hata richmond nina unaimani kuwa walimpakazia ..
Siku zote nimesema ndani ya Chadema kumejaa mapandikizi ya CCM (Lowassa). halafu watu wanapiga kelele humu JF kuwa wataing'oa CCM madarakani, wafuasi wa Chadema wameanza kukiri wote watarudi CCM na kumuacha Dr Slaa peke yake.
Mkuu hebu soma sababu yako ya tano, na ulinganishe maelezo yako hapo juu!
Katika sababu yako hiyo umesema kana kwamba una UHAKIKA...katika quoted post hapo juu imekuwa kinyume chake ..tukueleweje?
Nakubaliana na ww kwenye baadhi ya mambo hasa utendaji wake,nina shaka kwenye hoja ya kutokuwa fisadi. Nitangaze conflict of interest kuwa ni mpenzi na mshabiki wa CDM, but tukiacha mambo ya vyama umetangaza kumchagua uki ignore uwezo wa wagombea wengine kati ya machaguo tuliyo nayo kati ya wagombea, kutakuwa na tatizo kama atagombea kwa CCM kwa sababu mfumo ulisha haribika na unatakiwa kusukwa upya ili aweze kuwa na ujasiri na kuendelea kutokuwa muoga, alisimamia vizuri suala la shule za kata kama sijakosea, ni mtu anayeweza kuchukua maamuzi hasa magumu (ndio tatizo tulilonalo kwa sasa), kuna limitation ya baadhi ya maamuzi kulingana na mfumo hivyo kutoa picha ya Uoga, mfano si jambo jepesi kumchukulia hatua mtu aliyeua wakati amekusaidia kuua ili uwe kwenye nafasi uliyonayo.Nifupishe kwa kusema yafuatayo
1. Alikuwa mmoja wa wanamtandao waliochota fedha za wananchi ili kufanikisha ushindi wa CCM na uenda akatumia tena mbinu hizohizo na kuzidi kubobea kwenye ufisadi.
2. Atakuwa mgombea mzuri kama nchi haitakuwa na watu makini wa kugombea na hivyo taifa kukosa mbadala
3. Mtandao alioutengeneza uliojaa mafisadi ndani yake utamkwamisha na dhana ya kutokuwa muoga itatoweka kwa kuwa atalazimika kuwalinda.
4. Nguvu kubwa ya fedha inayotumika kumsafihsa na kujitengenezea mazingira/ network ya kushinda inaweza kulipeleka taifa pabaya.
utanielewa tu kama utataka kufanya hivyo.
Tumchoka na CCM kwa ujumla. Hakuna jipya Mkapa alukuwa mchapa kazi lakini ufisadi uliendelea. Hatutaki kuendeleza ufisadi TZ. waTZ msijute kama mtaendelea na CCM madarakani. Tuweke utaratibu wakubadilisha watawala ili wajue kuwa kama hawatekelezi matakwa ya wananchi wanatolewa na sula la "impunity" litakwisha na inch itakuwa na maendeleo. Zambia na Kenya mameweza kwanini TZ hatuamki ni usingizi huu tulio naio?
mimi sihitaji chapaa nataka kuona kila mtanzania akiwa na uso wa furaha kwenye hili taifa letu lenye utajiri wa kila aina'
mimi nampenda sana Dr Slaa pamoja na cdm yote ila huo ni mtazamo wangu unaweza kunibadilisha kwa hoja pia
kama anampenda anafanya nini cdm akanywe nae chai eboHoja ya kukubadilisha wewe ni bahasha iliyotuna,kutoka Bank na CDM hatuna vitu kama hivyo,labda ujaribu PPT.
Aliyekuwa waziri mkuu wa kwanza kwa utawala wa JK ndg Edward Lowasa 'EL' maarufu kama mzee wa 'RICHMOND' au mzee wa 'White hair' nadiriki kusema kuwa kama akipata nafasi ya kugombea taasisi ya Uraisi atakuwa na kura yangu moja kwa moja pamoja na uanachama wangu makini wa CHADEMA.
Hii ni kutokana na sababu zifuatazo;
1. Ni mchapakazi
2. Hana woga wa aina yoyote
3. Anajiamini kwa mambo anayoyasimamia
4. Anawapenda wananchi.
5. Siyo fisadi kama tunavyomtangaza.
6. Ni mpenda maendeleo kuliko kitu kingine.
7. Anasimamia maslahi ya taifa zaidi kuliko chama.
Hayo nimeyaona kwa EL' kuliko ninavyomwona Pinda.
Lowasa aliisimamia serekali kikamilifu sana ukimlinganisha na Pinda aliyejipambanua kama mtoto wa 'MKULIMA' kumbe ni mtoto wa mjini(mjanja tu), anajua anachokisema ila hawezi na wala hathubutu kukisimamia ila EL aliweza na nina imani ataweza.
Tutofautiane kwa hoja na siyo viroja na matusi yasiyojenga.
Nimeyasema haya nikiwa na imani kuwa Tanzania tunahitaji viongozi makini na siyo maswala ya vyama'.
Mungu ibariki Tz.
Duh jini la Lowasa ni kiboka sijui alilitoa wapi.maanake ili umupendekeze Lowasa kuwa rais wa tz unatakiwa uwe na akili za kijinijini tu.kutokana na ufirauni aliotufanyia wtz.kumpa urais lowasa ni sawa na kumkabidhi fisi bucha ili ailinde.
Je sifa hizo mgombea wa CHADEMA hana au unalinganisha majizi kwa majizi lipi nafuu? kama kweli wewe ni CDM kwa nini unamlinganisha na Pinda mtoto wa mkulima ambaye hana hisia za urais badala ya kumlinganisha Dr Slaa wa CHADEMA yako? kwa nini unaona aibu kujitangaza kuwa wewe ccm wa kundi la lowasa? Usione soo subiri utakumbana na kimbunga usichowahi kukiona maishani mwako na mgombea wako mgonjwa kila sikuAliyekuwa waziri mkuu wa kwanza kwa utawala wa JK ndg Edward Lowasa 'EL' maarufu kama mzee wa 'RICHMOND' au mzee wa 'White hair' nadiriki kusema kuwa kama akipata nafasi ya kugombea taasisi ya Uraisi atakuwa na kura yangu moja kwa moja pamoja na uanachama wangu makini wa CHADEMA.
Hii ni kutokana na sababu zifuatazo;
1. Ni mchapakazi
2. Hana woga wa aina yoyote
3. Anajiamini kwa mambo anayoyasimamia
4. Anawapenda wananchi.
5. Siyo fisadi kama tunavyomtangaza.
6. Ni mpenda maendeleo kuliko kitu kingine.
7. Anasimamia maslahi ya taifa zaidi kuliko chama.
Hayo nimeyaona kwa EL' kuliko ninavyomwona Pinda.
Lowasa aliisimamia serekali kikamilifu sana ukimlinganisha na Pinda aliyejipambanua kama mtoto wa 'MKULIMA' kumbe ni mtoto wa mjini(mjanja tu), anajua anachokisema ila hawezi na wala hathubutu kukisimamia ila EL aliweza na nina imani ataweza.
Tutofautiane kwa hoja na siyo viroja na matusi yasiyojenga.
Nimeyasema haya nikiwa na imani kuwa Tanzania tunahitaji viongozi makini na siyo maswala ya vyama'.
Mungu ibariki Tz.