Kama hamtaki nimuoe binti yenu semeni tu, msininyanyase na nimewachoka!

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,949
119,212
Najua fika kuwa Wazazi husika huu UZI watauona au huyo Binti yao atauona na pengine kuwafikishia taarifa.

Tumeamua kuachana na Umalaya ( Uhuni ) na kuamua sasa tutafute Wenza wetu ili tuyajenge maisha halafu hapo hapo nyie Wazazi mnafifisha ndoto zetu.

Nyie Wazazi wa huyo Girlfriend wangu mmenitaka nitoe Mahari yenu huku mkanihoji maswali yenu na nikawajibu mkaridhika huku mkinihakikishia kuwa mambo yatakuwa mazuri.

Nimeshajiaminisha kuwa sasa karibuni tu naachana na ukapera huku nikianza kuwatambulisha wenzangu juu ya huu mpango wangu mara nyie Wazazi ( Wakwe wenye Roho mbaya ) leo ndiyo mmenitibua kabisa.

Members humu JF hivi ni halali kweli Wazazi wa Girlfriend wako baada ya kuwapa Mahari yao kisha wanakutaka uwape vitu vifuatavyo?

  1. Academic Certificate tena cha University na kilichokuwa certified?
  2. Birth Certificate huku wakisisitiza kuwa wanataka kuwe na picha ya Utotoni?
  3. ATM card ambayo iko active?
Mpenzi wangu utanisamehe tu kwani nia yangu haikuwa kuwaumbua Wazazi wako " live " hapa JF ila nadhani nimeona bora tu nijitoe mhanga ili niweze kuwasaidia Wanaume wengine labda wanaopata matatizo au kero kama hii yangu.

Hata hivyo nimeamua rasmi kuachana na Wewe na sihitaji tena kuwa na Mke hivyo kwa hayo mahitaji matatu ya Wazazi wako unaweza tu ukawaambia kuwa:

  1. Wakuruhusu uolewe na Chuo Kikuu.
  2. Picha za Utotoni wanaweza wakaweka zao kama wanazo.
  3. ATM card yangu ipo dormant huu mwaka wa tatu sasa.
Sikutaki tena na unaweza tu ukawaambia hao Wazazi wako wakutafutie Bwana Mimi hivyo Vigezo vimenishinda kwani sitafuti PASI ya Kusafiria bali nilikuwa natafuta Mke.
 
Hawataki uoe binti yao hao. Bila shaka wamekupima katika vipimo vyao na umeonekana kuwa umepungua.

Usukumani kule enzi zile kama wakwe watarajiwa walikuwa hawakutaki walikuwa wanakupangia mahari kubwa (mf. ng'ombe 50+ bila punguzo lolote). Sasa naona mbinu zimebadilika...

Ili kukata mzizi wa fitina wavulana "wajanja" walikuwa wanapita njia ya mkato kwa kumtandika mimba binti halafu wanaishia kulipa ng'ombe 10 au 5 badala ya hao 50. Sikushauri ufanye hivyo ila kama umependa kikweli endelea na hiyo interview ya wakwe.
 
Rafiki yangu pole sana,duuh!!! Wazazi wengine sijui vipi?? Warudishe mahari tu wamchukue binti yao.
 
k
Najua fika kuwa Wazazi husika huu UZI watauona au huyo Binti yao atauona na pengine kuwafikishia taarifa.

Tumeamua kuachana na Umalaya ( Uhuni ) na kuamua sasa tutafute Wenza wetu ili tuyajenge maisha halafu hapo hapo nyie Wazazi mnafifisha ndoto zetu.

Nyie Wazazi wa huyo Girlfriend wangu mmenitaka nitoe Mahari yenu huku mkanihoji maswali yenu na nikawajibu mkaridhika huku mkinihakikishia kuwa mambo yatakuwa mazuri.

Nimeshajiaminisha kuwa sasa karibuni tu naachana na ukapera huku nikianza kuwatambulisha wenzangu juu ya huu mpango wangu mara nyie Wazazi ( Wakwe wenye Roho mbaya ) leo ndiyo mmenitibua kabisa.

Members humu JF hivi ni halali kweli Wazazi wa Girlfriend wako baada ya kuwapa Mahari yao kisha wanakutaka uwape vitu vifuatavyo?

  1. Academic Certificate tena cha University na kilichokuwa certified?
  2. Birth Certificate huku wakisisitiza kuwa wanataka kuwe na picha ya Utotoni?
  3. ATM card ambayo iko active?
Mpenzi wangu utanisamehe tu kwani nia yangu haikuwa kuwaumbua Wazazi wako " live " hapa JF ila nadhani nimeona bora tu nijitoe mhanga ili niweze kuwasaidia Wanaume wengine labda wanaopata matatizo au kero kama hii yangu.

Hata hivyo nimeamua rasmi kuachana na Wewe na sihitaji tena kuwa na Mke hivyo kwa hayo mahitaji matatu ya Wazazi wako unaweza tu ukawaambia kuwa:

  1. Wakuruhusu uolewe na Chuo Kikuu.
  2. Picha za Utotoni wanaweza wakaweka zao kama wanazo.
  3. ATM card yangu ipo dormant huu mwaka wa tatu sasa.
Sikutaki tena na unaweza tu ukawaambia hao Wazazi wako wakutafutie Bwana Mimi hivyo Vigezo vimenishinda kwani sitafuti PASI ya Kusafiria bali nilikuwa natafuta Mke.
kwani binti mwenyewe anasemaje?na mahusiano yako na binti ni mazuri au naye anaungana na wazazi wake?
 
Back
Top Bottom