Kama kuna mzazi anasomesha mtoto wake wa kike Dodoma Media College (DMC) basi ajiandae kisaikolojia

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
10,206
12,747
Hii ni serious

Wahusika chukueni hatua haraka sana kabla Hali haijawa mbaya.

Kama mtoto wako wa kike yupo hostel nakuomba mzazi/ mlezi tembelea hizo hostel ujionee Hali halisi na namna mtoto wako anapoishi.

Najua mnaambiwa mlipe pesa ya hostel na wazazi mnalipa lakini mazingira hamjayaona.

Mazingira yapo hivi.

1) Watoto wa kike wanaishi nyumba moja na watoto wa kiume yaani imechukuliwa nyumba kubwa yenye uzio/fence na Kisha kuchanganywa watoto wa kike na wakiume.

2) Hii hostel haina ulinzi wowote hii ni hatari sana wahuni watakapo vamia hakika usalama wao mdogo sana.

Wakaguzi mnaokagua hostels za vyuo hii hostel ipo mkoa wa Dodoma kata kizota mtaa wa FM.

Naomba ichukuliwe hatua ya haraka sana maana watoto wa certificate hawana walijualo wengi wao wametoka mikoani na wao wanashangaa sana kukuta mazingira ya hostel wanachanganywa na wavulana.

Kwa kua tayali walishalipa pesa/fedha imekua Ni ngumu kwao kujinasua katika mtego huo.

Kama wahusika msipofuatilia hili tutegemee kuvunjika kwa ndoto za watoto wanaosomeshwa na wakulima kwa kutiwa MIMBA nk.
 
Broo za Udom siyo Kama hiki kituko ninachokiongelea.

Yaani hii ni nyumba moja yenye uzio chuo kimpenga kwa hiyo wamechukua wanafunzi wa kike na wakiume wakawaweka humo humo.

Utaratibu wa hostel unataka hivyo??
Wabadilike kuendana na biashara ya kisasa ya elimu
 
Acha kuharibu biashara za watu
Mtu akifika chuo ni mtu mzima
Akifanya ngono ni maamzi yake

Sent using Jamii Forums mobile app
Ila mtoa mada amejaribu kusisitiza wenye watoto wao pale hasa wakike .... swali wew una mtoto pale? ..... na kwanini uingize swala la biashara ilihali tuna hatarisha usalama wa watot wengine kwanza ulisha wahi ona wapi bweni inakuwa na jinsia mbili tofauti tena ngazi ya certificate.... kama huna la kuchangia tulia utunze status yako
 
MIMI NINACHOKIZUNGUMZA HAPA NIMEKIONA.

HATA WAO WANAFUNZI WANASHANGAA WANASEMA KAMA "WAZAZI WANGEONA HIKI WASINGEKUBALI"

HUYO JAMAA ANALETA USHABIKI MAANDAZI.
 
Kuna kitu hua kinaniijia akilini kua linapokuja swala la Elimu ngazi ya Chuo serikali iko vizuri sana kuliko private institutions. Hua napata amani naposikia mtu/ ndugu/ jamaa/ rafiki/ mtoto yuko chuo cha serikali specifically chuo kikuu kuliko vyuo vya private. Kwakifupi vyuo vingi vya private havijajipanga kabsa kuhudumia jamii kitaaluma zaidi wamefocus kwenye kufanya tu biashara.

Kwa mtizamo wangu huku juu ngazi ya Chuo serikali ingeachiwa tu yenyewe angalau ijenge chuo kila mkoa kwa ngazi ya certificate na diploma halafu na chuo kikuu kimoja kwa Elimu ya juu kwa kila mkoa ingesaidia sana kuondoa huu ukakasi
 
Kuna kitu hua kinaniijia akilini kua linapokuja swala la Elimu ngazi ya Chuo serikali iko vizuri sana kuliko private institutions. Hua napata amani naposikia mtu/ ndugu/ jamaa/ rafiki/ mtoto yuko chuo cha serikali specifically chuo kikuu kuliko vyuo vya private. Kwakifupi vyuo vingi vya private havijajipanga kabsa kuhudumia jamii kitaaluma zaidi wamefocus kwenye kufanya tu biashara
UPO SAHIHI MKUU KWA HICHO UNACHOZUNGUMZA
 
Kuna kitu hua kinaniijia akilini kua linapokuja swala la Elimu ngazi ya Chuo serikali iko vizuri sana kuliko private institutions. Hua napata amani naposikia mtu/ ndugu/ jamaa/ rafiki/ mtoto yuko chuo cha serikali specifically chuo kikuu kuliko vyuo vya private. Kwakifupi vyuo vingi vya private havijajipanga kabsa kuhudumia jamii kitaaluma zaidi wamefocus kwenye kufanya tu biashara
HIVI HAKUNA WAKAGUZI WANAOKAGUA HUU MFUMO AISE.

MIMI IMENISHITUA SANA HII

MZAZI YUPO BUSH ANAFAIT KUMBE MTOTO WAKE KAPEWA BWANA AISHI NAE NYUMBA MOJA.

HATARI SANA.
 
Back
Top Bottom