Kama ni kweli basi mabenki yatafungwa na uchumi kudorora kuakisi umasikini zaidi

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,945
Kuna habari zinazozunguuka mtandaoni kwamba kuanzia julai 2017 mishahara ya watumishi wa umma kulipwa kupitia benki kuu yaani BOT moja kwa moja bila kupitia kwenye mabenki ya biashara, kama ni kweli pesa hazitapitia benki za biashara kuna hatari ya anguko zaidi la mabenki.

Aidha bado fedha zilizokua zinapitia katika mzunguuko baina ya taasisi na mashirika ya umma na benki za biashara sasa zinakwenda moja kwa moja benki kuu hazipitii mabenki ya biashara kama ilivyokua miaka ya awamu zote, kama ni hivyo kutakua na mdororo wa mabenki kunyimwa mzunguuko wa fedha.
 
Uzushi, hakuna ukweli wowote hapo. Elewa kwanza mfumo wa utendaji kazi wa Benki kuu.
 
Embu soma hiyo taarifa vizuri! BOT ina mtandao wa kutosha wa matawi kumudu kazi hiyo kweli?!
 
Bai itabidi benki kuu iwe na branch mikoa yote na wilayani pia, na hapo itapoteza maana ya ukuu wake, itabidi kiundwe chombo kingine cha kusimamia mabenki.
 
umekurupuka, hata sasa mishahara inalipwa moja kwa moja kutoka hazina kwenda kwenye ac za watumishi, kuhusu fedha za mashirika ya umma kukusanywa BOT pia linafanyika hata sasa. lkn serikal inasambaza fedha kwe taasisi kupitia mabenk ya kibiashara. hata wazabun wanaingiziwa fedha za mirad kupitia mabenki ya kibiashara. tatizo liko wapi hapo? au ndo ukilaza/unyumbu.
 
Wewe si mwalimu mzuri, au ni mwanafunzi asieelewa swali. Mwenzio anaomba ufafanuzi halafu wewe unamtukuna !! Kweli duniani kuna mambo !!?
 
Kuna habari zinazozunguuka mtandaoni kwamba kuanzia julai 2017 mishahara ya watumishi wa umma kulipwa kupitia benki kuu yaani BOT moja kwa moja bila kupitia kwenye mabenki ya biashara, kama ni kweli pesa hazitapitia benki za biashara kuna hatari ya anguko zaidi la mabenki, Aidha bado fedha zilizokua zinapitia katika mzunguuko baina ya taasisi na mashirika ya umma na benki za biashara sasa zinakwenda moja kwa moja benki kuu hazipitii mabenki ya biashara kama ilivyokua miaka ya awamu zote,
kama ni hivyo kutakua na mdororo wa mabenki kunyimwa mzunguuko wa fedha
Ni uzishi huu , Benki kuu ndiyo itakuwa inaingiza Fedha za watumishi kwenda mabenki mengine yanayotumiwa na Taasisi sasa mtu unakuja na hadithi zako za kutunga hapa.
 
Ni uzishi huu , Benki kuu ndiyo itakuwa inaingiza Fedha za watumishi kwenda mabenki mengine yanayotumiwa na Taasisi sasa mtu unakuja na hadithi zako za kutunga hapa.

Afadhali umekua mkweli maana watu wanakurupuka na kupost tu daah aje Waziri fedha na Waziri utumishi wafafanue hapa
 
Tatizo la Watanzania huwa tunasoma habari au kusikiliza habari ili tupate cha kujibu au cha kuongea....hivyo tunasoma habari huku tukiwa na majibu au hukumu zetu kichwani.....

Unatakiwa usome habari au kusikia habari kwa makini ili uielewe na kisha kutoa maoni yako....
 
Ok boss
 
Back
Top Bottom