MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,966
Jana kwenye kipindi cha kipima joto ITV kulikua na wadau kadhaa wa elimu walioalikwa kwa ajili ya kujadili upandishaji wa madaraja kwa wanaotarajiwa kujiunga na vyuo vikuu nchini. Kulikua na watendaji 2 wa TCU ambao walitambulishwa kama maafisa udahili wa tume hiyo.
Yaani mtu anaulizwa hawa wenye diploma waliopata GPA chini ya 3.5 wataenda wapi? Mtu anajibu kwamba eti sio lazima wote waende chuo kikuu, duh kama haya ndio mawazo yao tutegemee ubaguzi wa hali ya juu.
Mtu anazungumzia eti fursa za kusoma stashada na ajira zake ziko nyingi kwahiyo watu wasiogope, yaani mtoto wa maskini aliyesomea kibatari PCM kapata walao EEE anaambiwa kua hana sifa sio lazima aende chuo kikuu.Hatari sana.
Lingine wanaulizwa kwamba hawaoni kwamba huu utakua ni ubaguzi kua wanaosoma shule nzuri ndio watakaofaulu vizuri,akajibu kua mbona kuna shule za kata ziliongoza mtihani mwaka huu? Wangeenda kwenye mazingira ya shule hizo wajionee mazingira yalivyo na pengine ilikua ni kama bahati na sibu tu sidhani kama zitaongoza tena.
Kiongozi anadai kua haoni tofauti kati ya ufaulu wa arts na sayansi, zote sawa tu. Amesahau kua tatizo sio wanafunzi bali ni miundombinu ya shule zenyewe kama maabala na walimu.