Kama hii ni kweli... Basi ni KUFURU | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama hii ni kweli... Basi ni KUFURU

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kigarama, Oct 29, 2011.

 1. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2011
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mwandishi wa Habari Idrissa Jabir ameandika kwenye gazeti la mwanahalisi haya yafuatayo'

  1. Kuna mswada maalum kwa ajili ya mafao ya vigogo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) Zanzibar na familia zao unaandaliwa.

  2 Rais akifa. Kizuka (Mjane) wake alipwe pensheni sawa na mshahara wa Rais atakayekuweko madarakani kwa wakati huo

  3 Rais Mstaafu akifariki, watoto wake walio chini ya umri wa miaka 18 walipwe penseni sawa na mshahara wa Kima cha chini kwa wakati huo.

  4 Makamu wa Rais aliyefariki kabla ya kulipwa stahili zake, familia yake ilipwe stahili hizo kwa niaba yake.

  5 Kizuka wa Makamu wa Rais alipwe pensheni kwa miaka mitatu mfululizo kwa kiwango cha mshahara wa mumewe wakati akiwa madarakani.

  6 Makamu wa Rais akifariki, watoto wake walio chini ya umri wa miaka 18 walipwe pensheni sawa na mshahara wa kima cha chini kwa wakati huo.


  Jamani huyu ndiye mtoto aliyezaliwa kwenye ndoa ya CUF na CCM. Litakuwa toto shababy kweli kweli!!
   
 2. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #2
  Oct 29, 2011
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  It's our turn to eat!
   
 3. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Nilishakoma kushangaa mambo haya sikun nyingi maana sasa uamegeuka kuwa ni kawaida tu
   
 4. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #4
  Oct 29, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kaaaaazi kweli kweli!
   
 5. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #5
  Oct 29, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 21,995
  Trophy Points: 280
  Ngoja Chadema ichukue nchi, upuuzi wa namna hii hautokuwepo
   
 6. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #6
  Oct 29, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,990
  Likes Received: 2,649
  Trophy Points: 280
  Hivi hawa pro ccm mambo kama haya huwa hawayasikii/kuyaona?maana wao wanachojua ni kuitetea ccm tu hata kama wananyonywa,au wao hawana ndugu vijijini na sehemu zingine?
   
 7. Wed

  Wed JF-Expert Member

  #7
  Oct 29, 2011
  Joined: Mar 7, 2011
  Messages: 298
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 60
  Usikubali kabisa kurithika au kuchukulia ati ni kawaida. Ukizoea ujinga wa hawa wajamaa wanaoiba bila huruma, watakuchukulia kuwa nawe ni mjinga hivyo wataendelea kugawana hela zetu kana kwamba ni zao... Ndugu yangu Mpita Njia usikate tamaa.... Haki haiji bila kuipigania ... nakukaribisha kwenye mapambano ili 2015 mambo yaeleweke !!
   
 8. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #8
  Oct 29, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Basi waseme hiyo mishahara yao ni kiasi gani na wataje watoto wao wote PUBLIC sio waje kufa tubambikiziwe
  muhimu tujue hiyo misharaha ili tupime na kuona tunalipa kiasa gani? tatizo sio kulipa huo ni uungwana nchi nyingi ufanya hivyo
  lakini inajulikana ni kiasi gani za pesa kitakachilipwa na kwa nani?>
  hapo kwenye watoto wa marasi tuwe makini zaidi tunaweza kubambikwa na kulipa gost children
   
 9. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #9
  Oct 29, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mbona balaa tu?
   
 10. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #10
  Oct 29, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  ​CHUKUA CHAKO MAPEMA inaitwa
   
 11. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #11
  Oct 29, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Humu JF hakufai kabisa siku hizi. Watu wanaamua kutunga maneno ili kukashifu viongozi na serikali kwa ujumla. Hivi kweli maneno hayo yanatoka mdomoni mwa mtu mwenye akili timamu kweli. Unafurahi sana unapotajia CCM na CUF yaani unataka kuniambia umeajiriwa kwa kazi hiyo?. Halafu tunasema hatuwezeshwi na serikali au serikli haijali wananchi wake. Kama siku zote mtu anafikiri mabaya 2 hata kwake hawezi kujenga.
  "IRON BOYS ALWAYS TALKS ABOUT PEOPLE"
   
 12. Mbugi

  Mbugi JF-Expert Member

  #12
  Oct 29, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,488
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 160
  Mbona sijaona jipya hapo zaidi ya kuharmonize terms hizo zifanane na za bara? tafadhali naomba usome retirement benefit act for political leaders and that of civil servant ya 1999. na pengine soma sambamba na ile ya mafao ya majaji ya 2007.
   
