Kama Hauna Connection, Pesa au siyo In Service Kuna Kozi Hautakiwi Kusoma

Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
31,983
64,012
Kuna watu tunafanya makosa kisha makosa yetu yanakua case study kwa wengine kosa langu lilikua nilipofika level ya degree nikaamua kusoma kozi moja hivi inaitwa Management of Social Development.

Wakati nafika chuo nilikuta hiyo kozi ina jina linaitwa Degree in Politics and Management of Social Development waliograduate kozi ikiwa na jina hilo walirudi chuoni kulalamika kwamba hilo jina 'Politics' linasababisha wasiajiriwe. Chuo kikaamua kuondoa jina 'Politics' na kubakiwa na 'Management of Social Development'

Baada ya muda nikiwa mwaka wa pili mwishoni ikaja kufahamika kwamba kiukweli tatizo halikua neno 'Politics' tatizo ni kwamba hii kozi haitambuliwi na 'Lawson' ( sina uhakika kama nimeandika sahihi ila ni mfumo wa mishahara na kupandisha ngazi kwa serikali) hivyo utumishi wanaona kua kumuajiri mtu aliyesomea hii kozi italeta shida kwa kutojua kiasi cha kumlipa na namna ya kupanda cheo.

Anyway, nikiwa mwaka wa tatu ikaja julikana pia kwamba hata kozi nyingine pale chuoni nayo haitambuliki na Lawson. Hii kozi ni ya uchumi ila nimesahau jina lake.

Wanafunzi wa kozi yangu na wa uchumi tukaungana na kwenda utumishi kufuatilia. Tulivyofika pale tukakutana na wanafunzi wa Mzumbe (Jina la Kozi nimesahau) na wao wana shida inafanana na yetu.

Utumishi wakasema wao hawahusiki twende Wizara ya Elimu, Wizara ya Elimu wakatoa jibu la watafuatilia. Baada ya hapo ikawa ni kurushwa huku na kule mpaka tukawa tunakaribia kuondoka chuo.

Kufikia hapo Utumishi wakawa wameweka banner kwenye ajira portal kwamba kwa yeyote aliyesoma kozi ya Management of Social Development akiingia ajira portal aiandike kama Community Development.

And then baada ya 2015 ile banner ikaondolewa, serikali ikasimama kuajiri, akachaguliwa Waziri mwingine wa elimu na bahati mbaya kila kiongozi huja na kuanza upya.

Mwaka huu niliitwa kwenye usaili DUCE nilivyofika katika kukaguliwa nikaulizwa 'Mbona cheti kina jina Management of Social Development?' hivi unajua ni aibu kiasi gani kuanza kuelezea ishu nzima?

But I did.

Mkuu wa ule usaili akaniambia "Umeidanganya system, siwezi kukuruhusu kuingia"
Nikakasirika kwakua sikua naongopa na sina sababu. Nikaondoka.

Baada ya pale sijakaa karibu na maswala hayo kwa muda leo nimelog in ajira portal nimekuta kuna posts za Administrative Officers zipo kwenye cartegory ambayo imo kozi niliyosomea.

Nikalog in nikaclick apply ikaniambia sina vigezo.

Hii kozi ingawa inasemwa haitambuliwi lakini mule darasani tulikuepo wanufaika wa mkopo, binafsi nilinufaika na mkopo. Yaani HESLB inaijua kozi inahitaji ada kiasi gani na kiasi cha stationeries ila Utumishi na Wizara ya Elimu hawaitambui.

In service niliosoma nao wamepandishwa cheo kwa kozi hii ambayo haitambuliwi. Mambo ni vururu vururu. Baba na mama wananiambia mi muongo sikumaliza chuo 😅😅😅

Yaani kwa tulioisoma hii kozi tunabakiwa na options chache;
  • Kusoma master au Kurudi kusoma kitu kipya
  • Kuajiriwa na taasisi za serikali au taasisi binafsi (Connection)
  • Kujiajiri 🤡 🤡 🤡

Anyway, kilichotokea kimetokea. Kama naweza kumpa mtu head up kabla hajadumbukia humu acha iwe hivyo. Kama una ndugu au mdogo mpe ushauri haswa inapofika muda wa kuchagua kozi. Inawezekana 'Industrial Relation' inasound poa ila kwa hapa Tz bila connection ikawa ni tatizo.

