Kama mbinguni wanaenda wenye ndoa,basi sitaenda

Kama mbinguni wanaenda wenye ndoa,basi sitaenda

Mwenzenu nimeamua kuondoka kwangu,mume huyu wangu alinioa kihalali kanisani,leo nimenyoosha mikono najiandaa kuanza maisha peke yangu na wanangu,nimeshindwa,siko tayari kufa kwa ukimwi kwa kuwa sistahili,alinioa bikira na simjui mwanaume yeyote zaidi yake katika dunia hii.
Uzinzi,umalaya,matusi anayonipa,dharau,kejeli na kutokunijali vinanifanya niondoke kwangu,kuanzia leo nimedhamiria kuondoka rasmi,hata nikisikia umeoa chelenje sitakwenda kulalamika popote,kwa sababu najua utakuwa umemuoa mwanamke unayempenda,nimelia sana sasa nimeamua kufuta machozi na kusonga mbele,najua MUNGU HATANIACHA!:wave:
Hapo penye nyekundu ndio ulipokosea ndio maana una maumivu sana, otherwise ndoa yako inaweza kuendelea vizuri tu
 
Dada yangu kimbia na usigeuke nyuka ukageuka mti wa chumvi kama RUTU!
 
Hapo juu ni nyuma na si nyuka wasahihishaji mniwie radhi si unajua mkono hauna ulimi!..ok mr bak wimbo basi wa celine dione kumliwaza mamy!
 
Mwenzenu nimeamua kuondoka kwangu,mume huyu wangu alinioa kihalali kanisani,leo nimenyoosha mikono najiandaa kuanza maisha peke yangu na wanangu,nimeshindwa,siko tayari kufa kwa ukimwi kwa kuwa sistahili,alinioa bikira na simjui mwanaume yeyote zaidi yake katika dunia hii.
Uzinzi,umalaya,matusi anayonipa,dharau,kejeli na kutokunijali vinanifanya niondoke kwangu,kuanzia leo nimedhamiria kuondoka rasmi,hata nikisikia umeoa chelenje sitakwenda kulalamika popote,kwa sababu najua utakuwa umemuoa mwanamke unayempenda,nimelia sana sasa nimeamua kufuta machozi na kusonga mbele,najua MUNGU HATANIACHA!:wave:

good for you. you a woman and ahalf!
 
Na kesho akija hapa akawaambi amefuata ushauri wenu ....ameamua kukaa na mume wake sema ndo hivyo ameshamletea ukimwi .........mtamwambieaje.......wengine mtamgeuka hapa mtaanza ohhh we nawe ulikuwa mjinga ushaona mume kicheche bado upo tu? So wakati mnamshauri arudi mjue kuna hatari zake pia...atampa ukimwi na wataacha watoto yatima bila malezi bora....bora ujiondokee madame...na mbinguni utaenda...tena seat yako iko back bencher bale jirani na siti yangu.

Huogopi kuitwa mvunja ndoa za watu?
 
bora umejitambua! achana nae hata yesu mwenyewe alisema uzinzi mtyu achape lapa... sasa huyo mwenye madharau na matusi na manyanyaso plus ukicheche?....maisha ni haya haya
 
Alikuwa kalewa ndio maana. Msamehe bure. Hilo la kuchana nje ahhh. Ajabu hata wewe utachana nje baada ya kuondoka kwake. Na huyo wa pili atakuwa na chain refu kama reli ya kati. Then atakuja na mwingine na mwingine maana huna kizuizi. Nao watakuita malaya maana ni ukweli. jifunze kuvumilia na kuongea na mwenzio.

Umeongea kila kitu.....Hajui kwamba huyo mwingine naye ana mtu anadhani kukaa pekee yake ni kitu chepesi wengine hizo karaha watu wanazipenda tu..na kama kuna mtu kakudanganya angalia atakuja kulia pekee yake..na kama ni ukimwi kwa anayoyafanya angekuwa ameshapata siku nyingi lakini kama una mtuhumu lakini hujapata ukimwi basi usimsimange mwenzio sema ulikuwa na la kwako sasa umelitimiza ila siyo kwamba ni ndoa..Wanawake bwana viumbe hatari
 
Siku zote kunguru hawezi kuwa njiwa lazima ipo siku atakumbuka tabia za kunguru na atazirudia tu...
 
