Edward Lowassa adai kuwa TB Joshua amemtabiria ushindi katika uchaguzi Mkuu 2020

PRODA LTD

JF-Expert Member
Oct 20, 2016
1,005
1,333
Screen Shot 2020-06-04 at 18.14.36.png

Waziri Mkuu wa zamani na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa amedai kuwa mhubiri maarufu wa Nigeria, TB Joshua amemtabiria ushindi katika uchaguzi mkuu ujao (2020).

Akizungumza jana katika kikao cha ndani Mkoani Tabora, Lowassa alisema kuwa mhubiri huyo ambaye alikuja nchini siku chache baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu alikihakikishia chama hicho maono ya ushindi katika uchaguzi ujao.

“Najua waandishi wa habari wataandika, lakini sijali, rafiki yangu TB Joshua ametabiri Serikali ijayo itangozwa na Chadema,” Lowassa anakaririwa na Mwananchi.

Hata hivyo, Lowassa aliwaeleza viongozi hao kuwa mhubiri huyo alitoa masharti kuwa ili utabiri huo uweze kutimia ni lazima washikamane na wadumishe umoja ndani ya chama hicho.

Kabla ya kujiunga na Chadema, Lowassa ni mmoja kati ya wanasiasa walioenda nchini Nigeria na kuombea na TB Joshua. Rais John Magufuli pia pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba walifika katika kanisa la Synagogue Church of All Nations (SCOAN) na kuombea na mhubiri huyo kabla ya kuingia kwenye kinyang’anyiro cha urais.
 
Kwani Mwaka Jana hakushinda Urais?

Yeye aachane na hayo mambo ya Utabiri, Cha kufanya, watafute namna au mbinu ya kuulinda na kuutetea ushindi wao mwaka 2020.

Watafute namna ya kuhakikisha kura zilizotoka majimboni ndizo hizo hizo ambazo zinatangazwa na TUME YA UCHAGUZI.

Wawa-train watu wao mapema watakaosimamia uchaguzi, na katika majumuisho ya kura katika kata, na halmashauri.
 
Utabiri subject to certain conditions.

Watashikamana? Atapitishwa yeye kugombea na kama atakuwa mwingine, atamuunga mkono?

Au huo ushindi katabiriwa yeye akiwa mgombea?

Kwa utabiri wa TB Joshua, Hilary Clinton angekuwa Rais Mteule wakati huu.
 
Hizi staili za kutaka kuwahadaa wanachadema wampe tena nafasi ujinga huu.
Teh teh uyu mzee alitabiliwa hata2015 tena na watabili na maaskofu kibao Bora akachunge tu siasa apumzike.

Afu Tb Joshua alimtabiria hata Hillary, na Uefa vivyo hivyo lakini chalii uyu mzee utabili wake siku hizi hauna mashiko sana.
Sasa muache Edo aendelee kuiota magogoni.
 
Kwanza MAGOGONI yenyewe inahamishwa, sijui atelekea wapi huyu mzee.
 
Hajaumbwa kuhukumu au kulaani why Mnaingilia kaz ya Mungu, sishangai watu kama nyie hata kipind cha Yesu walikuwepo, ambao walikuwa wanadhihaki kaz ya Mungu, ivi wewe ni nan umsamae vibaya Mtumish wa Mungu? Ee Mungu baba Neno lako ambalo umenena na Nabii wako T.b. Joshua likapate kutia, Juu ya Mtu wako Mwaminifu Edward Ngoyai Lowasa awe Rais wa Tanzania 2020, kwa Jina La Yesu bwana wetu... Na wote tuseme aminaa
 
Hizi staili za kutaka kuwahadaa wanachadema wampe tena nafasi ujinga huu.
Teh teh uyu mzee alitabiliwa hata2015 tena na watabili na maaskofu kibao Bora akachunge tu siasa apumzike.

Afu Tb Joshua alimtabiria hata Hillary, na Uefa vivyo hivyo lakini chalii uyu mzee utabili wake siku hizi hauna mashiko sana.
Sasa muache Edo aendelee kuiota magogoni.
Wote tungekuwa tuna comment kama wewe.jamii forums ingependwa na viongozi wote wa serikali.
 
Back
Top Bottom