Kama ni huyu mbakwaji na kapuya, kapuya is innocent, kabisaaa!

Ukiwa mwongo jaribu kukumbuka vitu vidogo vidogo ulivyosema mwanzo. Kwa taarifa zilizopo ambazo hata Kapuya mwenyewe kazibitisha, kwa sasa binti ana miaka 16, kwahiyo basi 1999 alikuwa na umri wa miaka 2. Bila kupepesa macho hapa Kapuya hachomoki labda kwa kudra za GAMBA tu otherwise.

nani kakwambia huyo binti ana miaka 16..una uhakika katamka kapuya?
 
naona kuna pande mbili, yawezekana kapuya aliingia mkenge pasipo kujua wasifu wa huyo dada! na baadae akashindwa kujinasua anataka atumie nguvu aliyokuwa nayo pamoja na vitisho akidhani atafanikiwa
 
Kaka mbona unatoka Povu sana kwa hili, Kwa nini unakuwa biased na upande mmoja tu?, Hivi kweli hauoni tofauti ya Habari ya Tanzania Daima na ile ya Global Publishers? Kwa habari kama hizi ni kukaa kimya kwanza na siokufanya conclusion ya moja kwa moja, Kuna uwezekano mkubwa sana kuwa change Kota imefanyika, kati ya halisi na kanjanja.

ni kweli Kuna uwezekano kabisa huyo aliyeoneshwa na Global publisher ana tabia ya kusingizia watu na inawezekana pia ni kweli na wewe alikuingiza kwenye mtego, lakini swali ni hili HUYO MSICHAN NDIYE YEYE ANAEZUNGUMZWA NA TANZANIA DAIMA?
Mkuu Kituko,
Mimi binafsi hata ule uzi wa Tanzania Daima nao una scratches za hapa pale, labda nisaidie wewe kunijuza manake binafsi nimejiuliza maswali kadhaa ambayo nimekosa majibu. Kwenye ule uzi wa Tanzania Daima, tujikite kwenye paragraph tatu za mwisho ambazo mwandishi anadai kwamba baada ya kupigwa changa la macho kule Dom, hao mabinti wakaibukia ofisi za CCM Lumumba. Maelezo ya mwandishi yanaendelea kusema kwamba, baada ya kutoka pale Lumumba, wakawa wanaelekea kituo cha daladala lakini kabla hawajafika, mara akatokea mwanafunzi mwingine akamwambia kuna watu wanataka kumwagia tindikali. Binti kusikia hivyo, akakimbia to the point kwamba akapotea hadi alipookotwa na mama mmoja ambae alikata shauri la kumpeleka Channel 10. Akiwa huko Ch10, wakaja wale jamaa waliokuwa wanataka kummwagia tindikali lakini watu wa pale Ch10 wakakataza hao watu kuondoka na huyo binti. Ni katika mazingira hayo ndipo mwandishi wa Tanzania Daima alimkuta hapo Ch10 wakati hao jamaa wa tindikali wakiwa bado wapo!! Hayo ndo maelezo ya Tanzania Daima kwenye aya tatu za mwisho. Now questions:

>>>Je, hivi inawezekana kweli watu wamwagie binti tindikali mchana kweupe maeneo ya Mnazi Mmoja ambayo huwa na watu wengi? Ukumbuke kwamba, alishituliwa kwamba anataka kumwagiwa tindikali wakati anatoka hapo CCM kuelekea kituo cha daladala....na katika kukimbia Tanzania Daima linasema msichana huyo akaingia barabara ya Starlight Hotel, so there's no doubt kwamba tukio lilitaka kufanyika Mnazi Mmoja! Does it bring any sense? Kwanini asingesubiriwa mitaa kwao ambako kulikuwa unafahamika ambako pia "muuaji jambazi sugu wa kwanza alienda?"

>>>Swali la pili, baada ya binti kukimbia alipotea na baada ya kuuliza, ndipo mama mmoja akaamua kumpeleka Ch10! Kwanini ampeleke Ch10 wakati huyo binti sio mgeni hapa Dar? Kwanini tu asingemuonesha kilipo kituo cha daladala? Hivi kweli kwa maeneo ya katikati ya jiji kwa mwenyeji wa Dar es salaam anaweza kushindwa at least ku-guess direction ya posta mpya au posta ya zamani? Ilikuwaje apelekwe Ch10? Ikiwa maisha yake yalikuwa hatarini kiasi hicho(kumwagiwa tindikali mchana kweupe) kwanini hakumuomba huyo mama amwelekeze kilipo kituo cha polisi ili wamwakikishie ulinzi wake hadi anafika nyumbani?

