dist111
JF-Expert Member
- Nov 29, 2012
- 3,972
- 3,588
NILIWAHI kusoma hadithi moja kwenye magazeti iliyokuwa inamhusu mkuu
mmoja wa kituo cha polisi aliyefaa kuitwa Mtu Mzima Hovyo.
Kwa mujibu wa hadithi hiyo, afande huyo, licha ya umri wake mkubwa,
alikuwa hashikiki kwa kupenda wasichana, wengine wakiwa wadogo sana
wanaofaa kuwa hata wajukuu zake! Afande huyo mkware alikuwa akiwatokea
hadi mabinti wadogo walio wachumba wa vijana wake wa kiume.
Askari wa kike wote aliamini ni wake bila kusahau wanafunzi, wakiwemo wa
sekondari. Alikuwa pia akiwasumbua, akitumia pesa zake ambazo wakati
mwingine zilitokana na rushwa kuwalaghai ili kuwapata. Lakini afande
huyo alikuwa na wivu sana kwa mkewe wa tatu ambaye alikuwa dogodogo,
baada ya wakeze wa awali kushindwa kumvumilia.
Kadhalika alikuwa akiwalinda sana mabinti zake wawili, mmoja akisoma
shule ya msingi na mwingine sekondari dhidi ya wanaume walafi kama yeye.
Afande huyo, kwa kutumia pesa zake alikuwa keshawatoa mimba mabinti
kadhaa hadi mmoja kufa na yeye akatumia nafasi yake na pesa zake kuzima
kesi hiyo. Haukupita muda, Mwenyezi Mungu akaanza kumgeuzia kibao.
Binti yake yule wa sekondari aliyekuwa akimsomesha katika shule ya bei
mbaya akakataa shule kwa kunogewa na mapenzi na kisha akapata ujauzito.
Afande kabla hajatahamaki binti yake mdogo wa shule ya msingi akabakwa,
tena jirani kabisa na kituo cha polisi ambacho yeye alikuwa bosi.
Kwa mujibu wa hadithi hiyo, afande yule alihaha sana kumtafuta aliyempa
mimba binti yake na yule aliyembaka mwanawe na alipowapata watuhumiwa
hao, nusura awaue kwa kipigo ingawa iligundulika baadaye kwamba
mtuhumiwa mmoja wapo, yule aliyehisiwa kumbaka mwanawe, hakuhusika kabisa.
Wakati hayo yanafanyika, badala ya majirani kuguswa na yaliyompata
mwenzao huyo, wengi, wakiwemo maaskari wenzake hususan wa kike aliyokuwa
wakati mwingine akitumia nafasi yake kuwanyanyasa kijinsia, walikuwa
wakishangilia na ndio waliosaidia kumkemea afande wao asiwaue watuhumiwa
wake kwa kipigo.
Adhabu dhidi ya afande huyo haikuishia hapo kwani alipata mshituko
uliyompa kiharusi baada ya kushuhudia mkewe akifanya mapenzi na fundi
aliyekuwa akimtengeneza gari lake, tena sebuleni kwake!
Wengi miongoni mwetu tumekuwa tukitaka wadogo zetu, ndugu zetu ama
wanetu, wawe watu safi katika jamii, wawe na tabia njema, wasiwe watu wa
matusi, wasipate mimba, wasibakwe na mambo kama hayo lakini tuko tayari
kuyafanya hayo ama kuyafumbia macho yanapokuwa yanawatokea watu wengine
kwa vile eti hawatuhusu!
Katika hadithi niliyowamegea, Afande nusura apagawe na kuua wakati
mwanae alipobakwa, lakini yeye alikuwa akiwalaghai mabinti wadogo ambao
akili zao bado hazijatambua sawa sawa jema na ovu kwa kuwapa vijisenti
na kufanya nao ngono. Afande wetu alipagawa kushuhudia mkewe akifanya
mapenzi na mtumishi wake wakati yeye aliona sawa tu kutembea na wake
za wenziye.
Yaani kwake ilikuwa ni hadithi ya Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu
mchungu. Ni vizuri tukakukumbuka kwamba usipende kuwafanyia wenzako
mambo ambayo wewe mwenyewe usingependa ufanyiwe kama Afande wetu. Alamsiki.
Source: Habari Leo (Nicodemus Ikonko)