Kama kipimo cha ushindi ni idadi ya watu, Lowassa ndiye rais wetu

Tegemeo pekee la ccm ni watu hopeless kama Dr Mahera wa Nec.

Otherwise ccm ijiandae kukabidhi madaraka kwa Tundu Lisu hali halisi huku site siyo nzuri

Hata mimi nilikuwa naamini Magufuli anashinda bila tabu uchaguzi huu, but/lakini hii momentum of Tundu Lisu amegeuza upepo na unavuma upande wake na analitawala jukwaa na wananchi wanamwelewa.
Mkuu Matola , kiukweli, napenda sana watu wanao argue objectively kwa facts kama wewe kuwa hali halisisite sio nzuri!, kwasababu hii momentum of Tundu Lisu amegeuza upepo na unavuma upande wake na analitawala jukwaa na wananchi wanamwelewa.

Sijui ni members wangapi humu jf wamewahi kushiriki uchaguzi wakiwa front, huo upepo usikuzuzue ukidhani ni ushindi, hayo makundi ya watu kwenye mikutano ya mijini, sio kura, kura halisi za ushindi ziko vijijini ambako mgombea wenu ameshindwa kufika.

Kitu ambacho nakikubali kuhusu TL ni mzuri kuongea na analimiliki jukwaa, tena kwa msiojua, mimi ni miongoni mwa tulioshauri
Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli!

Ushindi wa uchaguzi sio wingi wa watu kwenye mikutano ya kampeni ya mijini!.
Subiria hiyo tarehe 28, utashangaa na hutaamini kitachotokea, sasa ili kuzuia kelele za kuibiwa kura,
nimeshauri
Uchaguzi 2020 - Ili kuondoa kelele za kutotendewa haki, nawashauri CHADEMA na ACT wekeni Mawakala kila Kituo ili kujiridhisha, Uchaguzi Mkuu ni huru na wa haki

Kama ushindi ni makundi ya watu, saa hizi EL ndie angekuwa ikulu!.
Kama kipimo cha ushindi ni idadi ya watu, Lowassa ndiye rais wetu

Elections 2015 - Hii 'Vox Populi' ni 'Vox Dei' Kuhusu 'Jiwe Walilolikataa Waashi'?

P
 
3X6A6344.jpg
Wanabodi,

Nimepita hapa Jangwani kwenye uzinduzi wa kampeni za UKAWA, mchana huu saa 8:45, kitu nilichokishuhudia, kama kipimo uha ushindi wa uchaguzi, ni Idadi ya watu waliojitokeza kwa ridhaa zao, bila kuhongwa Tshirt na kofia, nauli na shibe ya siku moja, na ikatokea umati wote huu ni umati wa wapiga kura wa kweli, na siku ya uchaguzi watajitokeza kwa wingi hivihivi na watampigia kura mgombea wa UKAWA, then, Edward Ngoyayi Lowassa, ndiye rais wetu ajaye!. Kwa upande huu wa idadi ya watu wa leo, nikilinganisha na idadi ya watu siku ya ufunguzi wa Mkutano wa CCM, then, CCM imezidiwa na Chadema, hivyo CCM itashindwa, Chadema itashinda!.

Hii inamaanisha, kama determinant ya ushindi ni idadi ya watu na umati unaojitokeza kwenye mikutano ya kampeni, na wote wamejiandikisha, na wote watajitokeza kupiga kura hiyo siku ya uchaguzi, mshindi wa uchaguzi huu atakuwa ni mwenye idadi kubwa ya watu.

Lakini ukweli, halisi ya matokeo ya kura sio huu unaoonekana machoni kwa makundi ya watu, hawa watu wenye boda boda, bajaj na umati uliojitokeza sometimes huwa wamehongwa pesa ili kuleta tuu ujazo wa wingi wa watu lakini hawajajiandikisha kupiga kura na sii wapiga kura, then hakuna ubishi, mshindi ataendelea kuwa ni CCM!.

Pasco wa jf, japo ni mwanachama wa chama cha siasa, lakini uchambuzi wake ni objective, na impartial, ni mkereketwa wa demokrasia ya kweli ndani ya Bunge, ambaye anaamini kwenye ukweli na uwazi!.

Pasco
Huyu nguli mwanasheria na mwandishi mwenye CV isiyo na shaka asiyeona zuri kwa Chadema! Ni, ni PMmmmmmm.
Hata hili sio zuri?.
P
 
Nimepita hapa Jangwani kwenye uzinduzi wa kampeni za UKAWA, mchana huu saa 8:45, kitu nilichokishuhudia, kama kipimo uha ushindi wa uchaguzi, ni Idadi ya watu waliojitokeza kwa ridhaa zao, bila kuhongwa Tshirt na kofia, nauli na shibe ya siku moja, na ikatokea umati wote huu ni umati wa wapiga kura wa kweli, na siku ya uchaguzi watajitokeza kwa wingi hivihivi na watampigia kura mgombea wa UKAWA, then, Edward Ngoyayi Lowassa, ndiye rais wetu ajaye!. Kwa upande huu wa idadi ya watu wa leo, nikilinganisha na idadi ya watu siku ya ufunguzi wa Mkutano wa CCM, then, CCM imezidiwa na Chadema, hivyo CCM itashindwa, Chadema itashinda!.

Hii inamaanisha, kama determinant ya ushindi ni idadi ya watu na umati unaojitokeza kwenye mikutano ya kampeni, na wote wamejiandikisha, na wote watajitokeza kupiga kura hiyo siku ya uchaguzi, mshindi wa uchaguzi huu atakuwa ni mwenye idadi kubwa ya watu.
Pasco[/SIZE]
Edward Lowassa alikuwa mtu wa watu na watu walijitokeza, jee katika safari yake ya mwisho, umati huu utajitokeza?.

Naendelea na My Tribute to this fallen hero, Mwamba wa Kaskazini, kwa kujikumbusha baadhi ya mabandiko yangu kumhusu shujaa huyu mpaka siku atakapo pumzishwa kwenye makao yake ya milele, let's celebrate the life and the times of Edward Lowassa.

RIP Shujaa Laigwanani Comred Edward Ngoyai Ole Lowassa,
Umepigana vita vilivyo vitakatifu, imani umeilinda.
Bwana alileta
Bwana ametwaa,
Jina Lake Lihimidiwe!.

Paskali
 
Mimi nitamkumbuka Kwa kuzuia Tanzania isiingie kwenye vita ya wenyewe Kwa wenyewe baada ya CCM kuiba uchaguzi.

Ni Lowasa ndio Alizuia watu wasiingie barabarani.
 
Back
Top Bottom