>>>Swali la tatu, ikiwa huyu binti alikimbia hadi kupotea, it's no doubt kwamba aliwapoteza hata wabaya wake waliokuwa wanamfuata! Sasa kama ndivyo, ilikuwaje tena wakakutana chumba cha habari Ch10? Hawa watu wa Tindikali walifahamu vipi kwamba yupo/angekwenda Ch10 wakati lengo la awali la binti huyo ilikuwa ni kwenda kupanda daladala?!

>>>Swali la nne; huyo binti anaonekana ni jasiri asiyeogopa kusema ukweli! So, baada ya kufika hapo Ch10 bila shaka alisema ukweli kwamba amewakimbia watu waliotaka kumwagia tindikali! Sasa basi, hao watu ambao nao walikuwa hapo Ch10 walipata wapi ujasiri huo wa kumfuata hadi hapo? Kama walimkuta, ina maana alishasema ukweli ingawaje swali linarudi palepale kwamba walifahamu vp kwamba yupo pale! Kama wao ndio wa kwanza, bado swali linabaki palepale, walifahamu vipi kwamba angefika hapo?

>>>Swali la tano, pale Ch10 kauli ambayo ilipewa uzito ni kuwataka mabwana tindikali kutoondoka na huyo binti! Hivi kweli katika serious issue( ya kumwagia tindikali) kama hiyo ilitosha tu kuwaambia hao jamaa wasiondoke na huyo binti bila kujali wht would happen to her akishatoka hapo Ch10? Hivi kweli hii haikuwa habari ambayo hata Ch10 nao walipaswa kuitangaza kwenye kituo chao? Kwanini wasitangaze sakata la watu wawili waliokuwa wanataka kumwagia tindikali binti mdogo?
>>>Swali la sita, mwandishi wa Tanzania Daima anasema alipofika hapo Ch10 ndipo alikuta hao jamaa wanataka kuondoka na huyo binti lakini watu wa Ch10 wakawagoma! Sasa huyu mwandishi alifika hapa wakati akitokea wapi? Alipigiwa simu, au?Ikiwa mwandishi alifika na kuwakuta watu wa tindikali bado wapo basi it's obvious kwamba huyo mwandishi alifika mapema sana eneo la tukio! Did he expect this call, or? Au pale Ch10 kuna waandishi ambao pia wanaliandikia Tanzania Daima?

Nisaidie wewe manake mie nimeshindwa kupata majibu!!
 
Last edited by a moderator:
unaweza ukasema hivyo ila yakikupata na ukikuutana na Halima akakuset utaelewa nina maana gani! kwa sasa sema tuu! Ila kama una muda fuatilia mafailai ya mtoto huyo polisi urafiki, she is just like that!
Atakuset vipi kama na wewe huna elements za umalaya? Unaacha kufuata wakubwa wenzio mnatafuta dezodezo kwa vitoto. Mkubwa mwenzio atakutoa kamasi ehh?
 
Na wewe una kiherehere kama mbwa jike. Wewe na nani mnamjua mbakwaji? Anaitwa nani? Mmemjuaje? Na kwa nini kama mnamjua hamjamsaidia hadi hivi sasa?

Mkuu
user-offline.png
Nyani Ngabu, inaonekana unazo source nzuri Global Publishers, hebu tuhabarishe huyu shahidi aliyefichwa uso hapa chini ni nani na ilikuwaje akaunganishwa na mtuhumiwa Kapuya.

attachment.php


attachment.php


Nahisi kuna mchezo mchafu unachezwa humu kuhusiana na hili sakata na ukiiangalia kwa makini body language ya huyu binti na body language ya huyo kwenye video ni kama usiku na mchana...kaazi kwako!

source: KAPUYA, DENTI KIFO NJE NJE - Global Publishers
 
Mkuu Kituko,
Mimi binafsi hata ule uzi wa Tanzania Daima nao una scratches za hapa pale,Nisaidie wewe manake mie nimeshindwa kupata majibu!!


