Kama ni kweli hili basi nita mshauri huyu rafiki yangu aachane na biashara ya madini Tanzania

Chilemba wamela pamputi

JF-Expert Member
Jan 10, 2019
465
500
Habari wana jukwa poleni na majukumu ya hapa na pale,
Kimsingi sisi vijana ni wapambanaji sana katika kufanya shughuli mabalimbali za kutuongozea kipato, na hivyo hujikuta tuna fanya biashara nyingi za kitaifa na zile za kimataifa .

Pamoja na kufanya jitihada zote hizo lakini tume kuwa na changa moto za hapa na pale , nyingi wazo zimekuwa ni zile zitokanazo na mitaji, kushuka na kupanda kwa bei , ubora wa bidhaa na upatikanaji wa masoko ya uhakika kwa aajili ya biashara zetu.

Pamoja na changamoto zote hizo nilizo zieleza lakini wakati mwingine tunakutana na changa moto kubwa ambazo kimsingi ni zile ambazo husababishwa na mamlaka kwa maana ya watendaji wa ofisi za uma zinazo hudumia biashara kwa ujumla wake.

Sasa kwa nini nimesema nita mshauri rafiki yangu aachane na hii biashara ya madini tanzania ?

Kiukweli kuna rafiki yangu anafanya biashara ya madini kwa muda mrefu sasa tokea enzi hizo, lakini cha kushangaza kwa huu wakati tulio nao ni kwamba amekuwa ni mtu wa kulalamika saana akidai kwamba kume kuwa na usumbufu mkubwa saana na wakati fulani usio wa lazima pale mtu unapo peleka madini yako yahakikiwe ili uweze kulipia kodi na baada ya hapo upate vibali kwa ajili ya kusafirisha mzigo wako.

Hivi sasa ni mwezi wa pili ana lalamika kwamba toka wapeleke madini yao kwenye maabara yahakikiwe na hatua inayofuata ili mkurugenzi wa madini asaini ili wapate kuya lipia ime kuwa ni sinto fahamu, hii ni takribani wiki ya pili namsikia akilalamika kwamba tunakwenda ofisi za madini tuna ambiwa mkurugenzi yupo dodoma kikazi.

majuzi kati nilimsikia akisema wameenda wakaambiwa kwamba nyaraka zao zimesha pelekwa dodoma mkurugenzi akizisaini basi hatua nyingine zita endelea. Sasa sijajuwa ni hatuwa gani na zita chukuwa muda gani kwakweli.

Kiukweli nimekuwa nikimuonea huruma saana maana unapo amuwa kufanya biashara na ukawa na spirit ya kulipa kodi alafu unakwamishwa kwa muda wa miezi miwili hii ni hatari saana kwa biashara.

Nimewaza nimwambie aachane na biashara ya madini kama imekuwa ngumu kiasi hicho maana ni bora afanye biashara nyingine walau.

MWISHO
Najuwa kabisa nia njema ya muheshimiwa raisi ya kufanya kazi kwa bidii ndio msingi wake kiutendaji lakini pengine nia hii nzuri ya muheshiwa raisi inaweza kuwa ina hujumiwa na baadhi ya watendaji wasio waadilifu na wenye moyo wa kuto penda kutekeleza majukumu yao kama viapo vyao vinavyo jielekeza.

USHAURI WANGU KWA WATENDAJI
Jamani tumsaidie mkuu wa nchi kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na si kufanya mambo ambayo yanapelekea watu kuwa na taswira hasi na kukata tamaa.

Aksanteni na mbarikiwe

"Chilemba wa mela pamputi "Sent using Jamii Forums mobile app
 

Ligogoma

JF-Expert Member
Aug 27, 2010
3,313
2,000
Hata mie ninachoona kinachofanyika sasa ni kuiua sekta ya madini badala ya kuiboresha iwe ya faida!
 

The Sun-of-a Beach

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
981
1,000
Huo wanaofanya ni urasimu na hujuma dhidi ya wananchi.Pia,serikali inataka ifanye hiyo biashara yenyewe.Inachofanya ni sawa na cha maksai kuwapiga pembe ng'ombe wengine watoke zizini ili yeye ajinafasi na HAITAFANIKIWA!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom