Kama Lowassa alitabiriwa na TB Joshua kuwa Rais TZ, Iweje sasa atumie Pesa kukampenia Urais?

Utabiri wa TB Joshua unakuwaga kweli...ana personal prophecy na zinazohusu taifa...ila hatujui kama ni kweli alisema hivyo....kama kweli alisema kuna dalili zinaonekana
 
Hata mm nilikuwa against TB lakini hivi karibuni nimeanza kumfuatilia baada ya kutabiri muda mfupi baada ya ndege ya Malaysia kutoweka,alisema ndege imeangukia bahari ya hindi na ikawa vigumu kuamini kwani hiyo ndege ilikuwa inaelekea China ambako haipitii kabisa Indian Ocean
Hivi majuzi mabaki ya ndege hiyo yameokotwa pwani ya kisiwa cha Reunion ambacho kiko katika bahari ya Hindi.

Unaamini utabiri wake au unamkubali kama mtumishi wa Mungu?
 
Acheni kumsingizia mtumishi wa Mungu kwa mambo yenu ya kishabiki wa simba na yanga, TB J ajawai kutamka juuu ya urais wa lowasa, kama lowasa kwenda kwake kusali alishaenda ata Makufuli pia alishaenda lkn swala la uraisi wa hiii nchi anayejua ni Mungu tu.uzushi muachee.

Mtafute mbunge Beatrice shelukindo .walikuwa wote msafara wa kwenda kwa TB Joshua.tena yeye ndio aliweka hiyo habari wazi .Lowasa mwenyewe hakuwahi elezea wazi
 
TB Joshua hyo baba ni msema kweli.. na lowasa ndie anaenda kuwa rais wa tanzania, nasema na iwe ivyo
 
Taarifa kutoka kwa watanzania walio enda TB Joshua walifika wakasema mbona ulisema Lowasaa atakuwa rais alafu akakatwa?

Tb Joshua akawambia uchaguzi umesha fanyika wakasema apana akawambia nendeni nchini kwenu mkafanye uchaguzi lowasa ndo raisi, siku wanafika Tanzania wakakuta ndo siku Lowassa anajiunga na CHADEMA peplessssssssssssssssssss.

Hahaaaa safiii
 
Hapo sasa unataka kusema madaktari hawaugui wala kufa, wanasheria hawahukumiwi wala kufungwa, kama wewe ni mkristo basi hujawahi kusoma biblia au kuhudhuria mafundisho yoyote maana ungejua habari za mambo yaliyowakuta manabii wa Mungu. kwani ukiwa muumini mzuri hupati shida yoyote hapa duniani?

Mpe vidonge huyo lol@ Monyiaichi
 
Marehemu Shekhe Yahaya Hussein alitabiri 2008 kuwa Lowassa atarudi kwenye madaraka ya juu ya nchi. Walio msikia watakumbuka
 
Taarifa kutoka kwa watanzania walio enda TB Joshua walifika wakasema mbona ulisema Lowasaa atakuwa rais alafu akakatwa?

Tb Joshua akawambia uchaguzi umesha fanyika wakasema apana akawambia nendeni nchini kwenu mkafanye uchaguzi lowasa ndo raisi, siku wanafika Tanzania wakakuta ndo siku Lowassa anajiunga na CHADEMA peplessssssssssssssssssss.

asipokua rais sijui utasemaje asee....
 
Naona propaganda za msukuma wa bamaga zinafanya kazi maana mara ya mwisho mwaka jana GAZETI ZAKE ZA UDAKU ZILIANDIKA HILI.LAKINI KIUHALISIA TB JOSHUA AJAWAI MTABILIA URAIS HUYU JAMAA
 
Thread nyingine bhana, dah uvumilivu unahitajika...huyo jushua kama yeye ni nabii anashindwaje kutatua matatizo yaliopo huko nigeria hadi raisi Buhari anaenda kuomba msaada Marekani, kumbe nabii yupo inakuaje anashindwa kutatua? Acheni ujinga bhana

Mkuu huyo Joshua angekuwa mkali jengo lake lisinge poromoka na kuua waumini lukuki!! Kwa nini hakuweza kutabiri in advance what was coming kwenye nyumba yake ya ibada?

kwahiyo mnataka kusema kile kipindi cha manabii wazito ktk agano la kale kwenye Bible mf akina Elia maisha yalikuwa tambarare?? hawakuwahi kupatwa na mabaya? au nchi zao kupatwa na mabaya!? mkae mkijua ili mradi mtu unaishi duniani hata uwe nani na unatumiwa na Mungu kwa kiwango gani...majaribu lazma yaje! na Mungu huyaruhusu kwa sababu zake, wakati mwngn huyaruhusu kwa Muda ili baadae atakapoleta majibu ajitwalie utukufu. Kumbukeni issue ya Ayoub!! wakristo kwa waislam wote tunajua yaliyompata Ayoub japo alikuwa mtumishi mwaminifu na mkamilifu wa Mungu
 
Sitaki kuamini kuwa hii taarifa ni sahihi KWANI nijuavyo mimi T.B Joshua yupo katika mapumziko na maombi kule Mexico tangia mwezi wa sita mwaka huu (naweza kukosolewa).

Back
Top Bottom