanzia Nchi tajiri hadi Nchi masikini. Nitatoa maelezo vizuri kidogo ili niweze kueleweka vizuri.

Kwenye nchi zote duniani kuna vitengo vyao vya intellejensia ambavyo kazi kubwa ni kusoma siasa na hali za uchumi za nchi husika na za nchi za dunia na hivo vitengo kazi yake kubwa ni kubashiri au hata kupanga kuwa kwa hali ilivo nchini na kwa hali ilivo duniani ni vizuri tukapata kiongozi au tukawa na kiongozi wa aina fulani ili kwanza nchi iweze kutulia na pili nchi iweze kusonga mbele. Hivi vitengo huwa vinastudy hadi sera za nchi fulani na kutoa ushauri kwenye nchi zao kuwa kutokana na nchi fulani kuchukua sera fulani basi nasi tuchukue njia fulani ili tu uchumi wa nchi na hali ya nchi iwe salama.

Ndo mana kama urusi unaona system inambakisha putin ili aweze kutengeneza watu wengi wa aina yake kwa ajili ya kuweza kupambana na hila za marekani kwa mustakabali wa nchi ya urusi, ndo mana hata china system saivi inatengeneza viongozi wenye kaliba ya unyenyekevu na upole kwa sababu china saivi inajijenga kimataifa ili kuwa nchi yenye ushawishi kibiashara duniani mfano waangalie raisi wa china aliyepita na huyu wa sasa xi jiping.

Ndo mana mnaona Iran inabadilisha viongozi kutoka mwenye msimamo mkali aliyeijenga irani kijeshi Mahmoud Ahmadinejad na huyu wa sasa mwenye hulka ya upole Hassan Rouhan kwa sababu tu wameona watulize mgogoro wao na marekani ili waweze kujijenga kiuchumi. Ndo mana kuna hata watu wanasema kuwa J.F Kennedy aliuawa na system yenyewe ya marekani baada ya kuona kuwa kuna mambo alikuwa akienda against nayo kwa mujibu wa mipango yao.

Nimesema haya kutokana na jambo lililo midomoni mwa watanzania wengi kuanzia siku ya jana hadi leo hii nalo ni kutangaza nia na kuchukua fomu kwa nguli wa sheria duniani Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani. Kuna watu wanasema kuwa huyu ni chaguo la system na wengine wanasema huyu ni chaguo na Kikwete.

Kuna kitu nimekiwaza sana na sidhani kama kweli ni system ndo imeshauri ivo ilikuwa makini kwa kuelewa tatizo letu Tanzania ni nini na tufanyeje ili kutoka hapa na ndo mana nimeamua kuandika hii thread. Kama tuna system makini lazima itajua kwa sasa Tanzania tunaitaji kiongozi wa namna gani. Na kama huyu ni chaguo la mkuu basi mkuu inabidi atafakari sana na washauri wake kama wana mapenzi mazuri na vizazi vyao huko mbeleni.

Hata kama umeshuka leo kutoka nchi jirani ukizunguka mikoa 5 tu na kuwauliza watu 20 kwenye kila mkoa watakwambia tatizo kubwa la Tanzania nchi haiendi, watu wanachukuliana poa, hamna userious kwenyew kazi na kuwahudumia wananchi,watakwambia kuna tatizo la rushwa na upigaji yani kila mtu ni mwizi na anataka apate nafasi aibe, watakwambia kuna matatizo ya afya,elimu,maji, miradi kutokamilika kwa wakati na watu kula fedha za miradi na watakwambia pia kun a utekelezaji wa miradi chini ya kiwango.

Ukitoka hapo ukifanya study ya jamii ya watanzania hata kwa miezi miwili tu, kwa kuanzia kwenye maofisi,kwenye television na mijadala inayofanyikaga kwenye television na hata kwenye vijiwe utagundua kitu kimoja kuwa watanzania ni watu wa porojo na siasa sana. Ni watu wa maneno mengi na kulalamika si maofisini,si vijiweni, si kwenye mitaa na vijiwe na si kwenye kwenye kumbi za starehe.

