WAKABAMBEE
JF-Expert Member
- Feb 3, 2012
- 605
- 275
Habari wanajamvi,leo nikiwa nimetoka k,koo naelekea zangu makumbusho ofisini kwangu,nilikuwa kwenye daladala.mara kukazuka story kuhusiana na meya wa jiji la DSM,kuna jamaaa kaongea jambo ambalo imenibidi niamini kwa kiasi fulani hasa kutokana na figisufigisu zilizotokea.jamaa anadai ya kwamba ccm wana mpango wa kuwanunua madiwani 11kutoka ukaww ili wampigie kura mgombea wa ccm.jamaa akaenda mbali zaidi na kusema hadi sasa wamefanikiwa kurubuni na kuwapa pesa madiwani 6 bado wa5 ili kazi iishe na ndipo waitishe uchaguzi,inasemekana wanachelewesha kwa sababu wanataka wahakikishe wamewapata hao wajumbe 11 na ndipo waitishe uchaguzi,,sasa kama ni kweli hizo habari basi ccm hawawezekani na ni bora mtu ufanye shughuri zako za kimaisha kuliko kufuatilia siasa za africa maba zote zipo sawa,laaana hii sijui tuliachiwa na nani ya kutofuata democracy
jamaa anadai ya kwamba ccm wana mpango wa kuwanunua madiwani 11kutoka ukaww ili wampigie kura mgombea wa ccm.jamaa akaenda mbali zaidi na kusema hadi sasa wamefanikiwa kurubuni na kuwapa pesa madiwani 6 bado wa5 ili kazi iishe na ndipo waitishe uchaguzi,inasemekana wanachelewesha kwa sababu wanataka wahakikishe wamewapata hao wajumbe 11 na ndipo waitishe uchaguzi,
Mkuu Nifah nawe umekata tamaa? Kama ni kweli hao watu wamenunuliwa basi hata ije katiba mpya usitegemee chochote maana hawa wanaonunuliwa ndio hao hao tutakuwa nao kwenye katiba mpyaSio umeya tu,hata Zanzibar mpaka sasa CCM ndio washindi.
Tutakapoweza kuing'oa CCM madarakani,na ni baada ya kupata katiba mpya pendekezwa ndipo tutakapoweza kufanya ya maana,tofauti na hapo ni ngumu kuzuia figisu figisu za CCM.
Huku kuwanunua watu ndio kujisahihisha? Basi shughuli bado pevuhamuiwezi ccm kwa sababu hamna watu wanaojua siasa, mageuzi ni safari ndefu siyo swala la kuamka na kuchukua nchi.wakati wananchi wameanza kupata mwamko wa mageuzi kwa kauli mbiu ya vita vya ufisadi ghafla mkawasaliti wananchi na kumchukua fisadi nkuwa mgombea wenu wa urais,kitendo hicho si tu kiliwachanganya wananchi bali kilirudisha nyuma mageuzi ya ukweli na kuwapa nafasi ccm ya kujisahihisha kwani wametambua wananchi wanataka mabadiliko na hawataki ufisadi sasa hivi kila mtu anaongelea kutumbua majipu na sio tena ufisadi kwani kiongozi wa mafisadi tayari amehamia kule walikoanza kumwita fisadi
ccm ina mbinu za kishamba sana !Huyo ni kada wa ccm tu alikuwa anapima kina cha maji na kusikia ya upande
mwingine hana lolote! Kawakuta nyie wasikilizaji wa mabadiliko mkaogopa; wangekuwepo makamanda wa kweli angewataja hao anaojidai
wameshanunuliwa; vinginevyo wangekiona kilichomnyoa kanga manyoya!
Hivi Ni Kweli tunaweza kuzeeka bila Kuona MABADILIKO yeyote? Hii kitu inauma sana, binafsi nilikua naamini kizazi chetu Ndio Muda muafaka wa kufanya MABADILIKO ya Kweli Kama kizazi cha Miaka ya 1950s-1960s.. Ila kwa jinsi upepo unavyovuma Ni Kama vile Hakuna lolote litakalofanyika, hii kitu inaniuma sana sio Siri.Sio umeya tu,hata Zanzibar mpaka sasa CCM ndio washindi.
Tutakapoweza kuing'oa CCM madarakani,na ni baada ya kupata katiba mpya pendekezwa ndipo tutakapoweza kufanya ya maana,tofauti na hapo ni ngumu kuzuia figisu figisu za CCM.
Mkuu hawa watu ni wapuuzi sana, mwaka wa Jana wamekausha Hazina weee kwa mambo km haya ona sasa tunavyoisoma namba, naichukia CCM acha tuMsiogope tupo imara