Kama ikithibitika ilikuwa staged, Nape Nnauye aondolewe CCM maramoja!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Kama ikithibitishwa kwamba lile tukio la Bastola lilikuwa limepangwa na kwamba Askari wetu hawakuhusika, nashauri CCM wasimvumilie Nape kidogo, wamvue uanachama kwani kwangu mimi Nape atakuwa ni mbaya kuliko hata fisadi Lowasa au Mama Sofia Simba kama ni kweli yule hakuwa Askari wetu na kwamba tukio zima lilipangwa!

Binafsi mpka sasa sijaona ushahidi wowote ule wa Askari wetu kuhusika, hivyo kama watu wanweza kupanga tukio kama hili, hawa ni watu hatari na waliohusika wote wakamatwe. Bila ya kukausha hili swamp hakuna mahali tutaenda, ni bora kupoteza hata Majimbo 10 lkn kuwa na Chama kisichokuwa na watu wenye uwezo wa kufanya mambo kama haya, lkn kama nilivyosema kama ikthibitishwa kwamba Nape&Co. walipanga hili tukio, kama ni kweli walikuwa ni Askari wetu basi pia hatua zichukuliwe ...
 
Dah kisa rais mcheza movie na ss mkijua ni wacheza movie hvyo umebugi wewe na kina bashite wako hao mnaa ulikosa cha kuposti hvyo
 
Kufutwa uanachama hapana, kuna maonyo mengine mbadala hiyo adhabu ya mwisho na mimi binafsi nisingependa kuona kila mwanaCCM anayekosea adhabu iwe kuvuliwa uanachama, 2020 itakuwa shida sana kumuuza mgombea maana anakuwa na makundi mengi ya maadui, Hata Nape alistahili kuonywa kwa hiyo insubordination hapakuwa na sababu ya kumvua cheo (ningekuwa mimi ndio JPM).
 
Acha ujinga kijana! Mbona aliyetoa silaha anafahamika sana mjini? Mbona shughuli zake ziko wazi? Yule jamaa kawaida yake sana "kuringishia" kile kibastola chake; masela mjini wanamjua sana ni ajabu polisi kujifanya eti "sura yake hainekani kwenye video mpaka tufanya uchunguzi".

Nenda pale mjini uliza muuza magazeti yeyote wanamfahamu fika na vijiwe vyake ni maeneo hayo hayo. Chukua chokoraa yeyote pale mjini atakupeleka mpaka kijiweni kwake fasta na libastola lake utamkuta nalo. Msitufanye wajinga bwana.
 
Acha ujinga wewe ndugu, huyo askari wenu si aliendelea kubaki hapo eneo la tukio hata baada ya Maulid Kitenge kumzuia? Na Kamanda wa Polisi wa Kinondoni si alikuwepo pale? Kwanini hakumkamata? Acheni ujinga bana..

By the way, Sizonje kakiri kuwa hilo kosa lilifanywa na mtu mmoja na wala siyo serikali nzima, ajabu anasahau kuwa alimtuma mwenyewe 'akampoteze' Nape...yeye si ndo mzee wa kutishia kupoteza watu???
 
Kufutwa uanachama hapana, kuna maonyo mengine mbadala hiyo adhabu ya mwisho na mimi binafsi nisingependa kuona kila mwanaCCM anayekosea adhabu iwe kuvuliwa uanachama, 2020 itakuwa shida sana kumuuza mgombea maana anakuwa na makundi mengi ya maadui, Hata Nape alistahili kuonywa kwa hiyo insubordination hapakuwa na sababu ya kumvua cheo (ningekuwa mimi ndio JPM).


Ukiniuliza mimi ni bora ubaki na watu wachache waaminifu na kuliko kuwa na watu wengi ambao huwezi kuwaamini!
Binafsi nimesikitishwa sana lile tukio la Bastola na bado siamini kama Askari wetu wanaweza kufanya vile, kuna maswali mengi kuliko majibu!
 
Wewe ukitazama hizo video clips unaona limepangwa au la? Kwani askari hawawezi kupanga tukio? Nani alikuwa kwenye ile gari iliyoi-block gari ya Nape kwa muda? Na kwa nini hakushuka na hakutaka aonekane mpaka Nape alipoenda kuongea nae?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom