Kama kweli kitambulisho cha NIDA kina umuhimu basi serikali itangaze kuwa ambao hawana wasiruhusiwe kupiga kura katika uchaguzi mkuu mwakani

live on

JF-Expert Member
Dec 30, 2018
790
1,264
Naona kitambulisho cha Taifa kimeshika hatamu kila sehemu kinahitajika

KUPATA AJIRA
KUPATA PASS YA KUSAFIRIA
KUFUNGUA KAMPUNI
USAJILI WA LAINI ZA SIMU

Lakini cha ajabu katika kupiga kura ya kuchagua Raisi, wabunge na madiwani huwa hakihitajiki
Mi nafikiri kuchagua raisi, wabunge na madiwani ni kitu muhimu sana kwa sababu unachagua serikali itakayo kaa madarakani miaka 5 hivyo wapiga kura ilitakiwa ni lazima wawe na kitambulisho cha Taifa

Lakini kwa kuwa hili la kupiga kura linagusa matumbo yao hapo kitambulisho cha Taifa sio lazima

Sheria za nchi hii zinachekesha sana
Screenshot_20190414-124133.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivyo vitambulisho wanatoa wapi? Ina maana Driving Licence na Passport hazina maana?
 
...
Kuna kauzo somewhere ...
Kitambulisho cha taifa kinapaswa kuwa ndo muhimiri wa vitambulisho vyote ...
Huna haja ya kuwa na msululu wa vitambulisho katika hii enzi ya digital ...
Matumizi ya biometrics yanatosha kufanya utambuzi wa vikolombwezo vyote hivi ...
Haya ya vitambulisho vya kuzurura ... vya uzee ... vya kula ... vya simu ..... vyote ni kitambulisho kimoja ... VIDOLE VYAKO !
...
 
Back
Top Bottom