Kama mbinguni wanaenda wenye ndoa,basi sitaenda

Kama mbinguni wanaenda wenye ndoa,basi sitaenda

ah ah ah ah ah! hongera bana kwa huo mzigo ingawa na baridi hii inabidi obama azibidiwe maana hali yako hiyo!

unatafutwa kung'olewa kucha na meno kwa prize weweee, haya usije sema sikukwambia.
 
Pole mwaya.. Wanaume wengine ni tatizo, lakini kama umeamua wewe nenda ila umejaribu kuongea na wazee kwanza? Viongozi wa Kanisa lako je? Pia watoto utawamudu peke yako? Mungu awe kiongozi wako popote..
 
Una bihashara yeyote au unakitu kinachoweza kuwamudu hao watoto? Maana usije kuwafanya wa ishi maisha magumu na kumbuka baba yao
 
Sakapal, sijui kama umemuelewa mleta mada
Just do this, before you
pack your bags and leave for good from your marriage with your kids, he
is still your husband, ask him for a one month leave that should tally
with the work leave only if you are working. Hapo waweza kwenda hoteli
yoyote kutokana na uwezo wako na kama inawezekana muombe na yeye
akufinance huko enjoy with your kids na usiwe na mawasiliano na mtu
yeyote yule yaani uwe wewe tuu na watoto. Kama ni mama wa nyumbani au
mjasiriamali au umejiri na biashara zako unaweza kaa zaidi ya miezi 2,
ukiwa huko kwenye hiyo likizo waza mara mbili je unaweza kaa bila mumeo
au utaanza kummiss na kuona bora awepo hata kama ni mzigo.
Usifikiri watu wengine wanaenda kwenye harusi pamoja wamevaa wamependeza
ujue wanalea watoto na mapenzi yalishaisha siku nyingi. Wakiingia
chumbani kwao wanalala mzungu wa nne au kila mtu analala kitanda chake
na wengine vyumba tofauti kabisa ila hawaachani.
Think twice before you leave your marriage. Namuomba
BAK aje akuwekee kibao cha celine dion cha think
twice may be kitakubadili mawazo yako.
All the best mamy.
 
Last edited by a moderator:
mtoa mada hiyo avatar yako unaiish kweli ama unaihubiria tu??

manake kama unaniish huo msalaba wa YESU KRISTO, ni dawa ndio mana umewekwa kwenye bomba la sindano ili kukuponya na kuponya ndoa yako.
Yaaan umemaliza kila kitu!sa hv akili mu kichwa yake!aiweke ndoa yake mikononi mwa bwana
 
Just do this, before you pack your bags and leave for good from your marriage with your kids, he is still your husband, ask him for a one month leave that should tally with the work leave only if you are working. Hapo waweza kwenda hoteli yoyote kutokana na uwezo wako na kama inawezekana muombe na yeye akufinance huko enjoy with your kids na usiwe na mawasiliano na mtu yeyote yule yaani uwe wewe tuu na watoto. Kama ni mama wa nyumbani au mjasiriamali au umejiri na biashara zako unaweza kaa zaidi ya miezi 2, ukiwa huko kwenye hiyo likizo waza mara mbili je unaweza kaa bila mumeo au utaanza kummiss na kuona bora awepo hata kama ni mzigo.
Usifikiri watu wengine wanaenda kwenye harusi pamoja wamevaa wamependeza ujue wanalea watoto na mapenzi yalishaisha siku nyingi. Wakiingia chumbani kwao wanalala mzungu wa nne au kila mtu analala kitanda chake na wengine vyumba tofauti kabisa ila hawaachani.
Think twice before you leave your marriage. Namuomba BAK aje akuwekee kibao cha celine dion cha think twice may be kitakubadili mawazo yako.
All the best mamy.

sahihi kabisa ila wasiwasi wangu anaweza rudi baada ya kujipa likizo ndo anakuta mji tayari una mwingine:help:
 
Mwenzenu nimeamua kuondoka kwangu,mume huyu wangu alinioa kihalali kanisani,leo nimenyoosha mikono najiandaa kuanza maisha peke yangu na wanangu,nimeshindwa,siko tayari kufa kwa ukimwi kwa kuwa sistahili,alinioa bikira na simjui mwanaume yeyote zaidi yake katika dunia hii.
Uzinzi,umalaya,matusi anayonipa,dharau,kejeli na kutokunijali vinanifanya niondoke kwangu,kuanzia leo nimedhamiria kuondoka rasmi,hata nikisikia umeoa chelenje sitakwenda kulalamika popote,kwa sababu najua utakuwa umemuoa mwanamke unayempenda,nimelia sana sasa nimeamua kufuta machozi na kusonga mbele,najua MUNGU HATANIACHA!:wave:

hivi kuna wasichana bado mnaolewa na bikira siku hizi. Masikini, ndio maana unanyanyasika! Hao watu hawana maana yoyote. Hata kama bikira unayo ingiza kidole mpaka itoke. Hiyo heshima hawastahili kabisa. Ndoa zenyewe zote ni Ndoano bikira ya nn?
 
