Kama Kiongozi hajiheshimu anastahili kuheshimiwa?

ubongokid

JF-Expert Member
Apr 30, 2017
2,031
3,911
Rais Samia,

Ukweli ni kwamba kama kiongozi hajiheshimu hastahili kuheshimiwa hata kama kiongozi huyo ni wewe.

Kila kiongozi kwa nafasi yake ni Taasisi. Kama anadharaulika basi hata taasisi anayoongoza itadharaulika. Hakuna namna nyingine yoyote.

Mh. Samia, wewe ni Rais wa nchi haijalishi umeingiaje madarakani unao wajibu kwa watanzania na ni lazima utimize wajibu huo.Kauli na matendo yako lazima viakisi nia na wajibu huu.

Jana katika mazungumzo yako na viongozi wako ulisema wazi kwamba Kuna migongano ya maslahi mawaziri wakigomea safari na kugombania maslahi. Hio ni aibu yako na serikali yako. Hiyo ina akisi kwamba aina ya viongozi ulionao ukiwamo wewe wamejikita katika kutumbua kodi za wananchi. Ulikiri wazi kwamba mawaziri wako wanakula pesa za miradi mpaka zinaathiri miradi ya kuwaletea maendeleo wananchi. Kukiri kwako kuna maanisha kwamba unajua na umeamua kuwacha hali hiyo iendelee.

Mh. Rais jana umesema kila mbuzi ale urefu wa kamba yake unajua maana ya msemo huo? Huku barabarani tafsiri yake ni kwamba sasa tutafuta namna ya kurefusha kamba zetu, tutafuta namna ya kula. Kuna ambao hawana pesa za safari wala hawana wakandarasi wanaotaka kuwapa 10% ili wapate vitalu vya kuwinda,na miradi ya barabara na Ujenzi wa shule za COVID. Mheshimiwa Rais urefu wa kamba unaozungumzia kama RAIS ni kuhalalisha UFISADI, RUSHWA na UNYONYAJI.

Suala langu kwako Mheshimiwa RAIS je Kamba yako ina urefu gani? Ni urefu wa kuweza KULA 10% za MIKOPO NA MISAADA KUTOKA IMF maana umetetea sana mikopo na Misaada au kamba yako urefu wako ni KUYAPA MAKAMPUNI YA KIARABU MAENEO WAWEKE MIRADI YAO KWA NJIA ZA MKATO? Au urefu wa kamba yako ni kuhakikisha ZANZIBAR inakuwa DUBAI ya AFRIKA at the EXPENSE of the MAINLAND huku wewe ukiwa Mmiliki mkuu?

Urefu wa kamba yako ni ipi Mheshimiwa RAIS?

Je, UREFU wa kamba ya wakurugenzi na wakuu wa wilaya ni upi?Je urefu wa watendaji katia na wa mitaa ni upi?Je urefu wa kamba ya watumishi wa afya ni upi?Je urefu wa vijana wasiokuwa na elimu wala ajira ni upi?Je urefu wa kamba za Majambazi na waporaji ni UPI?

Tunaongelea kila mbuzi kula urefu wa kamba yake.Je urefu wa kamba za wakuu wa mikoa ni upi,Urefu wa kamba yako ni UPI MHESHIMIWA RAIS.

Kila mbuzi atakula urefua wa kamba yake lakini vipi kuhusu wale mbuzi ambao hawajafungwa kamba ambao wanao uwezo wa kwenda kokote na kula kokote? Je, wale kila mahali? Wafyeke mapori na Misitu kwa sababu wao hawajfungwa kamba?

Tufafanulie kauli yako Mheshimiwa RAIS labda wewe ni Mmmakunduchi sisi wabara hatujui kiswahili

Mama Samia, Mawaziri wako hawatakaa wa kuheshimu kama hutawafanya waache kula urefu wa kamba yao badala yake wawatumikie wananchi. Manaibu waziri na Makatibu wakuu hawatakubali kukupa heshima unayotak iwe ya kitaasisi au ya binafsi kama wewe mwenyewe hutojiheshimu.

Kama unataka kuheshimiwa anza kwa kujiheshimu na kuwaheshimu wengine

Wasalaam

PBK
 
Umeandika ukweli mtupu ndio maana taasisi au kampuni huwa inapigana kufa kupona kutochafuka kupitia mtumishi wake (code of conduct) huwa zinajieleza kifasaha kabisa.

Kama mkuu wa taasisi hapendwi moja kwa moja taswira nzima huiwakilisha taaisis husika sio mtu mmoja.

Atoaye ajira kwa kiongozi wa taasisi kubwa hapo Tanzania ni wananchi lakini hawana nguvu yoyote kumchukulia hatua kama zinavyoelekeza sheria za kazi na utumishi kwa watu wengine.....hiyo sio sawa.

inatakiwa sasa wananchi wakithibisha mtu fulani waliyekasimu madaraka hatoshi utaratibu uwepo mara moja kumwondoa maana wanaumiza wananchi kwa maslahi yao huku wakisingizia wanaleta maendeleo yasiyoonekana, maisha kuwa magumu, mfumuko wa bei, ufisadi kuongezeka, matumizi mabaya ya madaraka na uonevu unaozidi uvumilivu.
 
