Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 10,027
- 20,912
Ukiwa ni mfuatiliaji wa siasa za dunia utagundua kitu kimoja kuwa kwenye nchi nyingi sana duniani kama sio zote systems zina mchango mkubwa sana kwenye kupatikana viongozi wanaoziongoza nchi izo. Hii ni kuanzia Nchi tajiri hadi Nchi masikini. Nitatoa maelezo vizuri kidogo ili niweze kueleweka vizuri.
Kwenye nchi zote duniani kuna vitengo vyao vya intellejensia ambavyo kazi kubwa ni kusoma siasa na hali za uchumi za nchi husika na za nchi za dunia na hivo vitengo kazi yake kubwa ni kubashiri au hata kupanga kuwa kwa hali ilivo nchini na kwa hali ilivo duniani ni vizuri tukapata kiongozi au tukawa na kiongozi wa aina fulani ili kwanza nchi iweze kutulia na pili nchi iweze kusonga mbele. Hivi vitengo huwa vinastudy hadi sera za nchi fulani na kutoa ushauri kwenye nchi zao kuwa kutokana na nchi fulani kuchukua sera fulani basi nasi tuchukue njia fulani ili tu uchumi wa nchi na hali ya nchi iwe salama.
Ndo mana kama urusi unaona system inambakisha putin ili aweze kutengeneza watu wengi wa aina yake kwa ajili ya kuweza kupambana na hila za marekani kwa mustakabali wa nchi ya urusi, ndo mana hata china system saivi inatengeneza viongozi wenye kaliba ya unyenyekevu na upole kwa sababu china saivi inajijenga kimataifa ili kuwa nchi yenye ushawishi kibiashara duniani mfano waangalie raisi wa china aliyepita na huyu wa sasa xi jiping.
Ndo mana mnaona Iran inabadilisha viongozi kutoka mwenye msimamo mkali aliyeijenga irani kijeshi Mahmoud Ahmadinejad na huyu wa sasa mwenye hulka ya upole Hassan Rouhan kwa sababu tu wameona watulize mgogoro wao na marekani ili waweze kujijenga kiuchumi. Ndo mana kuna hata watu wanasema kuwa J.F Kennedy aliuawa na system yenyewe ya marekani baada ya kuona kuwa kuna mambo alikuwa akienda against nayo kwa mujibu wa mipango yao.
Nimesema haya kutokana na jambo lililo midomoni mwa watanzania wengi kuanzia siku ya jana hadi leo hii nalo ni kutangaza nia na kuchukua fomu kwa nguli wa sheria duniani Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani. Kuna watu wanasema kuwa huyu ni chaguo la system na wengine wanasema huyu ni chaguo na Kikwete.
Kuna kitu nimekiwaza sana na sidhani kama kweli ni system ndo imeshauri ivo ilikuwa makini kwa kuelewa tatizo letu Tanzania ni nini na tufanyeje ili kutoka hapa na ndo mana nimeamua kuandika hii thread. Kama tuna system makini lazima itajua kwa sasa Tanzania tunaitaji kiongozi wa namna gani. Na kama huyu ni chaguo la mkuu basi mkuu inabidi atafakari sana na washauri wake kama wana mapenzi mazuri na vizazi vyao huko mbeleni.
Hata kama umeshuka leo kutoka nchi jirani ukizunguka mikoa 5 tu na kuwauliza watu 20 kwenye kila mkoa watakwambia tatizo kubwa la Tanzania nchi haiendi, watu wanachukuliana poa, hamna userious kwenyew kazi na kuwahudumia wananchi,watakwambia kuna tatizo la rushwa na upigaji yani kila mtu ni mwizi na anataka apate nafasi aibe, watakwambia kuna matatizo ya afya,elimu,maji, miradi kutokamilika kwa wakati na watu kula fedha za miradi na watakwambia pia kun a utekelezaji wa miradi chini ya kiwango.
Ukitoka hapo ukifanya study ya jamii ya watanzania hata kwa miezi miwili tu, kwa kuanzia kwenye maofisi,kwenye television na mijadala inayofanyikaga kwenye television na hata kwenye vijiwe utagundua kitu kimoja kuwa watanzania ni watu wa porojo na siasa sana. Ni watu wa maneno mengi na kulalamika si maofisini,si vijiweni, si kwenye mitaa na vijiwe na si kwenye kwenye kumbi za starehe.
Utagundua kuwa kuna opportunities nyingi sana Tanzania ila wazawa hawazitumii na wageni kutoka kenya,south africa na zimbabwe wanakuja wanazitumia na kutengeneza mamilioni ya fedha kila siku. Utagundua kuna tatizo kubwa sana kwenye mifumo ya uli[paji kodi na wananchi wengi sana hawalipi kodi, utagundua kuna ukwepaji mkubwa sana wa kodi unaoikosesha serikali mapato mengi sana.
Sasa kama tungekuwa na system makini iyo system ingeweza kuyaona haya yote na siku ya mwisho ndo ingeshauri nani wa kumpa hii dola ili arekebishe haya yote. Sishani kwa system makini ingependekeza mtu mpole, mkimya na asiyeweza kukemea kama Jaji Agustino Ramadhani.
Sina mashaka na weredi,uadilifu na hekima za Jaji Ramadhani ila kama kweli yeye ndo chaguo la watu fulani kama wanavojulikana "The System" basi watakuwa wamekosea sana kwa sababu Tanzania kwa ilipofika hapa na dunia inavokimbia bila shaka tunaitaji watu aina ya Prof Muhongo au John Pombe Magufuli. Tutadanganyana sana ila siku ya mwisho huu ndo ukweli na utabaki kuwa ukweli.
Kama nilivoandika kwenye post inayomuhusu Jaji Ramadhani napenda nirudie tena hapa na someni tena ndugu zanguni
Asubuhi njema ndugu zanguni

- TANZANIA INAITAJI MTU SERIOUS, MTU MKALI NA MFUATILIAJI WA MAMBO, MTU ASIYE MPOLE NA ANAYEJUA TATIZO KUU LA WATANZANIA NI UVIVU, KUPENDA POROJO, KUENDEKEZA SIASA KILA MAHALI NA KUTOJITUMA. TATIZO LA TANZANIA NI KUKOSA MTU THABITI MWENYE MAONO FULANI JUU YA UCHUMI WA NCHI NA UCHUMI WA DUNIA AMBAPO HAPA SIDHANI KAMA ATAFIT VIZURI. SIDHANI KAMA ATAWEZA KUPAMBANA NA FITNA ZA KINA MEDIA TYCOON AMBAO WAKIKOSA VITU WANAVYOVITAKA WANAANZA KUIYUMBISHA SERIKALI NA WATENDAJI WAKE KAMA WAPENDAVYO.SIDHANI KAMA ATAWEZA KULISIMAMIA BARAZA LAKE LA MAWAZIRI LIWEZE KUDERIVER KWENYE STANDARDS ZA JUU KABISA INAVOTAKIWA.
Asubuhi njema ndugu zanguni