Majuzi tuu nilimsikia waziri wa maliasili/utalii Balozi Khamis Kagasheki akilalamika kuwa nchi ya Qatar inakataa kutoa ushirikiano katika kuchunguza wanyama waliobiwa hapa Tanzania na inagoma kuruhusu Tanzania kuingia huko ili kuwaona wanyama hao. Sasa kama ndio hivo kuna haja gani kuendelea na mahusiano na nchi hii iliyoshiriki kuiibia nchi yetu maliasili muhimu?
Mimi naona ni bora sasa tu declare diplomatic protest na kumfukuza balozi wao hapa nchini mana nchi yake imetugomea kwa hili.
Huu ni uzumbukuku,hao wanyama waliibwa na nani?
Hivi hakuna vyombo vya kimataifa vinavyofanya kazi kama hizo?
Hao askari wa Q na ndege ya jeshi iliruhusiwa na nani kuingia nchini na kukaa zaidi ya wiki wakisubiri wanyama?
Hivyo vibali si viliruhusiwa kutolewa?
Hivi Mhe.sana alipokwenda Q na kupewa mafuta na misaada mingi mingine aliwaibia Q?
Hivi ni ustataarabu gani uliotumika katika jambo hili au ni kudhalilisha nchi nyingine eti wezi!
Tumeshawaita Q ni wezi wakati kulikuwa na mawasiliano ya awali na kuwadhalilisha kiasi hicho na bado unataka kwenda kuwadhalilisha kule kwao hii inawezekana?
Vipi ukubali msaada mkubwa na wewe ukitoa unadai umeibiwa?
Hivi ni mara ya kwanza kwa TZ kusafirisha au kufanya biashara ya wanyama hai au kuwapeleka huko ughaibuni?
Hivi Q ni nchi huru tena yenye maendeleo lukuki,eti unaenda kuchunguza wanyama wako,hivi hiyo nchi ni Ranch ya taifa?
Ikiwa mimi kama mkulima mdogo siruhusu kuingia shambani kwangu hata kupita tu,sembuse kwa nchi kama Q tena kufanya uchunguzi?
Hivi usalama wa T au vyombo vingine vya dola vilikuwa wapi hadi hao askari wa Q wakaja nchini eti kuwaibia wanyama?
Tumeacha maswali mengi saaaaana ambayo hayana majibu timilifu eti tunakimbilia wanyama waliopelekwa Q
Hivi hao wachina waliotusaidia kukamata makontena yaliyojaa meno ya Tembo yaliyotoke TZ hayahitaji kukagiliwa tujue yametoka TZ DRC kenya Zimbabwe au SA.au ni njia ya kututoa kwenye mstari tusifuatie hayo meno?
Tuache kufanya mambo yetu kwa kunyanyasana namna hivi kama walivyonyanyaswa kina babu seya na familia yake.kwani yapo mengi machafu kuliko haya na tunajidhalilisha sisi wenyewe mbele ya jamii ya kimataifa kwani yaliyopita ni ndwele tugange yajayo.