Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,413
- 31,403
Irene Isaka alitetea mswada kama ulivyoandaliwa, alifanya kazi yakeMswaada mpaka Kuwa Sheria unapita Kwenye Mikono, Taaasisi Na Mamlaka kadhaa
Iwe kuna makosa au la, jambo muhimu ni kuwa alifanya kazi yake
Mswada ulipitiwa na waziri (serikali)
Mwanasheria mkuu akaungalia kisheria (serikali)
Bungeni alikuwepo kiongozi wa serikali (Waziri mkuu)
Bungeni walikuwepo wabunge wanaopaswa kuuchambua mswada(wengi ni wa CCM)
Mh Rais anapoita viongozi wa vyama vya wafanyakazi na kutatua tatizo pale pale tunapata ujumbe
Ujumbe ni kuwa wasaidizi wake hawamsaidii, wabunge wake hawamsaidii
Kama Irene angekuwa na msimamo tofauti na serikali, alikuwa na chaguo moja 'kujiuzulu'
Kwavile hakuna pingamizi la serikali Irene aliendelea na kutoa elimu kwa kile anachoamini na serikali inachoamini
Irene naona ni 'bangusilo' tu. Ilibidi atolewe kafara ili 'script' isomeke vizuri
Kama ingalikuwa kutumbuliwa ni suala la kuwajibika,kuna mlolongo mrefu wangetumbuliwa jana hiyo hiyo