Great Thinker NasDaz,

Ni ukweli usiopingika kuwa kuna inconsitance ya hapa na pale kwenye maelezo yaliyomo kwenye gazeti la Tanzania Daima, na hayo uliyoyaweka ni miongoni wa hayo maelezo yasiyoukuwa na mfuatano sahihi wa kimatukio.

Kuna Hoja ambazo ziko kwenye hilo gazeti ambazo hazikumpasa Kapuya kutoa notice ya siku saba kwa sababu zilikuwa na instant demage kubwa sana kwake, ilimpasa Kapuya kulishitaki hilo gazeti na huyo mtoto onspot.
1. Hoja ya kwamba alimbaka huyo mtoto Hapo Mwanayamala (ofisin kwake), kisha kesi ikaenda Police Oysterbay na kisha makubaliano ya kutoa pesa ya mwezi yakafikiwa
2. hoja ya kusulishwa na WanaBunge wenzie kule Dodoma
3. Hoja ya Kusuluishwa na wana CCM pale Lumumba
4. Hoja ya kupeleka Benz
5. Hoja ya kutuma pesa kwa M-pesa
6. Hoja ya kutuma SMS za vitisho

Swali ni Hili Kapuya atenda Mahakamani kushtaki baada ya hizo siku saba alizotoa kwenye Gazeti la Tanzania Daima na Mitandao ya Kijamii? na kwa nini atoe rai ya kustaki gazeti na mitandao na wala sio kumshtaki huyo mtoto kwa kumsingizia na kumwaribia heshima yake?

Kaka hii hoja imeshaingia siasa, na Kapuya kwa kutokujua ameingiza siasa kwenye hii Hoja, Kauli ya Kova mwanzo ilikuwa kwa upande mmoja inamkinga Kapuya lakini sasa kuna mabadiliko makubwa ya kauli ya Kova hasa baada ya Mwema kutoa kauli,
kapuya alilikoroga hapa
1. Kitendo cha kuandika msg kuwa watoto wake wanauza Unga na wanaendelea kuishi bila shida (Tetesi zilishakuwa mda mrefu kuhusu watoto wa vigogo na biashara ya unga), ni kiashirio kuwa serikali ya JK pamoja na Jeshi zima la polisi linalinda genge la waarifu, Hii kauli haiwezi kumfurahisha JK na kwa njia moja ama nyingine lazima atamtenga Kapuya kwenye hili
2. Kitendo cha kusema yeye ni PM mtarajiwa nalo haliwezi kuwa na baraka kwa JK, kwani Kapuya ni team Lowassa ambayo haina support ya JK ambaye yupo team Membe

Kama Global Publishers wananunulika na team Lowassa, Tanzania Daima lazima watakuwa wanapata info sio kutoka kwa hao watoto pekee, bali na wapinzani wa hiyo team lowassa

Ni maoni yangu tu kaka
 
Last edited by a moderator:
ona sasa unavyozidi kijichanganya,kwa iyo ukaona uyo halima humud unayemfahamu ndio uyo aliyebakwa na kapuya,tatizo lako unakuwa bias kwa kuegemea upande mmoja,ndio maana tumechakuona we ni mamluki tu huna jipya,yaani unashindwa kuelewa mchezo unavyochezwa apa.

kosa kubwa kambi ya kapuya mmlilofanya ni kutokaa pamoja na kutunga uongo unaofanana,kama mngekaa pamoja bila kukulupuka na kutunga uwongo mmoja unaofanaa maybe mngeeleweka japo 50%,tatizo lenu mara kapuya anasema ivi,mwanasheria wake anasema ivi, na kasimba naye anasema vingine.
kijana basi kama unauwezo wa kuconvice watu,nenda umukonvice mke wa kapuya kuwa mumewe ni mwaminifu katika ndoa.

Sijawa biased ila nataka kuiponya jamii na watu design hii, pinch yake huijui mkuu!
 
naona kuna pande mbili, yawezekana kapuya aliingia mkenge pasipo kujua wasifu wa huyo dada! na baadae akashindwa kujinasua anataka atumie nguvu aliyokuwa nayo pamoja na vitisho akidhani atafanikiwa

Nakuambia huyo dada ni anajua kutunga mambo balaa, nimegusia kuwa hata clouds fm walikuwa wakimtumia kwenye kipindi chao cha watoto, nadhani kama mnataka ushahidi wa kina kaulizeni clouds fm watakuwa na taarifa za kutosha za Felister, a.k.a Halima!
 
