Kama aliyemuonyesha Nape bastola siyo askari, basi.......!!

the deadline

Member
Sep 26, 2013
62
106
Machi 23 mwaka huu. Aliyewahi kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo. Na mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye, alionyeshewa silaha (bastola) na mtu aliyedhaniwa kuwa ni skari aliyevaa nguo za kiraia. Akimzuia Nape kufanya mkutano alioupanga, akimuamuru kuingia ndani ya gari na kuondoka.

Tukio hilo, lilitokea baada ya Nape kutaka kufanya mkutano na waandishi wa habari, akitaka kuwaelezea kilichotokea kwenye uvamizi (na watu wasiojulikana), katika studio za kituo cha Clouds FM; baada ya uchunguzi kufuatia ripoti zilizokuwa zimemfikia ofisini kwake.

Mkutano aliouandaa kuufanya kwenye hoteli ya Protea, iliyopo jijini Dar es Salaam, lakini ulikumbana na vikwazo, vilivyochangia kutofanyika kama ulivyopangwa.

Machi 17 mwaka huu, saa tano usiku katika kituo cha kurushia matangazo cha Cloud FM kielezwa kuvamiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Ingawaje mpaka leo ukweli wa kuhusishwa Makonda na tukio hili haujajulikana kiundani.

Baadaye Serikali kupitia kwa Waziri wake Nape, ikaunda tume ya kulichunguza suala hilo.....majibu ya ripoti ya uchunguzi, pamoja na maelezo ya Mkurugenzi wa Vipindi Clouds Media, Ruge Mutahaba; ndiyo yaliyochangia kuenguliwa kwa Waziri Nape, akiwa kwenye ziara ya kikazi mkoani Arusha.

Kwani kwa mujibu wa maelezo ya Ruge kwenye kipindi cha Clouds 360, kinachorushwa na kituo hicho-hicho; alisema wazi kile kinachomuunganisha Makonda moja kwa moja na tukio hilo, kuonyesha kuwa alihusika. Ambapo Ruge alisema:

“Ijumaa saa tano usiku nikapigiwa simu na Ofisa wa Rasilimali Watu wa Clouds kuwa, Makonda amekuja ofisini na askari wakiwa na bunduki. Mlinzi hakusita kumruhusu aingie maana amemzoea, ila alishtushwa na askari wale waliokuwa na bunduki,” anaeleza Ruge kwa ujasiri mkubwa na kuongeza:

“Nilimwambia mlinzi aende juu studio aone kuna nini, na alipofika alimkuta Makonda akichukua mkanda kwenye ‘flash’ kisha akaondoka nayo. Hakuna kijana yeyote aliyepigwa usiku ule, lakini tatizo ni namna tukio zima lilivyotokea.”

Bado kwenye mwendelezo wa maelezo ya Ruge, anazidi kutanabaisha na kumweka matatani zaidi Makonda; kwa kumhusisha moja kwa moja na uvamizi ule anaposema:

“Makonda alikuja pale na askari, baada ya kuona kipindi chake hakirushwi. Hivyo ni kama alikuwa akihoji kwa nini hakijarushwa?” Anamalizia hivyo Ruge, kwenye maelezo yake yanayoonyesha ni jinsi gani alivyo na uhakika na tukio lile. Lakini hata katika hilo, upelelezi na uchunguzi wa Jeshi la Polisi umekuwa bubu.

Ndipo sasa, Nape alitaka kulizungumzia suala hilo kwa ujumla wake ikiwamo sintofahamu ya kutumbuliwa kwake; kukaibuka vikwazo.

Vikwazo ambavyo ni pamoja na, mtu huyo aliyedhaniwa kuwa ni askari. Akimtolea Nape bastola, jambo lililomfanya Nape kuahirisha mkutano ule japo kinguvu. Tukio ambalo lilishuhudiwa na waandishi mbalimbali, raia pamoja na baadhi ya askari waliovalia sare.

Kitendo hicho kwa nchi yetu, ambayo kiuhalisia imejitanabaisha na kujulikana kama ni kisiwa cha amani; kilisikitisha sana na militia doa Jeshi la Polisi na Serikali kiujumla, ambalo kufutika kwake si rahisi kwa simu za karibuni. Hasa ukizingatia lilifanyika kwa mtu ambaye ni mtumishi wa Serikali kama Nape.