Utagundua kuwa kuna opportunities nyingi sana Tanzania ila wazawa hawazitumii na wageni kutoka kenya,south africa na zimbabwe wanakuja wanazitumia na kutengeneza mamilioni ya fedha kila siku. Utagundua kuna tatizo kubwa sana kwenye mifumo ya uli[paji kodi na wananchi wengi sana hawalipi kodi, utagundua kuna ukwepaji mkubwa sana wa kodi unaoikosesha serikali mapato mengi sana.

Sasa kama tungekuwa na system makini iyo system ingeweza kuyaona haya yote na siku ya mwisho ndo ingeshauri nani wa kumpa hii dola ili arekebishe haya yote. Sishani kwa system makini ingependekeza mtu mpole, mkimya na asiyeweza kukemea kama Jaji Agustino Ramadhani.

Sina mashaka na weredi,uadilifu na hekima za Jaji Ramadhani ila kama kweli yeye ndo chaguo la watu fulani kama wanavojulikana "The System" basi watakuwa wamekosea sana kwa sababu Tanzania kwa ilipofika hapa na dunia inavokimbia bila shaka tunaitaji watu aina ya Prof Muhongo au John Pombe Magufuli. Tutadanganyana sana ila siku ya mwisho huu ndo ukweli na utabaki kuwa ukweli.

Kama nilivoandika kwenye post inayomuhusu Jaji Ramadhani napenda nirudie tena hapa na someni tena ndugu zanguni

  • TANZANIA INAITAJI MTU SERIOUS, MTU MKALI NA MFUATILIAJI WA MAMBO, MTU ASIYE MPOLE NA ANAYEJUA TATIZO KUU LA WATANZANIA NI UVIVU, KUPENDA POROJO, KUENDEKEZA SIASA KILA MAHALI NA KUTOJITUMA. TATIZO LA TANZANIA NI KUKOSA MTU THABITI MWENYE MAONO FULANI JUU YA UCHUMI WA NCHI NA UCHUMI WA DUNIA AMBAPO HAPA SIDHANI KAMA ATAFIT VIZURI. SIDHANI KAMA ATAWEZA KUPAMBANA NA FITNA ZA KINA MEDIA TYCOON AMBAO WAKIKOSA VITU WANAVYOVITAKA WANAANZA KUIYUMBISHA SERIKALI NA WATENDAJI WAKE KAMA WAPENDAVYO.SIDHANI KAMA ATAWEZA KULISIMAMIA BARAZA LAKE LA MAWAZIRI LIWEZE KUDERIVER KWENYE STANDARDS ZA JUU KABISA INAVOTAKIWA.

Asubuhi njema ndugu zanguni
 
wasiraisishe hivyo kama system inashidwa kufanya analysis ya aina gani ya mtu watu wanaemtaka iko shida na wanaidanganya ccm,oke! Urais wanaweza kumfanya ashinde lkn,je wabunge wao atawaombea kura na je watu watajiuriza amewajuaje maana hakuwai kufanya nao kazi,naiona ccm ikipata anguka la nguvu ndani ya bunge kiasi cha kuwatisha,maana watu watamuona ni mpole hivyo watachangua wabunge wa upinzani wengi ili kubana serikali,
je watafanya kazi ?
Je watakuwa wameisaidia ccm?
Je je wanajua watu wanamtaka rais wa aina gani?
Kazi kwao wajipime

Ndugu haizungumziwi ccm hapa, inazungumziwa system ya nchi.
System haipaswi kufanya kazi kuinusuru ccm bali maslahi mapana ya nchi.

Je, nchi inahitaji nini kwa sasa na baadae? Sio wabunge mangapi wa ccm!

Hauangaliwi umaarufu wa mtu BINAFSI hapa.
 
Wanao faa kuja kurekebisha hii system ni Jaji Augustino , Le Professor Mhongo na Mahiga , hao wengine ni chanzo au wanechafuka kwa kutumiwa kuharibu hii system hivyo watakosa kauli dhabiti ya kuirekebisha au kukemea mapungufu ya watendendaji rejea kauli ya J.K original ........ Ukimuangalia mtu usoni tu wajua Huyu anapinga rushwa
 
hv kweli ww umefikiria hiki ulichokiandika kabla ya kupost hapa ukaona kinaendana na hoja
Either umejaribu hata kidogo kupitia kile ambacho wenzio wamechangia toka mwanzo wa hii thread na ukaona ni sawa kuongea haya ulioyapost???
 
Ukawa pekee ndiyo yenye uwezo

Lord umetoa mawazo yako na ninayaheshimu, lakini nadhani inatupasa twende mbele zaidi ya hapo, hebu kwa maoni yako jaribu kupendekeza ni nani basi kati ya hawa walioonyesha nia ya kuutaka urais kutoka chama tawala au upinzani na hata kama kuna ambao hawajajitangaza anafaa kuwa rais wa nchi hii ya wadanganyika?
 
hv kweli ww umefikiria hiki ulichokiandika kabla ya kupost hapa ukaona kinaendana na hoja
Either umejaribu hata kidogo kupitia kile ambacho wenzio wamechangia toka mwanzo wa hii thread na ukaona ni sawa kuongea haya ulioyapost???
Vipi? kwani mkuki umeingia moyoni?
maana hapa kinacho ongelewa. Ni jinsi system ilivyo poromoka au kuharibika ktk kutupatia kiongozi bora , na pili ni jinsi gani tunaweza kurekebisha hali hii, ambayo itawezekana kwa kumpata Mtu au Watu wanaoweza rekebisha hali hii, Ndio Maana watia nia wote au wengi wa ccm wameongea ni jinsi gani wata rekebisha hali hii . Sasa cha kukuuliza ukimuangalia x je anaweza ??? Sasa Mimi kwa maono yangu Ndio hao niliwataja
 
Asante mkuu wa mchango wako murua. Ila kuwa na structures za kijamaa sio tatizo kubwa sana, mbona nchi kama China pamoja na kubadirika kutoka uchumi wa kikomunist hadi wa kibepari ila system yao inaonekana kuimarika zaidi na kufanya vizuri zaidi hadi China inazidi kupaa kiuchumi kila siku na kule China still kuna one party system?
Ninachokiona Tanzania ni kuwa ni kama kuna sehemu Sytem yetu imelala kama sio kufa na hiyo sehemu ni kwenye huo upande wa kupanga mipango na mikakati madhubuti kuhusu siasa na uchumi na ndo mana nchi yetu imekuwa inayumba sana hasa kwenye kupata viongozi bora wenye maono katika kuifanya nchi iweze kucompete vizuri kwenye dunia hii ya ushindani. Nakubaliana na wewe pia kuwa inawezekana kuna baadhi ya watu wanaififisha kwa maslahi yao binafsi na ninavoona kwa maslahi mapana ya nchi lazima system iamue kujiweka sawa kwa kuwaondoa na kufanya kazi zake vizuri ili iweze kutimiza majukumu yake vizuri.

Tatizo letu ni uwezo wa mtu mmoja mmoja. Inaelekea wachina wako more qualified than we are - wao hata mashirika yao ya umma bado yapo na ndo yanaendesha economy kwa kiwango kikubwa pamoja na kuwepo mashirika binafsi. Uchambuzi wa kina juu ya ni kwa nini mfumo wa kichina umefanikiwa na mfumo wa Kitanzania umeshindwa utaishia kwenye uwezo wa mtu mmoja mmoja. Tukubali kuwa wengi wa viongozi wetu (ambao ni sehemu yetu) hawajaonesha uwezo wa kizalendo wa kutosha kuzisimamia nafasi walizokabidhiwa. Hatuna uzalendo, tuna low IQ, low EQ, tamaa, njaa, kutojali, kujipenda wenyewe kuliko kupenda vya pamoja au vyote kwa pamoja. Tutazungumziaje kushindwa kusimamia sheria nyingi pamoja na milolongo ya vyombo kama - polisi, takukuru, CAG, tume za maadili ya viongozi, na lundo la sheria kibao, n.k. Maelezo magumu na ya ukweli ni kuwa we are inept. Hatuwezi.
 
Hii ni "thread" nzuri sana, iliyokaza manyiki yenye mshiko thabiti. Ni ukweli usio pingika system ya Baba wa taifa iliweza angalia yote. Maslahi ya chama na nchi. Kinachoshanghaza, CC! ya sas, sujui kwa nini haiigi wajamaa wengine Kama China, Urusi nk. Wamebadilika, "system" zao za maslahi ya nchi zao kwanza, hata kama Western watasema nini Na kwa ndani hawalindani, ukileta za kuleta n akujeorpodize maslahi ya nchi umeenda tend kwa kusaulika, bila kujali ulikuwa nani, kisiasa na hata kigedha.
 
Mkuu nimepitia mabandiko yooote hapa kuanzia juu hadi hili la kwako. Nimeona watu wanatoa analysis nzuri na zenye mashiko. Nimependa kuanzia Lord denning (Alfred Thompson Denning, Judge wa zamani wa Uingreza huyu aliyeheshimika sana) na wengine. Lakini nimependa zaidi zaid hii conclusion yako kwamba siasa za wakati huo siyo siasa za sasa hiyo system nguvu ya umma itawashinda. Hili ni jambo muhimu sana. Kama sysytem hai kuscan environment vizuri inaweza kuja kushangazwa na nguvu ya umma. Kuna sehemu mbalimbali tumeshuhudia system ikitaka kuweka mtu wao kwenye utawala lakini ikashindwa kwa sababu watu wamechoka, hawana tena utii kwa mamlaka hivyo wanaamua kufanya popular uprising matokeo yake system inajipoteza na kukubali kwamba yenyewe ni AGIP (Any Government In Power)!

System haiwezi kuibuka tu na mtu na ku uweka katika enzi hizi bila kwanza ku mgroom na kumpa uwanja wa kujulikana kwa watu ili iwe rahisi kwao kumpitisha na kushirikiana na nguv

Urusi na China ni tofauti kwa kuwa wao wanamtengeneza mtu ndani ya Chama (hizi nchi ni za chama kimoja japo urusi ina tuvyama) na hakuna jinsi mtu akishapitishwa na Chama lakini hapa kwetu ukimtengeneza wa CCM wananchi wanaweza kumkataa akaingia wa UKAWA ambaye hukumtengeneza bali ametengenezwa na nguvu ya umma.

umuhimu wa nguvu ya umma usibezwe hata kidogo.
Asante sana mkuu. Tuzidi kujumuika humu pamoja ili tuweze kuiweka nchi yetu sawa mkuu.
Umeongelea kuhusu nguvu ya system na nguvu ya umma, kusema kweli hapo zamani kuna kamsemo kalikuwa kanasema the army cant defeat people, ila kwa scenario za hivi karibuni huko misri(kuondolewa kwa Morsi na kuingizwa kwa fatal al sisi kutokana na influence ya system ya misri wakishirikiana na america) na thailand(kuondolewa kwa familia ya kina shinawatra iliyokuwa inaungwa mkono na watu wengi ila inapingwa na system) kumeanza kubadiri nadharia hii. Nitakuelezea hapa unielewe vizuri. Kwa misri popular uprising iliweza kumuondoa Hosni Mubarak aliyekuwa mshirika mkubwa wa marekani, hapo system ilishindwa kuzuia ila bahati mbaya sana aliyechukua nafasi yake alikuwa mohamed morsi na kutokana na system kujua kuwa yule alikuwa threat kwa future interest ya nchi yao ndo ikaonyesha nguvu yake kwa kumpiga fitna kutumia iyoiyo popular uprising na kurudisha tena utawala wa mwanajeshi(angalia kama kuna tofauti yeyote kati ya Hosni Mubarak na Fatal Al sisi alafu uniambie) sasa hiyo ndo nguvu ya system ninayoisema hapa. Ukienda Thailand kule kun a familia ya kina shinawatra ambayo ina nguvu kubwa ya kifedha na ushawishi kwa wananchi ila system imeweza kuwaondoa wote kwenye utawala wa iyo nchi pamoja na nguvu yao ya ushawishi kwa umma. Hii ni kwa sababu system ilishaona kuwa wale watu ni threat kubwa kwa future interest ya nchi yao.
Mfano mwingine ni kuwa imeonekana na kudhihirika kuwa system inapocollapse kwenye nchi basi iyo nchi inafeli na kushindwa kujiendesha na mfano wa nchi ambazo system ilicollapse kutokana na popular uprising na hadi leo hizo nchi zimeshindwa kusimama ni Libya, Yemen na hata Tunisia kwa mbali. Pia ndugu yangu kumbuka hata Bahrain popular uprising pia ilifeli kutokana na infuence ya system.
 