Mods tafadhali msiunganishe uzi huu na mwingine!

Kama ni huyo Halima Humud a.k.a Whatever name ndie mtuhumuwa wa kubakwa na J A Kapuya, hilo suala litakuwa la kusukwa! Huyo Binti ninamfahamu tokea akiwa na umri wa miaka kama 7 au 8 hivi, akiwa anaishi sinza madukani karibu na shule ya Iteba pembezoni mwa mto!

Binti huyo kishawahi kuwaumiza wengi, mimi mwenyewe nikiwa mmojawapo, binti ni yatima kweli, ana mdogo wake wa kike na kaka na dada zake, kwakweli familia yao mimi naifahamu kwa kina. Huyo binti kabla sijasimulia kitu gani kiliishawahi kunipata mimi binafsi, kwanza nieleze mkasa wa rafiki yangu mmoja Jina nalihifadhi. Mwaka 1999, binti huyo wakishirikiana na familia yake, walimtega collage mate wangu kwa kesi ya kubaka, Ilimsababishia rafiki yangu frustrations sio za kawaida, nadhani mpaka leo hii hayupo hapa Tanzania kwa sababu ya binti huyo, walikuwa wakifanya matukio yao professionally, very very, nadhani kuna mwanasheria mshenzi alikuwa nyuma yao na ndie alikuwa akiwapa maelekezo!

Approach yao, kwakuwa hiyo familia ilikuwa ni ya yatima, kwa mtu yeyote mwenye utu utafikilia kuwasaidia, rafiki yangu alijitolea kuwasaidia, lakini mwisho wa siku wakamtungia uwongo kuwa kambaka huyo huyo Halima Humud! By then tukio kama hilo halikuwa common huku kwetu Tanzania, watu wengi waliamaini, jamaa akawa kwenye depression kaali kabisa, bahati nzuri watu wakamtafutia scholaship kwenda nje.

Binti huyo, mala nyingi hushirikiana na mwanasheria mmoja mtukutu na mapolisi wasio waaminifu na kaka yake, jina nalihifadhi ambaye ni jambazi, sijui kama huyo kaka yake yupo hai mpaka leo hii ninapoandika ujumbe huu.

Ni kweli binti huyo hubadili majina kila uchao, ameshawahi fanya kazi part time clouds radio kipindi cha watoto, na nimuongeaji, ana ushawishi wa maneno saana kiasi cha kuwa unaweza kuamini mambo ayasemayo, kisa haswa kilikuwa kinasababisha familia yake imuamini katika kuframe kesi kama hiyo, hao watoto yatima walikuwa wakiishi na mama yao mkubwa hapo maeneo ya Iteba kama nilivyo andika hapo awali, Nesi, HALIMA HUMUD!

Kwa upande, nilikuwa sina taarifa za uhusika wa familia hiyo kwa rafiki yangu, kuna siku wakanipata na mimi, Tukio lenyewe lilianza hivi, Nilikuwa by then sina gari nategemea usafiri wa daladala, nikashuka kwenye daladala, nikashuka naye huyo Halima Humud, nikiwa naelekea nyumbani kwangu, huyo mtoto akiwa amevaa sare zake za shule, alianza kuniomba msaada wa kujua mahakama ya kinondoni ikowapi, bila kusita nikamuambia Binti umepotea, panda gari la msasani then shuka kituo husika utakuta hiyo mahakama.

Tukio hili lilisababisha nimuulize kulikoni? Akanisimulia kisa cha kupigwa panga na mama yake mkubwa kichwani, na akanieleza kuwa yeye ni yatima, kwa kweli roho ya huruma ilkaniingia, nikamuuliza anapokaa, akanieleza, nikamuuliza kama ana dada zake wakubwa na kaka zake, akasema anao, nikamuelekeza sehemu ninayo kaa na kumuambia akawaite dada zake na kaka zake ili nijue mkasa mzima, kweli akafanya hivyo, pasi kujua kuwa ile ni familia ya waovu! Nikawauliza maisha yao, wakanisimulia, kwakweli nikaingia huruma, nikaanza kuwasaidia, by then ni fresh graduate ndio tuu nimetoka UDSM sina hata uwezo kihivyoo!