 13. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #13
  Oct 29, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Don't support IRON BOYS like KIGARAMA, these were borned to talk about People
   
 14. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #14
  Oct 30, 2011
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,847
  Likes Received: 2,423
  Trophy Points: 280
  Hii kulipa watoto wa wakubwa mishahara inachangia kuwaharibu baadhi Yao.....najuwa huku bara...siku hizi wanalipwa Hadi posho baba Zao wakisafiri...yet baadhi bado wanafanya ufisadi
   
 15. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #15
  Oct 30, 2011
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  kuzungumzia watu ni kuzungumzia mambo binafsi kama vile anakula nini, anavaa nini au amemuoa/kaolewa na nani, lakini kuzungumzia matumizi ya fedha za walipa kodi huko si kuzungumzia mambo ya watu.

  Najua hata bara kuna sheria za kijinga kama hizi lakini sasa imekuwa kama ule mchezo wa ngamia na mwenye hema. Hivi kweli hawa watoto wa wakubwa walipwe posho sawa na mshahara wa kima cha chini cha mshahara kwa kazi gani wanayolifanyia taifa. Hizo fedha wanazaolipwa wazazi wao pamoja marupurupu yote na kutuibia kote bado na wao tuwalipe tena? HAPANA.
   
 16. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #16
  Oct 30, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  siye yetu macho nothing we can change
   
 17. G

  Godwine JF-Expert Member

  #17
  Oct 30, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  zanzibar imekuwa nchi kwa mujibu wa katiba yao mpya kwahihyo waache wafanye madudu yao
   
 18. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #18
  Oct 30, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Hii ndio past tense ya born?????
   
 19. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #19
  Oct 30, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  MAPENDEKEZO YA 'HAKI ZA MALIPO ENDELEVU KWA VIONGOZI WASTAAFU' NI SHARTI UWEKEWE 'WAJIBU' KWA UMMA UTAKAOGHARAMIA MALIPO HAYO KATIKA VIPINDI MBALIMBALI

  NI jambo dhahiri kabisa kwamba kokote uendako duniani, hakuna mahala ambapo mtu watu au kikundi chaweza kupewa haki yoyote ile bila ya kuhitajika kutekeleza mtiririko wa orodha fulani wa WAJIBU ili kuweza kuendelea kufaidi HAKI husika.

  Hivyo basi, endapo ni kweli kuna kitu chochote muswada mahala wenye malengo ya kuwashitiri viongozi wetu mara baada ya wao kuweka tamati kwenye utumishi wao HADI KUSTAAFU, basi hakuna shaka kwamba viainisho kwenye muswada kama huo ni sharti kwa VIHITAJIKE KWANZA KUKIDHI MISINGI FULANI (must first be QUALIFIED under very strictly observed rules - chini ya usimamizi wa taasisi HURU) kabla ya kutekelezwa hata kwa punje yake: kwamba hayo mapendekezo yatatekelezwa hadi pale tu ambapo;

  1. Huyo mwajiriwa wa UMMA imethibitishwa kimaandishi na takwimu sahihi kwamba alikua AKILIPA KODI ZOTE stahiki na kwamba wala hakuwahi kusaidia mtu au taasisi yoyote ile KULINYIMA TAIFA LETU kodi katika kipindi alipokua ofisini.

  2. Mwajiriwa huyo wa umma ni lazima ithibitike kwamba ni MTIIFU NA MUUMINI WA UTAWALA WA KISHERIA hivyo pindi kunapobainika kwake kuwahi kuwa ni kikwazo kwa dhana hiyo hapo juu na hata kusaidia kukiukwa kwa katiba, haki za binadamu na utawala wa kisheria ilhali nafasi na mamlaka aliyokua nayo ilikua ikiruhusu baya kuzuia kabisa au kukwepesha mazingira kama hayo basi kila malipo kwa jina lake kwenda kwake mwenyewe na au uzao wake MARA NNE YA KIMA CHA CHINI YA mshahara wa Mtanzania kwa kipindi cha sasa.

  Ila ikibainika kwamba kafaulu mtihani huu bila ya mwananchi yeyote kwa kipindi chochote kile kulithibitisha jambo hilo kwa kinyume chake, basi malipo hayo yazingatie misingi ya KIMA CHA CHINI YA MTANZANIA kwa wakati huo' si zaidi ya mara 8 yake.

  3. Mpaka pale ambapo itathibitika kuwa mhusika aliwekwa madarakani kwa NJIA ZA KIDEMOKRASIA KWA UHALISIA WAKE na UTAWALA BORA na kwamba katika vipindi vyote ofisini hakuwahi kuwa kikwazo kwa maendeleo ya misingi thabiti ya kidemokrasia ndani ya mipaka yetu.

  4. Kwamba wenye kupata faida zozote zile kwa jina la huyo aliyekua muajiriwa wa umma na ni sharti wakidhi kila kipengele cha miongozo hiyo hapo juu, ni uzao unaotambulika tu ndani ya ndoa ha ile siku ya mwisho wa utumishi wake huyu muajiriwa wa umma hadi pale ambapo maana ya familia kwa misingi ya baba, mama na watoto inakokomea.

  5. Kwamba kabla ya familia hizi kufaulu kwa kuandikiwa hundi nyingine yenye kuwaruhusu kuchotewa fedha za walipa kodi wengine nchini, ni SHARTI KUWEPO NA MAREJESHO JUU YA MAPATO HAYO NA MATUMIZI YAKE kuwekwa hadharani kila baada ya miezi mitatu kupita, kufanyiwa uhakiki wa mara kwa mara kwa kuzingatia misingi yote hapo juu.

  6. Kuwepo na sharti kwamba watu hawa au familia hizi, ama kwa pamoja au kwa mtu mmoja mmoja, zitaendelea kufaidi matunda hayo no kukoma kuendelea kuyafaidi matunda hayo PINDI WATAKAPOHIARI WENYEWE KUJIINGIZA ZOZOTE ZA KISIASA NA UONGOZI WA NGAZI ZOZOTE ZILE, kwa kuwa MISINGI YA KU-STAAFU masuala hayo ya kisiasa, uongozi au kuonekana kuegemea kikundi au chama chochote kile cha siasa, ndizo hasa zilizoleta UHALALI WA KUPEWA MALIPO YOTE HAYO.

  7. Kwamba sheria na taratibu zote zinazongoza akaunti hizi za waajiriwa wote wa umma wenye kupokea malipo ya ustaafu wa utumishi na yale yote yanayofanania zitakua zikipitiwa upya KILA BAADA YA MIAKA KUMI ili kufanya masahihisho na uboreshaji wake kwa kuzingatia misingi ya vipindi mbalimbali nchini.

  8. Kwamba ukiukwaji wa japo hata msingi wowote mojawapo hapo juu, rekodi zozote za shutuma za rushwa na ufisadi katika mali ya umma, udini, ukanda, ukabila, utabaka, haki za binadamu na utawala wa sheria, misingi ya demokrasia na kutokujitenga kiuhalisia na siasa ni sababu tosha kumpotezea sifa ya mafao haya huyu muajiriwa wa umma mstaafu na au uzao wake wenye kufaidika na taratibu hizi.

  9. Wakati wote ni muumini na mtetezi wa uwepo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania LAKINI katika sura na MUUNDO utakaoonekana ni vema na kukidhi mahitaji ya watu wa Muungano wetu huu katika vipindi mbalimbali ya uhai wa taifa letu.


   
 20. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #20
  Oct 30, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  UTITIRI WA THREADS DHAIFU ZENYE KUJIRUDIA MADA NA ZENYE KUJIKITA ZAIDI KWENYE TETESI ZIDHIBITIWE

  Kwa kweli inasikitisha mno kuona kwamba JF ya sasa, ambayo imetwaliwa na wanachama wa baada ya mauaji ya Igunga, kumetokea mabadiliko makubwa sana kutoka kwenye hadhi ya kuleta na kujadili hoja juu ya mada zenye tija kwa taifa hadi kufikia kwenye hadhi ya mazungumzo jikoni kujadili watu tu.

  THREADS 50 unazoona zikianzishwa hapa ubaoni ni zile chini ya 5 tu ndizo zinazoonyesha kusheheni CHAGIZO NA UCHOKOZI WA FIKRA; watu kufikiri kiundani zaidi na kuletea taifa ufumbuzi katika maoni murua kwa faida ya watu huko maofisini.

  Nadhani MODS wetu hawa wakipendezewa tu basi kuna uwezekano wa kubana nafasi kwa 'mada watu' na kupewa uwanja mpana zaidi 'mada hoja'. Ingawaje bado tu watu watajadiliwa tu lakini kwa kulenga zaidi hoja fulani na zaida zake kwa nchi basi.

  Kama mtu utakua umeangalia sana utagundua kama vile wenye kawaida ya kujadi hoja zai (mfano Mzee Mwanakijiji, Waberoya, CandidScope, na wengine wengi wa aina yao jamvini ni kama vile wamewapisha kimya kimya hili Jeshi Jipya linaloongozwa na watu kama vile Malaria Sugu, Rejao, Selemani, Omr, Wakigoma, FaisaFox na wengine wengi wa aina yao.

  Mara nyingi, utakubaliana nami kwamba idadi kubwa sana ya watu hawa huwa ni mwingi wa porojo porojo tu na kutafuta kule kushindana katika uanzishwaji wa THREAD hadi 6 kwa wakati mmoja ila ukifuatilia maswali anayoulizwa kila THREAD unakuta hayupo na pengi hana hata habari kwamba pindi uanzishapo mada ni sharti uwepo ndio mjadala upate kuendelea vizuri zaidi

  Tutarajie mabadiliko hapa jamvini na tutafute kujizuia na ile kasumba ya kile kinachotakiwa kuwa ni POST tu za kawaida chini ya mada iliokwishainishwa ubaoni na badala ya KUKIMBILIA KUZITUNDIKA ukutani kama madai mapya na kisha kubuka kwa utitiri wa TREADS ZINAZOFANANA ambazo hazi uwezo wa kudumu zaidi ya siku moja kabla haijafa.

  Ukitaka kuthibitisha ninachosema hapa utakuta kwa 5 ya 50 ya THREADS zilizoenda shule utakazozikuta humu tu huishi hamu ya kuzifuatilia na kuendelea kuchangia mawazo hata baada ya kupita miaka miwili mitatu hivi.
   
Loading...