pixel
JF-Expert Member
- Jun 22, 2012
- 1,630
- 406
Acha ubege wewe Mengi ndiyo enginia wa yanayomkuta kiongozi bora 2014 Prof. Muhongo, Unahitaji ushahidi gani zaidi kwani kipindi wanalumbania vitalu hukusikia au unajisahaurisha bwana kasinge. Mengi ni Fisadi mkubwa Tanzania hii amefilisi NBC kwa kugoma kulipa madeni aliyokopa, na kama ni mtu makini uliposoma ripoti ya CAG hakuna mahali panamtaja Muhongo kuchukua pesa za Escrow, pia unanisikitisha kama bado umekariri kuwa pesa zile zilikua za umma. napata wasiwasi na ufuatiliaji wako wa mambo, rais alikiri kuwa pesa zile hazikua za umma upo mzee, acha porojo zisizo na mantiki, tunataka maendeleo hatutaki porojo na ushabiki wa kisiasa.
1.Mengi kulumbania vitalu sio kosa mkuu,ni sawa na mtanzania akidai serikali impe elimu.
2.Kuhusu Mengi kukopa NBC,Mengi alikopa sio aliiba.hata hivyo aliwahi kuonyesha risiti analipa kidogo kidogo.ule ni mkopo.watu wote duniani wanakopa.
3.Ripoti ya CAG haiwezi kumtaja Muhongo,sio kwasababu hana kosa bali hadidu za rejea ndio frame work yao.
4.Hakuna sehemu iliyosema Muhongo amepatikana na kosa la kula hela ya Escrow sio kwamba alikula au hakula,Muhongo anawajibishwa na bunge kwakua Pesa ilikwapuliwa kwenye ofisi yake.Mule ndani ya Escrow kuna pesa ya uma na yeye alisema hakuna pesa ya uma.Lakini pia muhongo ali-accelerate mazungumzo ili wamiliki wazichukue,lazima alikuawa na maslahi,pia akili ya kusema sio pesa ya uma ni kosa kubwa.
5.Logic ya Escrow kuwa pesa ya Uma haifutiki:Mahakama ya kimataifa ilisema kuwa Ile pesa ifanyiwe Re-calculation kwa kutumia principle ya mtaji kianzio wa IPTL ambao ni elfu 50 na isitumike gharama ya uwekezaji wote ambao kimsingi lazima IPTL watataja mabilioni ya pesa maana ile ni kampuni na inakopa wakati wowote ili kutanua biashara yao.Gharama ya uwekezaji wote ukitumika kama ndo principle TANESCO wataendelea kulipa pesa nyingi sana.pia kuna kodi ya uma maana capacity charge ni faida ktk biashara.
6.Kama muhongo hana kosa,kwanini Maswi amesimamishwa?kama Escrow hakuna pesa ya Uma mbona Tibaijuka kang'olewa uwaziri kwa kupewa pesa na ndugu/rafiki/jamaa yake?Tibaijuka anakosa gani?shule yake,akaunti ni zake.kwanini analazimishwa kuweka hela kwenye akaunti ya shule?mlimsaidia kuomba hizo pesa.
NAJUA HUTANIELEWA KWAKUA UNATUMIA ELIMU YAKO KUWAFURAHISHA WACHACHE NA KULIHUJUMU TAIFA KIAKILI NA KIELIMU.