Kama kichwa hazungumzi....

Kama kichwa hazungumzi....

Dopas

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2010
Posts
1,151
Reaction score
392
Nachukua nafasi hii kuwapongeza marais wastaafu Mzee Mwinyi na Mkapa... Nawapongeza kwa sababu wametoa hisia zao kuhusu taifa hili ambalo waliliongoza kwa miaka kumi kila mmoja wao. Wamezungumza kwa uchungu kwanini hili suala dogo namna hii ikuzwe bila sababu ya msingi hadi mauaji... Nimefurahishwa na hili... hasa kutoka kwao.

Wengi wamezungumza, na wataendelea kuzungumza... ila kama JK ambaye ni kichwa hafunui mdomo wake katika suala hili nyeti... tusemeje???? Kama kichwa hakina maamuzi.. kiwiliwili kinaweza???? sina zaidi...yetu macho....

Mungu atuepushe na balaa kubwa zaidi katika Nchi yetu...iliyokuwa chemchemi ya amani...
 
JK alilizungumzia suala la udini unaojitokeza lakini the way alivyo zungumza hakua serious kabisa alionekana kama mtu aliyeamshwa toka usingizini akajulishwa kuwa kuna vurugu za kidini ndipo akatoa maoni LAINI SANA kama vile naye anashangaa. This is too much. Mihadhara hii inatupeleka mahala pabaya sana. Bora amalize kipindi chake tuanze upya na Rais ajaye.
 
Kikwete anawaonea haya jamaa, hata maamuzi hana ...
 
Ukiona kobe kainama ujue anatunga sheria. Dr. Slaa aliahidi kwamba atahakikisha nchi haitawaliki, hadi mtu anafikia kutoa kauli ya namna hii inamaanisha kwamba kajipanga kwahiyo hili jambo siyo la kulikurupukia.
 
Back
Top Bottom