Lord umetoa mawazo yako na ninayaheshimu, lakini nadhani inatupasa twende mbele zaidi ya hapo, hebu kwa maoni yako jaribu kupendekeza ni nani basi kati ya hawa walioonyesha nia ya kuutaka urais kutoka chama tawala au upinzani na hata kama kuna ambao hawajajitangaza anafaa kuwa rais wa nchi hii ya wadanganyika?
Asante Mkuu, nimeshasema kwenye main thread kama umeisoma vizuri mkuu. Nimeelezea kila kitu na kubainisha challenges zetu ni zipi na tunataka watu wa aina gani ili kuweza kuzimaliza na nimesema ni watu aina ya Prof Muhongo au John Pombe Magufuli, kwa kuongeza mwingine namuona pia Tundu Antipass na Mwigulu kwa mbali anaingia kwenye kundi hili. Ila kwangu mimi binafsi ninamuona anaefaa zaidi kuanzia upinzani na chama tawala kwa hali ya sasa ni Prof Sospeter Muhongo.
 
umejenga hoja vizuri lakini umerudia makosa kama yale yanayofanywa na system, ya kudhani kwamba lazima raisi atoke CCM, hayo ni mapungufu makubwa ya sysytem. Tz in watu takribani 50mill CCm ina wanachama 5mill nje ya mfumo wa kiccm kuna watu wengi sana wenye uelewa uwezo na elimu nzuri hutaki unaacha, je hao system haiwahitaji?? pia twende mbele zaidi ya hapo system inatakiwa kuwafanyia vetting watendaji wote wa ngazi za kiserikali hata utoaji wa ajira umulikwe na system naomba kuwasilisha
Ndugu sijasema lazima watoke ccm. Nisome vizuri utanielewa Mkuu.
 
Kuna anayeuliza kwa nini chama kushika hatamu imefail Tanzania na kufanikiwa China. Tofauti kubwa ni jinsi ambavyo power iko distributed kwa watu. Mfumo wa CCM asili yake ni China kwani mwalimu alichukua mengi Kule. Hata hivyo wenzetu mfumo umesha badirika sana (evolve) kutoka enzi za Mao ambapo madaraka yote yalikuwa yamerundikwa kwa mtu mmoja, Mao, hadi enzi za kina Deng Xiao Ping ambapo Politburo ilichukua powers.

General secretary wa Chinese Communist party hana powers alizo nazo Mwenyekiti wa CCM Leo. Kwa hiyo wakati CCM imebaki na mfumo wa Ki Mao Mao, wenzetu huko walishatoka. Politburo is very strong and above any one individual. CCM central committee ambayo tunaweza ifananisha na Politburo ya wachina, haina powers zozote over the president and chairman wa CCM. Nadhani hiyo ni big difference and you can see the results are very different
 
Nimeanza kurudisha imani yangu Jamii Forum. Hii ndio Jamii forum nilikuwa ninaifahamu, wanafalsafa wanagusa magombo ya Legendaries

Mkuu kwanini Politburo ina power, kwasababu its made of very few powerful minds. Currently wako saba tu. na hii ndio pia the Heart of Chinese system, hawa wana uwezo wa kumwambia President "NO".
CC ya CCM wako ngapi wale, unakuta wamo hadi akina Wema Sepetu, Jerry Slaa. Seriously, what do u think mayor wa Ilala anaweza kumwambia President?
 
Back
Top Bottom