Mwenzenu nimeamua kuondoka kwangu,mume huyu wangu alinioa kihalali kanisani,leo nimenyoosha mikono najiandaa kuanza maisha peke yangu na wanangu,nimeshindwa,siko tayari kufa kwa ukimwi kwa kuwa sistahili,alinioa bikira na simjui mwanaume yeyote zaidi yake katika dunia hii. Uzinzi,umalaya,matusi anayonipa,dharau,kejeli na kutokunijali vinanifanya niondoke kwangu,kuanzia leo nimedhamiria kuondoka rasmi,hata nikisikia umeoa chelenje sitakwenda kulalamika popote,kwa sababu najua utakuwa umemuoa mwanamke unayempenda,nimelia sana sasa nimeamua kufuta machozi na kusonga mbele,najua MUNGU HATANIACHA!:wave:
Try Jesus, your Avatar tells! Pili, kwa kuwa uliolewa kihalali kanisani (kama ulivyoandika), je ulipoulizwa lile swali liulizwalo katika kila misa takatifu ya ndoa "je utampenda na kumjali mume wako kwa shida na raha" ulilijibu NDIYO ama HAPANA? Naomba unijibi ili niweze kukushauri zaidi dada yangu! Otherwise, pole na matatizo!
 
hah aahah nimecheka sana bana siku hizi wadada hawaondoki tena ukiwa na watoto unanya kitu mbaya sana ile ilikuwa zamani siku hizi anamwambia mume kabisa kwa sababu wewe ndo umenichoka mimi humu ndani sitoki kama wewe umeona huyo mwezangu ni bora zaidi poa we endeleaaa ila mimi nikitoka tu humu ndani ujue kaburini hahaha sasa wewe unakimbilia kupack mbona utapaki sana
 
dah!hapa ndo huwa nachoka kabisa!
Wengine we a praying Mungu atupe waume,wengine wanajuta kuingia na wanataka kutoka!,..kazi ipo!
 
nahisi kama baadhi ya akinamama wana nidhamu ya woga sana....

kila maaumuzi ya faida na hasara zake, kipi bora uendelee kung'ang'ania ndoa ambayo thamani yako haipo tena na rafu nyingi za michangani which means .. uko ktk hatari kubwa ya maambukizo.. ili tu uiridhishe jamii kuwa uko kwa ndoa???

... hainingii akilini
 
nyumba si kitu,uhai wangu ndio wa maana sana na amani pia,niko radhi kuviacha my dia,hali ni mbaya kuliko mnavodhani,nilishafikiia kujitenga chumba but nikaona watoto wangeniuliza maswali ambao majibu ningekosa,acheni jamani

kaa naye mbali, akikutafuta manake wewe ni muhimu kwake, acipokutafuta manake alishakuchoka alikuwa anatafuta sababu ya kukufukuza. uhai ni kila kitu mali zinatafutwa.
 
Pole sana omba mungu atakupa msaada wa kumrejesha mumeo ndani ya mstari
 
Kunadhambi za kushindana nazo,dhambi nyingine ni za kuzikimbia!....watu tumekuwa wepesi wa kuona baadhi ya dhambi na nyingine hatuzioni kabisaaa!Leo hii itaonekana kuvunja ndoa ni dhambi kubwa saana kwahiyo uendelee kuugulia moyoni huku usoni unaonyesha tabasamu(wenyewe wanaita uvumilivu)ilihali katika hilo tabasamu lako fake unatoa kila laana moyoni mwako kuhusu huyo unayemvumilia,unamtusi(nafsini),unatamani mabaya yampate huku unajitabasamisha na kifake smile chako huoni kama unatenda dhambi kwa kuwa mnafiki? Uamuzi kamili unao katika kifua chako,maneno yetu yatakupooza tu kwa muda lakini mwisho wa siku,utaepata taabu au faraja kwa kuachana na mumeo ni wewe!Fanya maamuzi sahihi na uwe tayari kuyasimamia no matter what!ALL THE BEST!
 
nilijibu ndio
Try Jesus, your Avatar tells! Pili, kwa kuwa uliolewa kihalali kanisani (kama ulivyoandika), je ulipoulizwa lile swali liulizwalo katika kila misa takatifu ya ndoa "je utampenda na kumjali mume wako kwa shida na raha" ulilijibu NDIYO ama HAPANA? Naomba unijibi ili niweze kukushauri zaidi dada yangu! Otherwise, pole na matatizo!
 
mkuu natamani huyo mwingine ningemjua nimkabidhi mji kabisa,hilo kwangu si ishu kubwa ila nataka na yeye aje aonje joto la jiwe najua Mungu atakuja kumuadhibu vibaya, WHAT GOES AROUND COMES AROUND
sahihi kabisa ila wasiwasi wangu anaweza rudi baada ya kujipa likizo ndo anakuta mji tayari una mwingine:help:
 
Back
Top Bottom