Yaaan umemaliza kila kitu!sa hv akili mu kichwa yake!aiweke ndoa yake mikononi mwa bwana
Jamani hebu muoneeni huruma mwenzenu hata neno la Mungu lakataza zinaa sasa kama huyo mbaba anamtafutia ukimwi kwa lazima si bora asepe tu.
 
Kwa hayo uliyoeleza mtoa mada bora usepe tu na vile umeona mwenyewe umuhimu wa kufanya hivyo kwa kweli pokea pongezi toka ndani ya mtima wa moyo wangu. Unajua wengi wameaga dunia kwa mtindo wa kuvumilia wanaume wengine hawana staha wala heshima hata kidogo juu ya wake zao , na pia hawaoni umuhimu wa kuendelea kula ugali . Kuna maisha ya wanandoa wengine ni majanga kwa kweli sasa bora uokoe wanao na naamini Mungu hatokuacha yupo pamoja nawe.
 
hivi kuna wasichana bado mnaolewa na bikira siku hizi. Masikini, ndio maana unanyanyasika! Hao watu hawana maana yoyote. Hata kama bikira unayo ingiza kidole mpaka itoke. Hiyo heshima hawastahili kabisa. Ndoa zenyewe zote ni Ndoano bikira ya nn?
Hahahahahahaha umenichekesha sana lkn hapo nilipopigia mstari napenda nikutie moyo kua sio ndoa zote ndoano zipo ambazo zina raha mpaka unajiuliza kwanini hamkuoana mkiwa 18. Ni kweli zipo ndoa chungu lkn hii haihalalishi ndoa zote kua chungu , hapana. Zipo ndoa ukibahatika kuziona utatamani kuolewa/ kuoa kesho.
 
Mwenzenu nimeamua kuondoka kwangu,mume huyu wangu alinioa kihalali kanisani,leo nimenyoosha mikono najiandaa kuanza maisha peke yangu na wanangu,nimeshindwa,siko tayari kufa kwa ukimwi kwa kuwa sistahili,alinioa bikira na simjui mwanaume yeyote zaidi yake katika dunia hii.
Uzinzi,umalaya,matusi anayonipa,dharau,kejeli na kutokunijali vinanifanya niondoke kwangu,kuanzia leo nimedhamiria kuondoka rasmi,hata nikisikia umeoa chelenje sitakwenda kulalamika popote,kwa sababu najua utakuwa umemuoa mwanamke unayempenda,nimelia sana sasa nimeamua kufuta machozi na kusonga mbele,najua MUNGU HATANIACHA!:wave:
Hata sijui nianzie wapi, lakini naamini yawezekana umeshayatafakaria haya nitakayokueleza

1. Kwa kuwa ndoa ni agano baina ya watu wawili na mungu basi in the very beginning lazima kumshirikisha sana mungu katika hili, mara nyingi watu wamekuwa wakiforce kuoa au kuolewa na wanaume/wanawake wasio wake/waume zao. mungu ana njia nyingi za kukuonyesha kuwa huyo ni mkeo/mumeo. Kumbuka pia kuwa mungu hawezi kushuka na kukuambia, mara nyingi anatumia binadamu kwa hiyo si vema sana kupuuza maneno yote unayoshauriwa na binadamu. Dada reflect kwanza ilikuwaje kwenye ndoa yako na huyo bwana?? unadhani mungu alijaribu kukuambia si mumeo ukaendelea??? Hili ni la msingi sana kwa kuanzia.....

2. Kama namba moja ni No, shetani ni mjanja sana, tena mnoooo. kaa chini jiulize tena na tena, jitolee kupigana kwa ajili ya mumeo maana yeye mungu ndio alikupa. Si yeye mumeo bali kuna roho inayomtumikisha, na kama unavyojua wanawake ni jukumu letu kubwa kuombea familia zetu hasa waume zetu ambao shetani anawatafuta 24/7, kazi unayo na ukiifanya vyema mungu wetu atadhihirisha ukuu wake juu ya mume wako na mtaishi kwa furaha na amani tena

3. Kama Namba moja ni yes kabla ya kuondoka muombe mungu akufunulie zaidi na akuhakikishie kuwa maamuzi unayochukua ni sahihi.... amini nakuambia mungu wetu ni muaminifu mno, kitatokea tu kitu na hautajiuliza tena mara mbili.