Ambaye ukitazama ilivyokuwa, ni asubuhi tu ya siku hiyohiyo alikuwa Waziri; lakini masaa machache wadhifa wake ukaenguliwa na Rais John Magufuli, kwa sababu ambazo hazikuwekwa wazi.

Ni miezi takriban, sita hivi tangu kutokea kwa tukio lile la kihistoria, na Serikali kupitia Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba, kuagiza uchunguzi ufanywe kumbaini aliyedhaniwa ni askari; aliyethubutu kumtolea Nape bastola.

Majibu ya uchunguzi ule yamekuja na sintofahamu lukuki. Yaliyowaacha midomo wazi wananchi wengi kwa ujumla wake.

Waliohoji kwa asilimia kubwa uwezo, weledi, maarifa na umakini wa waziri kujibu maswali ya msingi na ya kitaalam. Kwa sababu, ndani ya majibu ya waziri Mwigulu kumeibuka maswali kedekede; huenda tofauti na ilivyokuwa kabla ya kutoa majibu.

Akilizungumzia hili, Waziri Mwigulu amesema kuwa, kumbe mtu yule (aliyedhaniwa ni askari) eti hakuwa askari kwenye kikosi chochote, miongoni mwa vikosi mbalimbali vya ulinzi na usalama hapa nchini.

Na kwamba, askari yule (feki) hajafahamika kabisa. Licha ya kwamba picha zake zipo, na zinaonekana wazi kwenye mitandao.

Isipokuwa inteljensia nzima ya askari polisi, imeshindwa kabisa kumtambua mtu huyo aliyejifanya askari na aliyepata ujasiri kutoka kusikofahamika; hadi akajitokeza mbele hali akijua wazi kama si askari; lakini akamtolea bastola Nape! Ni ajabu......nadhani haya yanatokea Tanzania tu!

Zaidi ya kusikitisha kwa matendo kama haya, lakini yanaleta kinyaa kuyaelezea. Kwani hata kama ukishindwa kuyaamini majibu ya Serikali, ndiyo yamekwishatolewa hivyo......na hakuna namna.

Lakini waweza kujiuliza ikiwa kama majibu haya, ni kweli yametolewa kitaalamu au ni katika kuwaridhisha tu wananchi? Ijapokuwa majibu yale yana mapungufu mengi tu.

Miongoni mwa mapungufu yaliyomo kwenye majibu ya Waziri Mwigulu, ni pamoja na: Kama mtu yeyote anaweza kujitokeza mbele ya halaiki na umati mkubwa kama ule, na kumnyooshea bastola kiongozi wa Serikali, na asiweze kujulikana wala kutambuliwa.

Je, kwa raia wa kawaida si itakuwa ni zaidi sana? Ukijiuliza, ni raia wangapi waliotishiwa, wakanyang’anywa mali za kwa vitisho tu vya wingi wa rundo la askari (feki) kama hawa?

Ni kweli Serikali imeshindwa kumbaini mtu huyo, au ni njia na mbinu tu za kujihami kutokana na tukio la aibu kama lile lililofanywa na askari wao? Kwenye tukio lile alikuwapo Kamanda wa Polisi Kanda ya Kinondoni jijini Dar es Salaam (wa wakati ule), Salome Kaganda, ambaye alishuhudia tukio lile.

Uchunguzi zaidi waweza kufanyika kuanzia kwa kamanda huyo, anaweza akatusaidia kumbaini huyo aliyejifanya askari. Wakati ukweli na kwenye majibu ya Serikali, kumbe hakuwa askari na hafahamiki!

Wananchi wanafika mbali kuhoji mambo haya. Hivi Jeshi la Polisi, kwa nini inteljensia ya ufanyaji wa kazi zao inashindwa kufanya kazi kwa uwezo sawasawa na kwingine?

Kwa mfano, inteljensia hiyo inafanya kazi kwa haraka na kwa kasi ya ajabu kwelikweli, pale tu inapobaini na kugundua kuwepo kwa mikutano; ile ya ndani na ile ya nje ya upande wa kambi ya upinzani pekeee. Lakini wakati huo huo, inteljensia hiyo inashindwa kabisa kufanya kazi kwenye mambo ya msingi; hasa yale yenye ushahidi wa wazi na vielelezo vyote vikiwapo.

