Kama ndivyo, kuna shida. Kubwa!

Vyovyote vile:
Kama hiyo barua ilikuwa ni ya kughushi, ni kwanini mamlaka husika (Msajili) haikukanusha habari hizo?
Unyumbu wa kisiasa ni mfumo unao wezesha wanaopewa dhamana kuahirisha kufikiri kwa nafsi kwasababu ya kulitumikia kundi fulani kwa masilahi binafsi ambapo hufanya hivyo kwa kujipendekeza ama kwa uoga wa kuigiza, (unafiki), a.k.a kujizima data kwassa uchawa tuseme kuahirisha kufikiri kizalendo
 
Kuna mambo kadhaa yanakupiga chenga. Ukiyaelewa, utajua nini kipo nyuma ya upuuzi huu wa serikali;

1. Barua ile inayofanyiwa utekelezaji na DC Albert Msando, Afande Muliro na Polisi wake imekuwa addressed kwenda kanisa linaitwa The Glory Of Christ Church - GCC (hili sio kanisa linaloongozwa na Askofu Gwajima)...

2. Mpaka sasa kanisa linalodaiwa kufutiwa usajili wake lenye jina la The Glory Of Christ Tanzania Church - GCTC maarufu kama "Jumba la Ufufuo na Uzima" (ambalo ndilo kanisa halali linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima) halina barua yenye jina lao lakini wakati huohuo linaathirika kwa adhabu au matokeo yatokayo na barua ile ambayo siyo yao...

3. DC Albert Msando na wengine wanadai kuwa, barua halisi yenye jina la kanisa la Askofu Josephat Gwajima (GCTC) na kusainiwa na Registrar of Civil Society - Wizara ya mambo ya ndani ndugu Emmanuel Kihampa kwa ukamilifu wake wanayo wao kina DC Msando na Muliro na sababu wanayotoa (wasikilize kwa makini wanavyoongea) ni kwa kuwa uongozi wa kanisa unadaiwa ulikataa kuipokea barua hiyo😕😕

4. At the same time, uongozi wa kanisa la GCTC unakanusha kuwa, hawajawahi kuletewa barua yao kuwataarifu kuwa hawana uhalali tena kisheria kufurahia haki yao ya kikatiba ya kuabudu kwa kuwa wamefutiwa usajili wa taasisi yao achilia mbali kukataa kuipokea hiyo barua. Lakini kumbuka na liweke hili akilini kuwa, pamoja na yote hayo kanisa linaendelea kuathirika na adhabu wasiyohusika nayo..!!

Maswali yaliyo kwenye vichwa vya wengi ni haya:
• Kama ni hivyo, kanisa lilienda mahakamani na kufungua kesi kwa base ipi?

• Vivyohivyo lilikata rufaa kwa Waziri kwa msingi upi au kwa kutumia taarifa/barua ipi?

• Lilitumia taarifa ya barua gani maana wao hawajafutiwa usajili..
?

MAJIBU YA MASWALI HAYA NI RAHISI SANA:

1. Wewe unafikiri wangefanyeje? Maana Polisi wame trespass kwenye eneo lao, wamezuia shughuli zote zisiendelee kwa madai na taarifa potofu zilizosambaa mitandaoni na kwenye vyombo vingine vya habari. Obvious huwezi kuanza kupigana nao kimwili na mtu kichaa asiyejua anafanya nini. Ni lazima utaratibu wa kudai haki yako kisheria ufuatwe Ili kuepusha athari zingine..

2. Kwa kuwa Kuna barua inayosambaa mitandaoni na ndiyo inayosemekana kufanyiwa kazi na Polisi na DC Albert Msando, unaichukua hiyo na kuitumia kama kielelezo ili kama sio halali, basi waseme wao..

3. Ndiyo maana Wakili wa kanisa, akakata rufaa kwa Waziri. Jibu la Waziri likawa very clear kuwa, haijui barua na haijatoka wizarani kwake, Kwa hiyo hawezi kuamua rufaa ambayo kesi yake haipo ofisini kwake. Bahari mzuri ni kuwa mahakama nayo imesema hivyo hivyo, kuwa, GCTC ni taasisi halali as it is for now na ambapo maana yake waendelee na shughuli zao kama kawaida...

4. Wakili Kibatala hakuishia hapo, aliwataka wasimamizi wa sheria Polisi waliohusika na vurugu hizo kanisani pamoja Wizara kupitia ofisi ya Msajili wa taasisi za kiraia waitoe barua hiyo inayowapa uhalali wa kufanya hayo wanayoyafanya kisheria..

KWA HIYO:

√ Msingi wa mchakato wote wa kanisa ni barua iliyosambaa mitandaoni na kwenye mainstream medias zote isiyowahusu lakini ikiwaletea athari hasi wao. Kama barua imekanwa na mamlaka za serikali zinazodaiwa kuitoa, basi maana yake kila kilichofanyika ni batili na wote waliofanya hayo kwa kukosa umakini, wawajibike kulipia gharama ya hasara ya mali na muda walioisababishia taasisi

√ Na hili nadhani, Afande Jumanne Muliro RPC wa Kanda maalumu DSM anaweza kuwa kwenye position nzuri zaidi kulitolea ufafanuzi. Kwa kujibu swali moja tu. Polisi wake wanafanya nini kwenye kanisa la GCTC wakati barua inawaelekeza kwenda kwenye kanisa la GCC bila kujali ni halali au siyo halali.?
 
Serikali inaongozwa na walevi
 
Wakati mwingine akili ya kuwa nilifanya kosa huja baada ya majuto fulani
 
Haa😀😀haa

Huyu ndiye DC? Hataki kabisa kuulizwa baadhi ya maswali
 
Tatizo ni vuombo vya serikali kufanuia kazi barua haramu.
Hiyo ni uwongo. Polisi na mkuu wa wilaya hawafanyi kazi kwa barua za mitandaoni tu (bila maagizo maalum). Serikali imeamua kufanya kazi kihuni kwa mtindo wa kihuni.
 
Huko sahihi kabsa, au ilitoka bila kuwa na makubaliano.
 
Hiyo ni uwongo. Polisi na mkuu wa wilaya hawafanyi kazi kwa baraua za mitandaoni tu (bila maagizo Mwalimu). Serikali imeamua kufanya kazi kihuni kwa mtindo wa kihuni.
True. Ni mchezo wanaufanya in the Name of ....!!
 
Wajinga wanaposhika madaraka, na kuwatumia wajinga zaidi kusimamia Sheria utayaona ya wale waliowashambulia raia kisutu mahakamani na kwenda kuwatupa mabwepande, mahakama ikarule ni Haki yao kwenda mahakamani, Bado polisi wakarudi na kuonekana kuwapiga watu kama wanapiga punda!
Usisahau DC ni mjumbe wa kamata ya siasa ya Wilaya kama alivyo RC kwemye Ile ya Mkoa, na ni hivi msimamo wa Chama Cha mapinduzi ni kuhakikisha aliyeko agaisnta abduction anakua halali ya Watawala kisheria na kiharamu.
 
Iwapo ni sahihi alyoyasema Msomi Kibatala waliosimamia utekelezaji wa barua hiyo wanatakuwa wajiuzulu kutoka kwenye nyadhifa zao. Vinginevyo mamlaka za uteuzi ziwafukuze kazi.
 
Kuna habari za ndani kabisa Ila kila nikitaka kuziweka humu moyo unasita kabisa.

Ngoja nitulie TU.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…