Naattach kozi zilizofundishwa kwenye hii kozi.

IMG_20210829_065808.jpg



IMG_20210829_065857.jpg



Update 17th April 2022

Katika tangazo la ajira lenye post ya Afisa Maendeleo ya Jamii II post location ikiwa ni Halmashauri ya Mwanga mtu ambaye amesoma hii kozi ameweza kuapply.

Post ni 1. Na tangazo ni la 31st March 2022,

Maoni yangu:
Katika hili tangazo kuna posts ambazo mtu aliyesoma Community Development au Social Welfare anaweza omba, nafikiri hizo posts hata aliyesoma Management of Social Development anaweza kuomba lakini bado utumishi hawaruhusu.

Update 5th May 2022:
Wizara ya Afya kupitia Sekretarieti ya Ajira imetangaza nafasi za kazi za 'Afisa Ustawi wa Jamii' mtu aliyesoma hii kozi ameshindwa kufanya maombi.
 
Tatizo letu kubwa ni kutokuwa na watu waliotutangulia pamoja na mihemko ya kkwenda chuo.

Yaani unaenda kusoma kozi ambayo huijui hata ukihitimu utakuwa nani yaani ni ilimradi tu mtaani wanajua uko chuoni.
Kweli kabisa wengine wakimaliza kozi wanaitwa ie wanasheria,wahasibu,madaktari.......
sasa huyu tumuite nani na kozi yake aliyosoma!!??
 
Daaaah,mtu kapambana miaka yote hiyo halafu analetewa longolongo kwenye ajira tena na taasisi za Serikali na Serkali hiyo hiyo ndiyo iliyoruhusu hizo kozi zifundishwe huko vyuoni,inaumiza sana
 
Tatizo letu kubwa ni kutokuwa na watu waliotutangulia pamoja na mihemko ya kkwenda chuo.

Yaani unaenda kusoma kozi ambayo huijui hata ukihitimu utakuwa nani yaani ni ilimradi tu mtaani wanajua uko chuoni.
Au siyo?
 
Bado wanapanga ila ni kwa system tofauti.

Zamani majina yalikuwa yanachukuliwa vyuoni, sasa hivi wanatuma maombi halafu wanapangiwa. No interviews.
Anyway sijasomea afya wala edu sitasema sana kwakua sijui mfumo wenu ila niliwahi ona hilo tangazo la mfumo ule kuvunjwa.
 
Mkuu kozi zingine ni shida kweli lakin pia kwa uzoefu wangu mm naona pia tatizo liko kwa wanafunzi wenyewe mnashindwa kusoma alama za nyakati..

Nyakati hizi si za kusoma ukitegemea 100% kuajiriwa. Somen mkiwa mnatarajia kutumia hizo kozi mtaani kuwaingizia vipato.

Ajira imekuwa ngumu na si kwa Tanzania tu hata nchi nyingine. mm nimepata ka-neema kadogo ka kudhurura nchin nyingi tu so naona watu wanavyo kula misoto.

Kuweni wajasilia Mali. Ajira zenyewe mishahara yake ya sasa hv mpaka usomeshe watoto wako shule nzur, mpaka ununue kiwanja angalau ata sinza, mpaka ununue gar litakalo endana na shule yako.. utasubiri Sanaaaaaa

Sana Sana ajira za sasa hv, wengi Wana ambulia kukopa arafu wakatwe kwenye mishahara. Jitahidin vijana mkitoka chuo mje na majibu mawili vichwan mwenu kuajiriwa au kujiajiri. Magufuri alitaman Sana Tanzania ya viwanda nadhan alitaman watz wengi wawe wamiliki si watumikishwa.
 
Back
Top Bottom