Kama Mchakato wa Katiba mpya ungeanzishwa chini ya Uongozi wa Mh. Magufuli, tungelikuwa nayo leo

Lekachonka

Member
Dec 17, 2016
35
17
Ndugu wana bodi,
Kwa haya yanayotokea na kuonekana kwa macho yetu ya nyama. Bila kupepesa macho, mchakato ule wa Katiba chini ya dreva huyu mpya ungemalizika kwa muda mwafaka na kwa gharama nafuu.

Tumeshuhudia kwa muda mrefu, kamati zikiundwa na majibu yake hayaonekani, tumeshuhudia michakato inavyochelewesha haki katika Nchi hii. Lakini toka Mh. Rais wa awamu hii ya Tano ashike madaraka, mambo haya sasa yameanza kuwa ndoto. Kamati tunaona zinaundwa na ripoti zinasomwa, maamuzi yenye tija kwa Taifa hutolewa.

Heko Mh. Rais, usiishie hapa, mfumo ndo tatizo. Leo Prof. Mhongo katoka, lkn wengine tunaamini tatizo si Prof. Mhongo, tatizo ni mfumo na mikataba iwekwe wazi na iwe shirikishi kwa wadau wote. Ili uweze kutatua suala hili gumu la mfumo, suluhisho ni KATIBA Mpya...

Haikuwa ajenda yako na si kipaumbele chako lkn kwa jinsi mambo yalivyo...huna budi kulifufua suala hili.
 
Back
Top Bottom