Nakumbuka siku moja najirudia nyumbani kwangu nakuta polisi wamekuja kunichukua kwa kesi ya kumbka HALIMA HUMUD! Nikahuzunika na nikaenda kulalal ndanikwenye kituo cha urafiki, huko haswa ndiko HALIMA HUMUD na lawyer wake na Polisi waovu, walikuwa na Kundi lao!

Kwahiyo kesi ya rafiki yangu ilikuwa kituo hichohicho, kesi ya namna ileile, kumbaka HALIMA HUMUD!, na mimi nikapata kesi ya namna ileile ya kumbaka HALIMA HUMUD, kwa kweli hiyo familia baada ya kunisakizia mimi, ilisambaratika, you know what happened? Nilikuwa naset nao meeting kila baada ya muda furani eti tu-settle out of court, criminal case! Nikawa nawarekodi madai yao, bahati mbaya kuna siku wakajua kuwa nilikuwa nawavideo record, wakakimbia na wakahama sehemu walikuwa wanakaa na wakauza nyumba yao na wakawa watoto wa mtaani since then!

Kuna siku nikakutana na huyo Halima, akaniambia ati ndugu zake wengi waliohusika kwenye mkasa wangu wamekufa hivyo ananiomba msamaha, mimi nikamuambia amuombe Mungu msamaha sio mimi! Nikamuhoji je ni watu wangapi waliwafanyia kitu walichonifanyia mimi, akaniambia ni wengi, waliishawahi kufanya mikocheni na sehemu nyingine nyiingi tuu baada ya kunifanyia mimi wakasambaratika, akiamini kuwa mimi labda ni mchawi!

nikajaribu kufuatilia, ni kweli baada ya tukio langu, familia ilisamabalatika, lakini nashangaa kumsikia kwa Kapuya tena! Nilihisi ni yeye the very first day, Le Mutus akatoa maada yake humu nikamuhoji je ni nani? i mean nikitaka anipe details za huyo binti, nikajua ni Halima Humud, that girl is devoulish!

Mimi nina misimamo yangu kisiasa lakini lets call a spoon, spoon, Msimuamini huyo toto hatachembe, ameanza utukutu huo tangu ana miaka 7 amezoe kwenda polisi na kutunga uongo kwa uongozi wa polisi wenyewe! nadhani kwa sasa kweli atakuwa 20z huko, imagine 1999 alikuwa na 8!

Nawasilisha!


Umeeleza "hadithi" ndefu sana ambayo inahusu sifa za huyo binti na matukio yake. Tufanye ni kweli,ila hakuna popote ulipothibitisha kuwa na la Kapuya pia ni mchezo wa huyo binti. Umeishia kutoa sifa za binti na matukio ya "maneneo ya nyuma ya keyboard" tu. Hujatuambia kuhusu sms amabazo ziliwekwa wazi kabisa,idadi ya pesa na muda. Je siyo kweli? Umemtaja Le Mutuz,ila umesahau kuwa yeye alikili kuwa huyo binti alikua na uhusiano na Kapuya! Matendo ya huyu binti hayaondoi ukweli kuwa Kapuya ni mbakaji!!!
 
Umeeleza "hadithi" ndefu sana ambayo inahusu sifa za huyo binti na matukio yake. Tufanye ni kweli,ila hakuna popote ulipothibitisha kuwa na la Kapuya pia ni mchezo wa huyo binti. Umeishia kutoa sifa za binti na matukio ya "maneneo ya nyuma ya keyboard" tu. Hujatuambia kuhusu sms amabazo ziliwekwa wazi kabisa,idadi ya pesa na muda. Je siyo kweli? Umemtaja Le Mutuz,ila umesahau kuwa yeye alikili kuwa huyo binti alikua na uhusiano na Kapuya! Matendo ya huyu binti hayaondoi ukweli kuwa Kapuya ni mbakaji!!!

Ungetaka opinion yangu ningekuambia labda wahusika walikuwa na mahusiano, ja[o siwezi prove hilo, lakini la kubakwa ni approach ya huyo binti, Fuatilia kila kitu nilichokiandiaka utaelewa! angalia majibu ya post zangu!

