kwisha
JF-Expert Member
- Sep 9, 2021
- 1,788
- 5,027
Ilikuwa Alhamisi ya last week nilikuwa nasikia maumivu ya tumbo sana. Familia yangu wakanikimbiza hospitali maana hali yangu ilikuwa siyo nzuri, ndugu na jamaa walikuwa wanasubiri majibu kutoka kwa docters tu maana nilikuwa na hali mbaya.
Nilifika hospitali kwa bahati mbaya kama maelezo yao walivyonisimulia kuwa nilikufa kabisa wakanifunika na shuka. Sasa kilichonishangaza mimi kipindi nipo kitandani pale mimi nilihisi kuwa nimelala, yaani nimepumzika maana akili yangu bado ilikuwa inafanya kazi kabisa.
Nilikuwa nasikia vilio vya watu na kutambua huyu ni mama yangu, huyu ni fulani, ila kule kuongea au kutikisika na kufungua macho ndiyo nilikuwa siwezi kabisa.
Kwa maelezo yao walisema nilifanya kitu cha masaa matatu maiti yangu iko tu kitandani, walikuwa wanafanya utaratibu wakunipeleka mochari ndiyo nikafufuka tena.
Mpaka sasa hivi bado najiuliza kumbe mtu akifa akili yake bado inafanyaga kazi? Kweli ninaamini wangenipeleka udongoni ningejua na pelekwa udongoni, maana nilikuwa nafahamu na nilikuwa nasikia watu wanavyo lia.
Kama ndiyo kufa ni Mungu tu mwanadamu hawezi, watu wanazikwa huku wakijua kabisa wanapelekwa udongoni ila nguvu ya kukataa ndiyo hawana!