4. Muombe mungu akuongoze huko unakoenda, maana amesema yeye hatotuacha kamwe basi mlilie na hakika kama wewe ni muaminifu kwake utaona baraka zitakavyotiririka juu ya maisha yako.

Nakutakia yote yaliyomema maana safari unayoianza ni ngumu mno, ila kwa uwezo wake yeye utashinda tu.
 
Vizuri, endelea hivyo hivyo na msimamo wako. Ikiwa hutojali tafuta mwingine uishi nae, maisha ya kuwa single yanahitaji moyo mgumu kama bati la South Africa.

Kweli umesema kama ni kaka au dada umesema ukweli mtupu.
Hakuna maisha magumu kama ya kuishi peke yako. kwa sasa dada anaona ni shida kuendelea kuishi na huyu bwana asiyetulia lakini atajikuta ana wakati mgumu wa upweke.
Je umeji check afya yako?
Maana unawea sema unaogopa UKIMWI lakini ukaenda tena mahali ambapo upo kwa mwingine
Piam afya yako na tulia hata mwaka hivi kisha omba sana Mungu akupatie mtu mtulivu asiye na VVU
NIna kisa kikubwa sana na unaweza nitumia private sms nikuelezee upande wangu
Mtegemee Mungu na omba sana bila kuchoka
asante, mama mwenzio aliyeshindwa kama wewe akaondoka
 
Ha ha haa hapo kuna utata kidogo.

Mkuu yaani weee acha tu....utakuta binti alianza kufumuliwa tangu high school, akiwa chuo kafumuliwa mpaka na ma-lecturer. Akiolewa na mwanaume ambaye hajawahi kulala naye akiwa shule wala chuo, siku akikorofishana na mumewe anapolia anadai 'huyu mwanaume nilimthamini sana maana ndiye alinitoa bikira yangu' ......
 
Mwenzenu nimeamua kuondoka kwangu,mume huyu wangu alinioa kihalali kanisani,leo nimenyoosha mikono najiandaa kuanza maisha peke yangu na wanangu,nimeshindwa,siko tayari kufa kwa ukimwi kwa kuwa sistahili,alinioa bikira na simjui mwanaume yeyote zaidi yake katika dunia hii.
Uzinzi,umalaya,matusi anayonipa,dharau,kejeli na kutokunijali vinanifanya niondoke kwangu,kuanzia leo nimedhamiria kuondoka rasmi,hata nikisikia umeoa chelenje sitakwenda kulalamika popote,kwa sababu najua utakuwa umemuoa mwanamke unayempenda,nimelia sana sasa nimeamua kufuta machozi na kusonga mbele,najua MUNGU HATANIACHA!:wave:

Pole sana na Mungu akusaidie kwenye maamuzi yako. Ni busara kuishi pekee yako, kuliko kuishi na mtu ambaye anaweza kukusababishia mauti au anayekupa maudhi, karaha, kejeli, dharau na gadhabu kila siku. Ndoa siyo kwa ajili ya hayo matatizo, ndoa ni heshima na kusaidia, kupenda, juheshimiana, kujaliana, kujenga na kutunza familia, furaha, amani na mengineyo mengi yanayofanana na hayo.
All the best!
 
chelenji umemkuta mtoto wa watu bikra kwanini unamnyanyasa? kwanini usimfundishe mapenzi taratibu kwa upendo? kwanini humthamini naye akajiona yupo Heaven on earth ? kwanini humtunzi inavyostahili? kwanini haki yake ya ndoa huitunzi na kuiheshimu?

hivi cheleji hao magumegume wa mtaani unaohangaika nao wanakupa nini ambacho mkeo hana?

chelenji usimwache giningi aondoke mpe tulizo la moyo na faraja la nafsi mkeo , kama ni uvumilivu mkeo kakuvumilia sana.
 
Last edited by a moderator:
Kuwa makini sana kwsbbu watu wengi hushauri kitu ambacho wao wenyewe hawawezi kutekeleza kama wangekuwa ktk nafasi yako. Just listen to ur heart, Friend.
 
Back
Top Bottom