Huyo binti ni bad news, inabidi sometimes tu ili jamii ipone, amewafunga wengi huyo, ni mzoefu amekubuhu na ni rahisi kuaminika kwa jinsi alivyo na uwezo wa kujenga hoja, primary kalikuwaga briight hako katoto, sema kamekosa directives, ni hatari saana huyo!
 
Ungetaka opinion yangu ningekuambia labda wahusika walikuwa na mahusiano, ja[o siwezi prove hilo, lakini la kubakwa ni approach ya huyo binti, Fuatilia kila kitu nilichokiandiaka utaelewa! angalia majibu ya post zangu!

Huyo binti ni bad news, inabidi sometimes tu ili jamii ipone, amewafunga wengi huyo, ni mzoefu amekubuhu na ni rahisi kuaminika kwa jinsi alivyo na uwezo wa kujenga hoja, primary kalikuwaga briight hako katoto, sema kamekosa directives, ni hatari saana huyo!

Mwisho unataka kusema kuwa Kapuya is innocent?
 
1.natamani kupata uwaziri mkuu kabla sijazeeka-samweli sitta (mp)
2.nina maadui 11 wawili waandishi wa habari na nane wanasiasa nikiwa rais nitahakikisha wanahama nchi-bernard membe(mp)
3.division four point 29 = masters mzumbe university-nape nnauye (dc)

hao ndio walio-engineer na wanaoongoza na kusponsor mkakati wa kumchafua adui na hasimu wao mkubwa kisiasa- alhaj; juma kapuya
 
Mwisho unataka kusema kuwa Kapuya is innocent?

Somehow, sijajua kama walikuwa na mahusiano, ila kwa pattern ya huyo binti no doubt! Ukikutana naye utajua ninachokuambia is even hard to express!
 
hao ndio walio-engineer na wanaoongoza na kusponsor mkakati wa kumchafua adui na hasimu wao mkubwa kisiasa- alhaj; juma kapuya

Hebu tusiwe na mawazo mafupi kiasi hicho, mimi i was no body by then, just a fresh graduate na aliniframe, kwa nini kuwasingizia watu? Huyo mtoto ni stand alone kwa age aliyonayo kwa sasa, ana utashi na uzoefu kwa kazi hiyo!
 
I am not making politics here, huyo mtoto namjua, Halima, mgogo ana dada yake anaitwa Anna myakyusa na ni mayatima kweli ila ni wasanii na wanaijua michongo hiyo, nimekuambia alikuwa jirani, inawezekana Kapuya hajui umlri wake mi namjua, ulizia sinza madukani wanamjua shetani huyo! Nasikia hata kesi ya babu seya alikuwa mmoja wa mashahidi, we fuatilia utajua!
kwababu seya ni kosa ila kwa huyu tahira kazingiziwa??
 
Ukiwa mwongo jaribu kukumbuka vitu vidogo vidogo ulivyosema mwanzo. Kwa taarifa zilizopo ambazo hata Kapuya mwenyewe kazibitisha, kwa sasa binti ana miaka 16, kwahiyo basi 1999 alikuwa na umri wa miaka 2. Bila kupepesa macho hapa Kapuya hachomoki labda kwa kudra za GAMBA tu otherwise.

Wewe humu jamvini inaelekea ni mgeni, katika unafiki mimi sio mnafiki, just andika uzi uulizie kama nina unafiki, kwanini niliandika uzi huu? ni kwasababu nilitaka tuu kuiponya jamii na watu design hii, wewe unasema mimi ni muongo? Unanijua? Japo ungespend muda uone machapisho yangu humu! Huyo binti ni bad news au unataka mpaka yakukute wewe?

We niambie unakaa wapi harafu nimuunganishe huyo binti uone kama utachomoka! She is bad news!
 
kwababu seya ni kosa ila kwa huyu tahira kazingiziwa??

Sasa, kama huyo binti amesingizi wengi, wapo waliohuru kama mimi, wapo waliofungwa wengi tuu, sasa utasema tuwaache au utasema tufanye mpango kuwatoa waliosingiziwa na huyo binti? Babu Seya anaozea huko, na wengine wengi wasiohusika kabisa, wanaumia kisa shilingi milioni! Hebu japo kidoogo tuwe na utu!
 
Back
Top Bottom