Rais Samia,

Ukweli ni kwamba kama kiongozi hajiheshimu hastahili kuheshimiwa.Hata kama kiongozi huyo ni wewe.

Kila kiongozi kwa nafasi yake ni Taasisi.Kama anadharaulika basi hata taasisi anayoongoza itadharaulika.Hakuna namna ingine yoyote.

Mh. Samia, wewe ni Rais wa nchi haijalishi umeingiaje madarakani unao wajibu kwa watanzania na ni lazima utimize wajibu huo.Kauli na matendo yako lazima viakisi nia na wajibu huu.

Jana katika mazungumzo yako na viongozi wako ulisema wazi kwamba Kuna migongano ya maslahi mawaziri wakigomea safari na kugombania maslahi. Hio ni aibu yako na serikali yako.Hiyo ina akisi kwamba aina ya viongozi ulio nao ukiwamo wewe wamejikita katika kutumbua kodi za wananchi.Ulikiri wazi kwamba mawaziri wako wanakula pesa za miradi mpaka zinaathiri miradi ya kuwaletea maendeleo wananchi.Kukiri kwako kuna maanisha kwamba unajua na umeamua kuwacha hali hio iendelee.

Mh. Rais jana umesema kila mbuzi ale urefu wa kamba yake unajua maana ya msemo huo? Huku barabarani tafsir yake ni kwamba sasa tutafuta namna ya kurefusha kamba zetu, tutafuta namna ya kula. Kuna ambao hawana pesa za safari wala hawana wakandarasi wanaotaka kuwapa 10% ili wapate vitalu vya kuwinda,na miradi ya barabara na Ujenzi wa shule za COVID. Mheshimiwa Rais urefu wa kamba unaozungumzia kama RAIS ni kuhalalisha UFISADI, RUSHWA na UNYONYAJI.

Swala langu kwako Mheshimiwa RAIS je Kamba yako ina urefu gani? Ni urefu wa kuweza KULA 10% za MIKOPO NA MISAADA KUTOKA IMF maana umetetea sana mikopo na Misaada au kamba yako urefu wako ni KUYAPA MAKAMPUNI YA KIARABU MAENEO WAWEKE MIRADI YAO KWA NJIA ZA MKATO? Au urefu wa kamba yako ni kuhakikisha ZANZIBAR inakuwa DUBAI ya AFRIKA at the EXPENSE of the MAINLAND huku wewe ukiwa Mmiliki mkuu?

Urefu wa kamba yako ni ipi Mheshimiwa RAIS?

Je, UREFU wa kamba ya wakurugenzi na wakuu wa wilaya ni upi?Je urefu wa watendaji katia na wa mitaa ni upi?Je urefu wa kamba ya watumishi wa afya ni upi?Je urefu wa vijana wasiokuwa na elimu wala ajira ni upi?Je urefu wa kamba za Majambazi na waporaji ni UPI?

Tunaongelea kila mbuzi kula urefu wa kamba yake.Je urefu wa kamba za wakuu wa mikoa ni upi,Urefu wa kamba yako ni UPI MHESHIMIWA RAIS.

Kila mbuzi atakula urefua wa kamba yake lakini vipi kuhusu wale mbuzi ambao hawajafungwa kamba ambao wanao uwezo wa kwenda kokote na kula kokote? Je, wale kila mahali? Wafyeke mapori na Misitu kwa sababu wao hawajfungwa kamba?

Tufafanulie kauli yako Mheshimiwa RAIS labda wewe ni Mmmakunduchi sisi wabara hatujui kiswahili

Mama Samia, Mawaziri wako hawatakaa wa kuheshimu kama hutawafanya waache kula urefu wa kamba yao badala yake wawatumikie wananchi. Manaibu waziri na Makatibu wakuu hawatakubali kukupa heshima unayotak iwe ya kitaasisi au ya binafsi kama wewe mwenyewe hutojiheshimu.

Kama unataka kuheshimiwa anza kwa kujiheshimu na kuwaheshimu wengine

Wasalaam

PBK
Mkuu

Wala usisumbuke na maswali hayo tayari ameshatoa majwabu ya maswali mengi yaliyoyokuwa yakiwasumbua watu kadhaa. Kuna wakati alianza kugomba kwanini mnadai ufisadi na rushwa vimerejea kwa kasi..............lakini katikati ya safari akabaini ni kweli ndio maana akasema kila mtu hula kwa urefu wa kamba yake; na kwamba lakini wasipiitilize kula hadi wakavimbiwa.....hivyo wajipimie kiasi wasije wakagundulika na wananchi wakashituka!!!!

Tanzania=76=13=4=even
T-20=2=even
Financial position-Success
Business growth-positive if hardworking is the choice
Health status-complex and marred with pulmonary complications to medium and aged prominents
Way forward-brilliant after blackout lapse
Political outlook-scrambled for justice
 
Back
Top Bottom