G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,880
Mchungaji Msigwa Peter ambaye ni mbunge wa Iringa mjini (Chadema) na waziri kivuli wa maliasili na utalii ameshusha tuhuma nzito baada ya kuzihusisha serikali za juu za Tanzania na Qatar na ujangili unaoendelea chini, imefahamika.
Hayo aliyaeleza jana kujibu swali la kutoroshwa twiga wawili wakiwa hai kwenye uwanja wa ndege wa KIA.
Akiongea kwa kujiamini alipokuwa akihojiwa jana kwenye kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na kituo cha ITV, mchungaji Msigwa alidai hayo huku akitolea ufafanuzi swala la uchunguzi wa sakata hilo lililokwamishwa kwa makusudi na serikali ya Qatar.
Katika maelezo ya balozi wa Qatar nchini ambayo yalinukuliwa na mchungaji Msigwa, balozi huyo alitajwa kuizuia viza ambayo ilikuwa itolewe kwa jopo la wachunguzi kutoka Tanzania ili waingie nchini Qatar kuchunguza sakata hilo.
"Mimi siwezi kutoa viza kwenye jambo hili wakati hawa wanyama tumeuziwa na serikali ya Tanzania, sasa tunataka kuchunguza nini tena? Hii ni biashara baina yetu na serikali ya Tanzania" alisema balozi huyo.
Katika sakata hilo mchungaji Msigwa alidai kuwa biashara hiyo ya wanyama kati ya serikali za Tanzania na Qatar ni ya muda mrefu na inafahamika vyema na serikali zote mbili.
Aidha alisema kuwa watanzania wasahau fikra za kutoroshwa kwa wanyama kwani hakuna kitu kama hicho bali ni biashara iliyohalalishwa na viongozi wa juu wa serikali ya Tanzania.