Kama huna hakika, usimwache

MtamaMchungu

JF-Expert Member
Apr 10, 2011
6,899
2,000
Kama kuna kitu ambacho huwa napata tabu kukielewa ni hiki cha mtu kumrudia X wake hasa baada ya kumuacha kwa vituko vya kila aina.

Kuna kesi moja ilitokea kati ya binti na jamaa yake. Walikuwa wapenzi kwa miaka karibu 10, kutoka form II mpaka baada ya kumaliza chuo na zaidi ya hapo. Siku moja jamaa akampigia simu binti anataka wakaongee sehemu. Binti akajibeba, probably alidhani anaenda kutangaziwa ndoa. Kufika kule baada ya maongezi mafupi, jamaa anamwambia binti, hataki tena uhusiano nae kwa sababu ameamua kuwa kuokoka na kuwa mchungaji!! Mara ya kwanza binti akadhani labda jamaa anatania, lakini kadiri maongezi yaliyoendelea, aka-realize kwamba the man is dead serious. Baada ya maongezi na kurudi nyumbani, binti aliumwa siku tatu yuko hospitali amelazwa.

Baada ya kutoka hospitali, akaamua kumtafuta jamaa. Bembeleza sana, jamaa katia ngumu. Akaamua mpaka kuwashirikisha wazazi, cause they had been together for so long mpaka wakawa wanajulikana hadi nyumbani kwa wote, lakini wapi. Binti akaamua basi na iwe hivyo. Kama kawaida, we unasema wa nini wenzio wanasema watampata lini. After kama miezi miwili hivi, inaonekana kuna jamaa alikuwa anasubiri tu chance yake. The other man hakuchelewa, kaenda kwa binti na proposal full. Binti nae akakubali, jamaa akaenda kwa wazazi.

The X kusikia tu watu wamepokea posa, akarudi fasta home(alikuwa amesafiri by that time). Moja kwa moja kwa binti anataka maongezi, akakataliwa hata nafasi ya kujieleza. Kama kawaida yetu wanaume, story zikawa nyingi, tumetoka mbali.... nimeshindwa kuishi bila wewe and so much blah blah. Binti alikuwa bado anampenda sana tu, you don't stop loving someone you have been with for 10 years + your first love. Lakini akatia ngumu, baada ya mwezi akaolewa na jamaa mpya na mpaka leo 5 years later they are together. Mwenzake nae, wa zamani ali-move on baada ya kukubali ukweli kwamba alikfanya blunder na hadithi za kutaka kuwa mchungaji zilikuwa hadithi tu za kutafutia sababu.

Kuna visa vingi sana vya aina hii, either ni mwanamke au mwanaume kumwacha mpenzi wake na baadae kuanza kujilaumu na kutaka kurudi tena. Tatizo ni nini? Ni kuwa na maono mafupi (short-sighted), au mazoea yakizidi mtu anaanza kuwa too comfortable na kuanza kuchukulia kila kitu kawaida tu (taking things for granted). Au ndio hisia za "wako wengi sana, nitapata mwingine wakati wowote", feeling of invincibility.

Personally nimekuwa kwenye mahusiano mara kadhaa na hata sasa nipo. Kitu ambacho nimekuwa nikisisitiza mara kwa mara ni kwamba, jitahidi usibabishe mahusiano kuvunjika kama huna hakika na maisha yako bila huyo mpenzi wako wa sasa. Ni kosa kubwa na pia it goes on to show how someone lacks good judgement when it comes to important decision in life. Huoni aibu kumrudia mtu uliyemwacha miezi kadhaa iliyopita(tena bora wa miaka) na kuanza kulia lia. What kind of a person are you?

If you can't live without her/him, make sure you don't leave him/her....
And if you are not sure, just make sure you don't leave him/her....
 
Blue G

JF-Expert Member
Jun 20, 2012
5,337
2,000
yeah uko sawa MtamaMchungu wengi inatuponza kwa sababu tu ya kujiamini kupita kiasi na kujiona sisi ni wakamilifu hatukosei ila wapenzi wetu ndio wenye makosa,kuamini kabisa kuwa hatuna mapungufu na hivyo kuamini ukimwacha mwenzi wako atajutia tu na pia kuhisi kwamba u mzuri sana na wengi wangetaka kuwa na wewe lakini unakosa chance ya kuonja ladha tofauti kwa ajili ya huyo uliyenaye.
 
sister

JF-Expert Member
Nov 23, 2011
9,017
2,000
Mimi nachoona hawakupaswa kuwa mke na mme ndo mana wakaachana ili huyu dada akakutane na mme ambaye Mungu amempangia....
 
Me370

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
986
0
Hii inatokea kwa kuwa sometimes hawa viumbe wanachosha, ukiwa nae muda mrefu sana unaanza kutafuta something better. Inafika wakati ushaachana nae ndo unagundua kwamba una mmiss ile mbaya na huyo uliyemfikiria ata m replace wasn't that good.
 
