Kama huna hakika, usimwache

Umenena mkuu..nilivunja mahusiano na mtu niliempenda sana bila sababu nikijiamini kwamba atarudi tuu..
..kilichofuata ni historia..sintorudia tena kosa kama hili..

Aisee pole sana hiyo inaumaga. Wakat mwingine huwezi kujua uthamani wa kitu hadi pale utakapokipoteza....
 
Umeandika haya kwa hisia sana mkuu.... ni kweli kabisa, wengine wakioneshwa kupendwa sana sijui ni nini wanaanza kuamini kuwa hata afanye nini hutoki kwake, wanasahau kuwa hata uvumilivu una mwisho wake, na mtendwa akishachoka amechoka kweli akiondoka hapo hakuna kutazama nyuma...shukrani kwa kutufungia mwaka vizuri ....
 
Wewe sio wa kwanza mkubwa, hili tatizo tunalo sana wanaume. Kuna jamaa yangu mmoja alikuwa na mwanamke mzuri hakuna(I mean very beautiful) na zaidi alikuwa ana tabia nzuri sana. Kila aliyekuwa anamwona alikuwa anataka kuoa kabisa.

Lakini jamaa alivyokuwa anamchukulia yule binti kama takataka fulani hivi. Na binti alikuwa anamuheshimu kama mume wake. Imagine tuko chuo anaweza akapiga simu akamwambia acha discussion nenda kalale, na binti anafunga vitabu anaondoka.

Kila siku ni cheating tu, na anaomba msahama anasamehewe tu. Siku moja wamegombana, jamaa akamwambia binti kuwa wanaume wako wengi, usije sema nilikupotezea muda!! That was the final word she needed, kesho yake jamaa kamwagwa. Kama kawaida akajua masihara, kuku wangu mwenyewe atarudi.... kumbe ndio nitolee, jamaa alilia karibu mwaka mzima, mpaka akamua kuokoka na kwenda kuombewa but It was too late....

Ukipata mwanamke anakuheshimu na anajua kusamehe, wewe mheshimu mara mbili kwa sababu hawapatikani kirahisi siku hizi

ila mie wa kike jamani!
 
Mim hua nikiachana na mtu hua sirudian nae hata kwa dawa hata anibembelezeje anidanganyaje kurudiana ni ngumu
Bora nimkubalie mpya kuliko kurudiana na wa zamani
 
Acha tu hii topic ni sensitive. Nilivumilia all ---- for 6 solid good years, baadae nikaona he is not worth me. I just disappeared and cut communication. Hata akisali novena sirudi aisee.
 
Acha tu hii topic ni sensitive. Nilivumilia all ---- for 6 solid good years, baadae nikaona he is not worth me. I just disappeared and cut communication. Hata akisali novena sirudi aisee.

6 good years. This happens to many, you are not alone. Watu huwa wanaamini atabadirika, lakini old habits die hard, if they ever die because in most cases they dont.
 
No issues, this applies to all of us. Out of curiosity, ulijiona keki dada yangu?

Hukujua kuwa dunia ni bakery isiyo na likizo??

tatizo ni kuishi na mtu kwa mazoea..na kupenda kubembelezwa...na huku Jf last seen ni 2010..aisee basi tu nisije nikaharibu siku yangu..
 
Kama kuna kitu ambacho huwa napata tabu kukielewa ni hiki cha mtu kumrudia X wake hasa baada ya kumuacha kwa vituko vya kila aina.


Kuna kesi moja ilitokea kati ya binti na jamaa yake. Walikuwa wapenzi kwa miaka karibu 10, kutoka form II mpaka baada ya kumaliza chuo na zaidi ya hapo. Siku moja jamaa akampigia simu binti anataka wakaongee sehemu. Binti akajibeba, probably alidhani anaenda kutangaziwa ndoa. Kufika kule baada ya maongezi mafupi, jamaa anamwambia binti, hataki tena uhusiano nae kwa sababu ameamua kuwa kuokoka na kuwa mchungaji!! Mara ya kwanza binti akadhani labda jamaa anatania, lakini kadiri maongezi yaliyoendelea, aka-realize kwamba the man is dead serious. Baada ya maongezi na kurudi nyumbani, binti aliumwa siku tatu yuko hospitali amelazwa.


Baada ya kutoka hospitali, akaamua kumtafuta jamaa. Bembeleza sana, jamaa katia ngumu. Akaamua mpaka kuwashirikisha wazazi, cause they had been together for so long mpaka wakawa wanajulikana hadi nyumbani kwa wote, lakini wapi. Binti akaamua basi na iwe hivyo. Kama kawaida, we unasema wa nini wenzio wanasema watampata lini. After kama miezi miwili hivi, inaonekana kuna jamaa alikuwa anasubiri tu chance yake. The other man hakuchelewa, kaenda kwa binti na proposal full. Binti nae akakubali, jamaa akaenda kwa wazazi.


The X kusikia tu watu wamepokea posa, akarudi fasta home(alikuwa amesafiri by that time). Moja kwa moja kwa binti anataka maongezi, akakataliwa hata nafasi ya kujieleza. Kama kawaida yetu wanaume, story zikawa nyingi, tumetoka mbali.... nimeshindwa kuishi bila wewe and so much blah blah. Binti alikuwa bado anampenda sana tu, you don't stop loving someone you have been with for 10 years + your first love. Lakini akatia ngumu, baada ya mwezi akaolewa na jamaa mpya na mpaka leo 5 years later they are together. Mwenzake nae, wa zamani ali-move on baada ya kukubali ukweli kwamba alikfanya blunder na hadithi za kutaka kuwa mchungaji zilikuwa hadithi tu za kutafutia sababu.


Kuna visa vingi sana vya aina hii, either ni mwanamke au mwanaume kumwacha mpenzi wake na baadae kuanza kujilaumu na kutaka kurudi tena. Tatizo ni nini? Ni kuwa na maono mafupi (short-sighted), au mazoea yakizidi mtu anaanza kuwa too comfortable na kuanza kuchukulia kila kitu kawaida tu (taking things for granted). Au ndio hisia za "wako wengi sana, nitapata mwingine wakati wowote", feeling of invincibility.


Personally nimekuwa kwenye mahusiano mara kadhaa na hata sasa nipo. Kitu ambacho nimekuwa nikisisitiza mara kwa mara ni kwamba, jitahidi usibabishe mahusiano kuvunjika kama huna hakika na maisha yako bila huyo mpenzi wako wa sasa. Ni kosa kubwa na pia it goes on to show how someone lacks good judgement when it comes to important decision in life. Huoni aibu kumrudia mtu uliyemwacha miezi kadhaa iliyopita(tena bora wa miaka) na kuanza kulia lia. What kind of a person are you?


If you can't live without her/him, make sure you don't leave him/her....
And if you are not sure, just make sure you don't leave him/her
....

... There is not such thing as true love, ni vile watu huvumilia na kuwa na mentality "Tumetoka mbali".
Nitaanzaje?..
"But kama hatukuzaliwa wote then hatutokufa wote na kama hatutokufa wote milele hatutokaa wote".

You may not be my LAST,my FIRST,or my ONLY,I loved before I'll love again
IF I love you now it is your present!!!!!!!!!

Heaven on Earth
 
Ukishamzoea mtu unamchukulia poa sana. Ukiwa in a relation endelea kujikumbusha feeling za mwanzon mlipoanza relation
 
Back
Top Bottom