Kama hili la huyo anayedhaniwa kuwa ni askari (feki), lakini pia kwenye sakata la uvamizi wa kituo cha Clouds FM; linalomhusisha zaidi Makonda. Eneo kama hilo, mara kadhaa Serikali imekuwa na kigugumizi haswaa! Tena cha ukubwani.

Mara nyingi sana, wabunge wa upinzani wamekuwa wakiibua uozo na madudu mengi yanayofanywa na baadhi ya viongozi waliopewa mamlaka, wakiitaka Serikali kuingilia kati kufanyia uchunguzi wa kina na kuchukua hatua kali za kisheria. Ila Serikali imekuwa na uzito fulani kuchukua hatua stahiki.

Hatimaye mambo mengi hasa ya kimaendeleo, yamekuwa yakikwama na kwenda mrama kila wakati; na kujikuta tukiitwa na kujulikana kama ‘taifa changa’ wakati ukweli ni uzembe ndiyo umelifikisha Taifa hili hapa lilipo; hasa katika ule mtindo wa kulindana zaidi, na kutokuwa na viongozi makini na wazalendo.

Serikali ikiendelea na mtindo huu wa kuwa na majibu mepesi kwenye maswali magumu, mambo mengi yatazidi kuibuliwa na kufunikwa tu kama hivi. Na ndipo kusudi la wengi kutaka msaada wa vyombo vya uchunguzi kutoka nje ya nchi litakapojulikana.

Matukio ya mara kwa mara ya kuripotiwa kupotea kwa baadhi ya wananchi, kuwepo kwa habari za kutekwa kwa baadhi ya wananchi na watu (wasiojulikana).

Wakati huo, kukiwepo na taarifa za kupatikana kwa miili ya binadamu ikielea kando-kando mwa fukwe za bahari ya Hindi na kwingineko; ni habari za kuchukiza na ni matukio ya kuhuzunisha sana, maana huenda ni miili ya wanao ripotiwa kupotea bila mafanikio ya kujua walipo. Ila ni kama bado pia Serikali inashikwa na kigugumizi kwenye eneo hili.

Umefika wakati sasa, wa Serikali na Jeshi la Polisi kujenga imani kwa wananchi wake.......ikiwa ni pamoja na utendaji wenye umakini mkubwa, pamoja na majibu ya kushibisha mahali ambapo pana utata na siri iliyofichika; mahali ambapo wananchi wanahoji na kuwa na shaka.

Nje na hapo, imani ya wananchi wengi itapungua kwa kasi ya ajabu ndani ya jeshi lao, lakini pia na Serikali nzima kiujimla.
 
Attachments

  • pic+nape.jpg
    pic+nape.jpg
    20 KB · Views: 26
hili la viroba vya maiti mkuu wa kaya hata lizungumza hata siku moja japo ni suala zito kitaifa na kimataifa.. Anajua wanaofanya hivyo
 
Mkuu ukweli inashangaza kuona serikali kupitia kwa taasisi zake nyeti za kiusalama kushindwa kutoa majibu ya moja kwa moja kwa mambo yenye utata ata yale yenye ushahidi wa kutosha kabisa kuwatia waharifu hatiani....

Sijui serikali hii inakusudia kutupeleka wapi coz kila siku hofu inakua kubwa sana kwa wananchi, matishio kwa usalama wa raia yamekua mengi na imani ya wananchi kwa taasisi zetu za kiusalama imepungua kwa kiasi kikubwa.
 
watu wasiojulikana
 
Inatia aibu kuzungumzia jambo ambalo ufafanuzi ulishatolewa, kama unamfahamu ungetujuza kuliko kuchapisha gazeti lisilo na maana
 
Mleta mada naomba nikupe pole maana Serikali yetu kwa sasa pamoja na watendaji wake hawako kwa ajili ya RAIA wa Tanzania bali kwa ajili ya MATUMBO yao,kwa hiyo hata Sirro atapata akili akisha retire.
 
Back
Top Bottom