Kama hujayapitia haya maisha, kubali umekosa mengi

1. Tulikuwa tukicheza michezo kwa msimu, mfano ukiingia msimu wa kupunana Mabetri, utapenda. Hapo msosi kulika ni shughuli pevu na ukimpuna mwenzio haina kuondoka mpaka ummalize yote. Thamani ya betri la National ilikuwa tofauti na la ABC kitambo hicho, thamani ya betri lililobondeka hailingani na ambalo halijabondeka(Tuliamin ni Jipya). Hapo kwenye mabetri zilikuwa zinapigwa daily.

2. Monjo(Mbegu ya Sungwi iliyosuguliwa sawia mpaka inachongoka kama mshale mbele). Kwa wakazi wa Mwanza mtakuwa mnapajua vizuri Esso, miaka ya Tisini mwanzoni kulikuwa na hiyo Esso ingawa sijuagi mpaka leo maana yake, sasa sisi tulikuwa tunakwenda hapo Esso, tukiwa tumetokea Mabatin stendi hapo kwenda kupunana Monjo, kila mtu na ufundi wake wa kuifanya izunguke sana. Panatengenezwa dimba, yaan unakusanywa mchanga halafu unatawanywa katikati panakuwa na uwazi, unatafutw mfuko wa Rambo au Malboro enzi hizo tunaanza kushindana kuzungusha Monjo zetu, ukipigwa ukatoka nje ya ulingo umeliwa au ikisukumwa ikadondoka umeliwa, sasa kimbembe ipulizwe na upepo idondoke, mchezo ndio umeishia hapo.

3. Sarakasi, nilikuwa mtaalamu sana katika watoto wote, nilikuwa mimi na mdogo wake aliyetufundisha. Kuna muda ilikuwa inafikia tunafunga mtaa, hapo watu wamepanga mstari pembeni na pembeni wanatushangaa tunavyobinuka.
 
Pumzika kwa amani baba yangu. Alikuwa akitoka safari maana alikuw dereva wa kampuni ya sigara TCCL akifaika ata kama sipo lazima aniulizie sungusungu yuko wapi? By the way ilo jina sio langu ila matendo yangu ilibidi wanipe ilo jina maaa kwa walio zaliwa miaka ya 1987 kuendelea wanafahamu vzr shughuli ya sungusungu, bora ukamatwe na mjeda kuliko awa jamaa. Basi bwana mzee akifika home anataka nimpigie salakasi, mm ndo nilikuwa bwigwa wa salakasi nafikili wilaya nzima, basi nilikiwa napiga salakasi za mzunguku( nyuma) umbali wa dodoma mjini mpaka wajenzi. Ukimaliza mzee anakupa mia mbili, kipindi hicho mia mbili ya noti ni pesa kubwa nafikili nikama elfu mbili ya sasa. Pumzika kwa amani baba yangu uku ndugai ndo kwanza ameamia kwa masele.
 
Rip .. best dad

sisi tulikuwa tunatembea na magongo , kucheza kwenye kingo za makorongo, kuogelea kwenye mito dah ila mungu mkubwa alitulinda mno
 
Siku hizi mambo yamekuwa mengi. Watoto hawawezi kukutana hivyo. Siku hizi motto anatoka shule za Kiingereza saa 11 ana home work atakutana na wenzie saa ngapi? Halafu pia siku hizi kuna stori za watoto kutekwa, kuuawa na kuondolewa viungo, hivyo watu wanalinda watoto wao
hata kabint kangu kadogo kamepelekwa boarding na kakirudi kanashinda tuition nangalia hadi najicheka wakati ilikuwa shule ikifunguliwa unakunguta vumbii na ukifika hujasahau mnaendlea
 
Mkuu katika yote siwezi kusahau hii,kunasiku tulienda kuamia ndege wasile mtama.Tulikuwa kama sita hivi, shamba lilikuwa karibu na uwanja Fulani,Baadae akili ya kijinga ikatuvaa tukajigawa makundi mawili( watatuwatatu) .
Kila kundi likaenda upande mmoja wa uwanja,kila mmoja alikuwa na kombeo,sasa kila upande ukaanza kurusha mawe kwa kombeo kwenda upande pinzani,huku tukiona ni mashindano.Jiwe lilinipata kwenye maungio ya pua nusura upande mmoja wa pua ung'oke.Nina alama mpaka Leo.
 
Kwa kweli mengine sitaki hata kukumbuka, mm nawadogo zangu tulikuwa tunambembea na kamba chini kuna mto una kina kirefu ikidondoka hapo kama hujui kuogelea basi tena .unabembea mpaka ngambo ya mto ukirudi wezako wanaendelea kukusukuma bila hata woga.Mungu kweli ni mlizi wetu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom