Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,581
- 46,178
TB Joshua ni mtu aliyejitengenezea jina kubwa barani Africa kwa injili yake ya mafanikio. Aliwakamata wafanyakazi, maskini, matajiri, wafanyabiashara na wanasiasa wakubwa kabisa katika ngazi za Urais na wakuu wa upinzani.
Watu hawakulizungumza tu jina lake bali walisafiri hadi Nigeria katika kanisa lake alilolipa jina la Sinagogi kanisa la watu wote(SCOAN). Inasemekana kuna wakati watu 6 kati ya 10 ambao ungewakuta wakisafiri kuingia Nigeria walikuwa wanaenda kanisani kwake!
Watu mashuhuri walimwalika kwao pia. Mfano hapa Tanzania amewahi kufika na kukutana na JK, Magufuli, Mbowe na Lowassa.
Mpaka sasa nikiacha hii sababu ya hulka ya watu kupenda kuambiwa, kuhadiwa na kutabariwa mafanikio makubwa kwa yale wanayoyatamani sijui kwa uhakika hasa ni kitu gani kingine kilimfanya TB Joshua ambaye aliendesha huduma yake kwa mfumo wa Mwamposa na Mzee wa Upako kuwa maarufu mkubwa hivyo kiasi cha kuliteka bara zima na kuweza kuaminiwa hata na pande zilizokuwa mahasimu mara nyingine.
Huenda waliomuamini na kumhusudu wana sababu nyingine za msingi walizoshawishika nazo lakini sasa akiwa hayupo tena duniani ni nani watampa nafasi hiyo? Wale mlioko Mikocheni B kanisani kwa Getrude Rwakatare tuelezeni mambo yanavyoendelea kwa sasa tupate mwangaza.