Mr Rocky

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
15,188
2,000
Kwani kuwa mchungaji hakuruhusiwi kuwa na mke
Sema kama angekuwa padri hapo sawa ila mchungaji ilikuwa sababu ya kitoto sana na haikupaswa hata kuwa sababu ya kuachana
Inawezekana alizuzuliwa na mwingine kaona huyu hafai na kwenda kule nako kakuta hakufai kaona arudi
Ndo maana wanasema ukikataa wenzako wanasema utamuacha lini ili sisi tuchukue na ukiona mbaya kwako wengine wanasema nitampata lini
 
Hili tatizo tunalo sana wanaume, ukishapewa PAPUCHI basi unahisi kama umemaliza kila kitu, na usonge tena mbele. Lakini ukweli unabaki palepale, mwanamke ni zaidi ya PAPUCHI yake. Jamaa alikuwa hana sababu ya msingi basi tu.
 
MtamaMchungu ndo hapo nimeiona sababu yake ya kitoto sana na kaikuwa na msingi wala hakuna na sababu ya kumuacha huyo dada ila alishajiona amepata alichokitaka na kuna mwingine huko anamzuzua kajiona kidume ndo maana kaamua alichoamua
Ila kuja kushtuka alikataa dafu bila kujua kuwa embe ni tunda la msimu mambo yashaharibika na bibiye aliyemkataa kashapata wa kupata
 
Last edited by a moderator:

Himidini

JF-Expert Member
May 8, 2013
5,536
1,225
^^
Uko sahihi Mkuu, ila wapo wanaorudiana hata baada ya miaka 10.. Tukiacha hadithi za " MFADHILI " wapo wasio na misimamo thabiti katika mapenzi.
^^
 
Hornet

JF-Expert Member
Apr 29, 2013
23,939
2,000
Umenena mkuu..nilivunja mahusiano na mtu niliempenda sana bila sababu nikijiamini kwamba atarudi tuu..
..kilichofuata ni historia..sintorudia tena kosa kama hili..
 
Baraka Roman

JF-Expert Member
Feb 16, 2013
692
0
Ndo maisha yalivyo huwa tunakumbuka shuka wakati kumekucha

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
MtamaMchungu

JF-Expert Member
Apr 10, 2011
6,899
2,000
Umenena mkuu..nilivunja mahusiano na mtu niliempenda sana bila sababu nikijiamini kwamba atarudi tuu..
..kilichofuata ni historia..sintorudia tena kosa kama hili..

Wewe sio wa kwanza mkubwa, hili tatizo tunalo sana wanaume. Kuna jamaa yangu mmoja alikuwa na mwanamke mzuri hakuna(I mean very beautiful) na zaidi alikuwa ana tabia nzuri sana. Kila aliyekuwa anamwona alikuwa anataka kuoa kabisa.

Lakini jamaa alivyokuwa anamchukulia yule binti kama takataka fulani hivi. Na binti alikuwa anamuheshimu kama mume wake. Imagine tuko chuo anaweza akapiga simu akamwambia acha discussion nenda kalale, na binti anafunga vitabu anaondoka.

Kila siku ni cheating tu, na anaomba msahama anasamehewe tu. Siku moja wamegombana, jamaa akamwambia binti kuwa wanaume wako wengi, usije sema nilikupotezea muda!! That was the final word she needed, kesho yake jamaa kamwagwa. Kama kawaida akajua masihara, kuku wangu mwenyewe atarudi.... kumbe ndio nitolee, jamaa alilia karibu mwaka mzima, mpaka akamua kuokoka na kwenda kuombewa but It was too late....

Ukipata mwanamke anakuheshimu na anajua kusamehe, wewe mheshimu mara mbili kwa sababu hawapatikani kirahisi siku hizi
 
MtamaMchungu

JF-Expert Member
Apr 10, 2011
6,899
2,000
MtamaMchungu ndo hapo nimeiona sababu yake ya kitoto sana na kaikuwa na msingi wala hakuna na sababu ya kumuacha huyo dada ila alishajiona amepata alichokitaka na kuna mwingine huko anamzuzua kajiona kidume ndo maana kaamua alichoamua
Ila kuja kushtuka alikataa dafu bila kujua kuwa embe ni tunda la msimu mambo yashaharibika na bibiye aliyemkataa kashapata wa kupata

It was stupid na watu walimwambia, lakini si unajua tena sikio la kufa halisikii dawa. Yeye alijionea poa tu.
 
Last edited by a moderator:

farkhina

Platinum Member
Mar 14, 2012
14,576
2,000
Umenena mkuu..nilivunja mahusiano na mtu niliempenda sana bila sababu nikijiamini kwamba atarudi tuu..
..kilichofuata ni historia..sintorudia tena kosa kama hili..

Hahahhh shosti ulikua unatikisa kibiriti?

Btw pole sana....
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom