JERUSALEMU
JF-Expert Member
- Sep 19, 2012
- 3,112
- 3,536
Habari wanajamvi!
Sijaamini maneno ya msemaji wa chama cha Mapinduzi labda nitaaminishwa baadae. Kwa maneno yake Katibu mwenezi anasema ni kweli mwanasiasa nguli na Katibu Mkuu wa chama cha mapinduzi comrade Alhajji Abdulrahman Kinana alikuwa anaumwa, na alipelekwa nje ya Nchi kwaajili ya matibabu,lakini kwa sasa amerudi yupo Nchini anapumzika nyumbani kwake! Hajafafanua kama ni Dar es salaam au Arusha. Nikajiuliza maswali yafuatayo;
- Hivi inawezekana kweli Katibu Mkuu wa chama arudi kutoka kwenye matibabu halafu asipokelewe na Mtu yeyote pale Airport? Hata ndugu zake hawakwenda kumlaki? Yaani asionekane na mwandishi wa habari hata mmoja?
- Tuseme yupo nyumbani kweli anaendelea kupumzika baada ya matibabu na huenda ana ED za miezi miwili au mitatu, lakini hakuna hata mtu mmoja alie kwenda kumpa pole? Yaani hata katibu mwenezi Naibu katibu mkuu hawajaenda kumpa pole!
- Yaani hata viongozi wote wanao julikana kwa uungwana wao wa asili kama Mbowe, Maalimu Seif, n.k Hawajaenda kumjulia hali? Nini kimetokea?
Ndio maana nikaishia kusema kama ni kweli kuwa Comrade Alhajji Abdulrahmani Kinana amerudi yuko nyumbani na hakuna mtu hasa wanao penda kuonekana kwenye vyombo vya habari, basi ni dhahiri ndugu yetu amedharauliwa na kupuuzwa.
Binafsi naomba wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari kampeni pole kwa niaba yangu.